uyu jamaa anatuchanganya sana. sisi wengine hapa hatutaki hata kuiona sura ya rostam azizi, lakini tukija kwa mtikila, nashindwa kumdefine, ilikuwaje akaanza kumkopa Rostam pesa tena hela ndogo kama hiyo, alikuwa anajibembeleza nini?walikuwa kwenye mazingira gani? kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kinaendelea hapo? au walikuwa marafiki toka mda mrefu? najiuliza maswali mengi sana aisee. au mtikila aliona kuwa Rostam yuko kwenye ufa na kwasababu yeye ndo mpiga mabom, akaamua to take advantage of that loop hole, kwamba, nikimuomba hela lazima atanipa tu kwasababu ataogopa kuwa nisipompa mtikila hela, atanipiga mabom yake? au mtikila ndo inakuwaga zake to take advantage of the suspects?...mhhhh! mi sijui. kama yupo humu ndani, tafadhali mtikila tueleze vizuri, manake wewe ulimkopa hela rostam, kwani rostam anamiliki benk ambapo mlikutania? yaani ulimfuata ofisini kwake ukamkope hela wakati unajua kuwa yeye ni fisadi? hauoni hata aibu mtikila? jamani tumueleweje sasa huyu jamaa?
pamoja ya yote, nakupongeza kwa kuzila hela ambazo ni za kwetu. hata kama hautarudisha, si kosa kwasababu hizo zimejilipa zenyewe, ni zetu na wewe chukua chako hicho toka kwa Rostam. hahahaha.