Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,702
- 2,571
Ni muda mrefu Mtikila amelalamikiwa na wanasiasa wenzie wa upinzani kwa kuwazunguka na kutoa misimamo yenye utata, yaliyomtokea juzi baada ya kulipuliwa na RA imetoa picha kamili kwamba jamaa na yeye ni fisadi aliye jificha kwa kisingizio cha upinzani na uchungaji.
Haiwezekani upinge ufisadi halafu unufaike na ufisadi, hoja kusema kwamba alikopa na msaada ni dhaifu sana kwani zipo taasisi zinazokopesha na kwanini asiende huko kukopa, na mbona hakuwahi kusema kwamba wanaoshutumiwa mafisadi ni rafiki zake na anapata pesa kutoka kwao.
Mtikila ametuyeyusha kwa muda mrefu na kujifanya mtata katika kupigania maslahi ya nchi hii, kumbe ni mnafiki mkubwa, anatakiwa atuombe radhi watanzania badala ya kwenda mahakamani kupoteza muda wakati pesa amepokea na pia ahorozeshe ni wapi tena amekuwa akipata pesa na amepata jumla ya kiasi gani kutoka kwa hao rafiki zake anowaita mashetani na mafisadi kutuzuga. Kama atataka kuendelea na mapambano dhidi ya ufisadi arudishe pesa zote alizopokea kutoka kwa mafisadi.
Mtikila anatakiwa kutambua kwamba watanzania wanaelewa na wanaouwezo wa kupima na kuchukua hatua bila ya kwenda mahakamani, badala ya kujifanya hamnazo amrejee mungu wake na kuomba msamaha kuliko kuendelea kukimbia wakati nguo zimeshadondoka na aibu itampata zaidi kama ataendelea kukimbia.
Siasa za kibongo zinaonekana sio kabisa, jamaa amewaita sana magabachori kumbe anazunguka kwenda kuvuta mapene kimtindo! Jamaa tuendelee kuwakimbiza hivi hivi watatajana tuu!