TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Mtikila alivunjika 8 Ribs na alipata internal breeding na kusababisha damu kuingia kwenye njia ya hewa na kusababisha kifo chake mimi ni moja ya madaktari tuliokagua mwili wa rev. Mtikila ila alikua hana injuries zozote na tulivyoona kulikua hakuna mkono/mguu/kisigino wala korodani la mtu cause kama mkono wa mtu ni kuwa alikua assassinated but the deceased body passed all tests including gunshot, and whether he was hanged but he passed all test. Ninaomba uni pm number yako unipe your thoughts .
Vile vile ripoti ya polisi inasema hakuvaa mkanda...
 
akihojiwa kiongozi ambae nae alijeruhiwa amedai kabla ya Ajali kuna land cruiser ilipita mbele yao kwa spidi na ndio chanzo cha wao kupt Ajali
chanzo. ch10

my take: polisi msipuuzie kwan kwenye mitandao kuna kauli isemao huna haja kujiua taja ugonjwa wa mh it will happen.

[h=2]Familia yafunguka kifo cha Mtikila.[/h]
Hatimaye, familia ya Mchungaji Christopher Mtikila, imeibuka na kuelezea hisia zao kuhusiana na uvumi uliozagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya chanzo cha kifo cha mpendwa wao huyo aliyefariki dunia juzi alfajiri baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka akiwa njiani kutokea Njombe kuelekea jijini Dar es Salaam.

Mchungaji Mtikila ambaye hadi umauti unamfika alikuwa Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alifariki dunia katika ajali iliyohusisha gari alilokuwa amekodi aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 189 AGM, kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani. Taarifa ya Polisi ilieleza kuwa ajali hiyo iliyotokana na mwendokasi mkubwa, ilimkuta Mtikila wakati akirejea kutoka katika mikutano ya kampeni ya wagombea ubunge na udiwani wa chama chake mkoani Njombe.
Hata hivyo, taarifa mbalimbali zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kifo cha Mtikila kimejaa utata na baadhi yao kwenda mbali zaidi kwa kukihusisha na baadhi ya wanasiasa wakiwamo wanaogombea uraisi; kwa madai kuwa msimamo wa Mtikila kuhusiana na baadhi yao ndiyo chanzo cha ajali iliyomuua.

Baadhi ya mitandao ya kijamii imekuwa ikieleza kuwa marehemu Mtikila alifikwa na mauti hayo kwa kunyongwa, jambo lililoibua mkanganyiko kwa baadhi ya wananchi kuhusiana na kifo cha mwanasiasa huyo aliyekuwa mmoja wa wapambanaji wasiosahaulika katika harakati za kurejesha mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Hata hivyo, kwa kutambua hilo, familia ya Mtikila iliibuka jana na kuamua kuelezea kwa kina juu ya suala hilo kwa kile ilichodai kuwa ni kuwawezesha Watanzania wafahamu undani wake na pia kujua juu ya msimamo wao.

Msemaji wa familia hiyo, Victor Manyahi, akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam, alisema Mchungaji Mtikila alifariki dunia kwa ajali ya kawaida tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya watu, baadhi ya vyombo vya habari na pia kwenye mitandao ya kijamii.

"Mchungaji alikufa kwenye ajali ya gari ambayo kimsingi ilikuwa kwenye mwendo wa kasi wa takriban kilomita 120 kwa saa na bahati mbaya hakufunga mkanda, hivyo gari lilipopoteza mwelekeo na kupinduka, akatoka na kukandamizwa nalo,"alisema.

Akieleza zaidi, alisema wakiwa safarini, kuna gari lilitanua upande wao na dereva wa gari alilokuwa amepanda Mchungaji Mtikila, kwa kujihami akaamua kupeleka gari porini na kusababisha gari hilo kupasuka matairi ya mbele kabla ya kupinduka.

Manyahi alisema baada ya ajali hiyo kutokea, Mchungaji Mtikila alipata majeraha kichwani na gari lilimkandamiza kabla ya wasamaria wema kufika eneo la tukio na kumtoa.

"Mchungaji alibanwa na gari na kusababisha akose hewa... na kama angepatiwa huduma ya kwanza vizuri, pengine maisha yake yangeokolewa,"alisema na kuongeza:

"Inasikitisha sana kuona watu wanazusha mambo ya ajabu wakati ajali ile ilikuwa ni ya kawaida, licha ya kwanba imeleta maafa."

Akieleza zaidi, alisema wakati kunatokea ajali hiyo, hakukuwa na mtu yeyote mahali pa tukio na kwamba, hata waliokuwamo katika ajali hiyo wamethibitisha kwamba hakukuwa na mkono wa mtu.

"Nadhani wanaosambaza taarifa hizo za uongo wana sababu zao binafsi... huwezi kuhusisha watu katika tukio kama hilo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi," alisema Manyahi.

RATIBA MAZISHI
Katika hatua nyingine, Manyahi alitoa muhtasari wa ratiba ya mazishi ya Mchungaji Mtikila kwa kueleza kuwa kesho (Jumatano), wakazi wa jiji la Dar es Salaam watapata fursa ya kuuaga mwili wake kabla ya kuusafirisha kwenda kwao wilayani Ludewa, mkoa wa Njombe.

Alisema mazishi yatafanyika kati ya Alhamisi au Ijumaa wiki hii katika Kijiji cha Milo wilayani humo (Ludewa).

POLISI WAFAFANUA
Kufuatia kuzagaa kwa taarifa potofu kuhusu ajali ya Mtikila, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani chini ya Kamanda wake Jaffary Ibrahim, jana lilitoa taarifa kuelezea ajali hiyo na kusema kuwa uchunguzi wao umethibitisha kuwa ilisababishwa na mwendo kasi mkubwa na kwamba hata baada ya ajali, ilirushwa umbali wa mita 125 kutoka barabarani.

Kadhalika, taarifa hiyo ileleza sababu nyingine za ajali hiyo ni uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha; kutofunga mikanda ya usalama kwa marehemu Mtikila ambaye baada ya ajali alirushwa nje kupitia kioo cha mbele na pia ubovu wa gari, hasa mfumo wa usukani (steering system).

Taarifa zaidi ya Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wa daktari unaonyesha Mchungaji Mtikila alipoteza maisha baada ya kuvunjika kwa mbavu nane upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kumuondolea uwezo wa kupumua.

Kwa sababu hiyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewataka wananchi kuacha kutoa taarifa za uongo na uzushi pindi ajali na matukio mbalimbali yanapotokea na kwamba halitasita kuwachukulia hatua waenezaji wa taarifa potofu kwenye mitandao kwa mujibu wa Sheria ya Mtandao.
 
Mtikila alivunjika 8 Ribs na alipata internal breeding na kusababisha damu kuingia kwenye njia ya hewa na kusababisha kifo chake mimi ni moja ya madaktari tuliokagua mwili wa rev. Mtikila ila alikua hana injuries zozote na tulivyoona kulikua hakuna mkono/mguu/kisigino wala korodani la mtu cause kama mkono wa mtu ni kuwa alikua assassinated but the deceased body passed all tests including gunshot, and whether he was hanged but he passed all test. Ninaomba uni pm number yako unipe your thoughts .

Hakuna daktari bogus wa aina hii!
Ungekuwa daktari kwa ninavyowajua usingekuwa unaripoti kijiweni habari za ofisi! Bleeding unaandika breeding!
Wewe Utakuwa kishoka tu, wale wachunguzi wakuangalie na wewe pia kwanini unakwepesha kwa kutoa ushahidi wa uongo ili uchunguzi usifanywe? Kwa !maslahi ya nani?
 
Kauli hii imetolewa na uongozi wa chama cha UDP ,kuwa kifo cha mch mtikila kuna mazingira ya utata kufuatia nyenendo zake za hivi karibuni na mikutano Aliyoifanya mwenyekiti kwa kuwataja baadhi ya watu wakubwa katika uhusika wao na ufisadi nchini Hivyo basi tunaomba serikali na vyombo vya dola vya nje na ndani kufanyia uchunguzi tukio hili Source:clouds tv
 
Kwel watz tuna akili za hovyo kabisa hivi mtu amepata ajali alaf mtu mwenye akili timamu unasemaa anahusianisha na kauli za utata alizozitoa hizi karibuni kwel?
Watu wamekuwa wajinga kiasi hiki?
Haya embu wajaribu tushawishi kwa kuelezea uhusiano uliopo baina na ajal na matamko yake

Tufike mahali tuwe na fikra chanya sio kila jambo linahusianishwa na siasa tu, kama ndo hivyo wamkamate dereva ake sasa si yupo hai na hajakimbia yeye anaweza wasaidia huo uchunguzi ambao wanautaka japo nina hakika majibu yatakuwa tofauti na vile ambavyo wao wanataka yawe
 
mbona unatoa povu, acha uchunguzi ufanyike. Mtikila anapata ajali siku hiyohiyo babu kingunge anahamia ukawa. kuna nn hapo?

UDP kama nan watoe tamko hilo?
 
mbona unatoa povu, acha uchunguzi ufanyike. Mtikila anapata ajali siku hiyohiyo babu kingunge anahamia ukawa. kuna nn hapo?

Uchunguzi gani zaidi ya ule wa polisi ambao repoti yao imeshatoka? hivi kwenye nchi hii ukiwa mwanasiasa kifo ni exception kwako? Hivi ni kweli vifo vya wanasiasa ni political scoring board? Pumzika kwa amani mchungaji the true hero of Tanganyika.
 
Muwe mnafunga mikanda mnapokuwa kwenye magari la sivyo mtakufa na kuwasingizia majirani zenu kuwa "fulani kaniua kwa vile sikumualika kwenye harusi yangu"
Tokea serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, mambo ya umbea na majungu yamepamba moto na maendeleo yamekuwa yakififia kwa kasi ya ajabu sijui kwa nini. Kuna mwenye jibu anijuze?
 
UDP Inahusikaje Na Mtikila?? Mzee Cheyo Unawasikia MISUKULE Humu, Wanavyokuhusha Na Ujinga! Mbona Mnachachama Kudai Hilo Mtikila Tu!! Kuna Matukio Mengi Tu Yametokea!! Hamjatoka Na Kudai Uchunguzi!!!
 
Hakuna daktari bogus wa aina hii!
Ungekuwa daktari kwa ninavyowajua usingekuwa unaripoti kijiweni habari za ofisi! Bleeding unaandika breeding!
Wewe Utakuwa kishoka tu, wale wachunguzi wakuangalie na wewe pia kwanini unakwepesha kwa kutoa ushahidi wa uongo ili uchunguzi usifanywe? Kwa !maslahi ya nani?
Nakubaliana na wewe kabisa.Taarifa ya uchunguzi wa kifo kama hii, Ni taarifa nyeti kuweza kutolewa mahali kama hapa kwa mtu makini aliyepewa jukumu la kutunza afya za watanzania.Sitaki kuamini kuwa mheshimiwa Allen snr ni daktari pamoja na kujipambanua kuwa aliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu,Yaelekea hajui taarifa kama hizo zinapelekwa wapi na bila shaka hajui kuwa ni suala la kisheria linaloweza kumweka matatani.Nafikiri ni wale madaktari wetu fake wa BRN.
 
Back
Top Bottom