mie naona huyo mbwete hajakosea kitu chochote
Mie nimekuwa nikifundisha hapo open kwa kipindi fulani,kusema kweli elimu imekosa wasomaji,yaani ni vituko vitupu.Kwanza hamna maandalizi ya kutosha kwa wanafunzi,watu wanazima moto,matokeo yake ndo hao wanaotusainia mikataba feki mpaka taifa linaangamia,hawana intergrity hata kidogo.Walio wengi pal hawana msingi mzuri wa elimu wanarukia tu.
Mie naona imefika mda wa kuacha ubabaishaji,hii sio bongo flava kila mtu anajaribu,we need natural certificates not arfificial one.Lazima mtu ukae darasani usome kweli kama umekuja kusoma.Sawa utaibia mtihanio lakini utafika ofisini mambo yatakuwia magumu ndo maana unaona mashirika yetu mengi yanakufa kwa sababu ya ubabaishaji wa elimu zetu,watu wengi wanakuwa waongeaji tu kichwani hamna kitu
Sio lazima watu wote wasome,kazi ni nyingi na mtu unaweza pata maendeleo kama kawaida.