Mbwembwe za ndege zimeishia wapi?

Naomba data kwamba malaria imetokomezwa. Source isiwe Humphrey Polepole Wala Paul Makonda a.k.a Mkuu DAUDI BASHITE
 
Uko mbali na uhalisia, tunahitaji ndege tena sana,lkn si kwa utaratibu huu wa mtu mmoja kuamua

Kwahiyo utaratibu upi utumike? Suala la utaratibu na uhitaji wa ndege vina uhusiano gani?
 
Usichanganye mambo boss,walioweka taratibu za manunuzi walijua iko siku atatokea mjinga mmoja afanye yake,hata lugola yalimfika kwa kutofuata kanuni

Hapo ndipo unapojichanganya na kutoelewa jambo linalozungumzwa. Suala hapa ni utaratibu wa manunuzi au uhitaji wa ndege?
Tofautisha kati ya mabo hayo then utoe hoja zako Gosha
 
ila kwa wakati huu ni vigumu kupima mafanikio ya ndege, hata ulaya wanasema ni baada ya miaka 3 ndo usafiri wa ndege utarudi kama zamani ( kimapato) mfano shirika kubwa kabisa la Australia (Quantus) limeomba msaada serikalini wa dola Bilioni kumi, ili liweze kutekeleza shughuli zake
 
watu tuna ajenda mpya"nchi ya uchumi wa kati"kwenye mambo ya ndege tumetulia kidogo
 
Sijui kama wanatambua corona imeleta athari kubwa sana, hasa kwenye sekta ya utalii na vivyo hivyo usafiri wa anga, watu wanasahau haraka sana, na kupandisha uzi wa namna hii

Utalii upi umeathirika na Corona ?

ATC ilikuwa inabeba watalii kutoka wapi, MUMBAI ???????
 
Zimeshatosha vipi nawe unataka kuongeza zako! 😁
 
Corona imeanza juzi hebu tupe faida ya ndege zetu kuanzia 2016 hadi 2019 kabla ya corona.

Faida ipi wakati hatukua na ndege.. maswali mengine ya kijinga hivi usiwe unauliza uliza tu bila kufikiri
 
sasa wewe inaonekana unafurahia pale matatizo yanakumba mipango ya taifa!!! sasa hiyo ni tabia ya kihaini, kiuasi, na kizandiki
 
Sema kwa faida ya wachache,ni lini masikini anayehangaikia mlo mmoja kwa siku atapanda ndege?hata hesabu za manunuzi yake zimefichwa au we unazo?
Kwani pia sisi sote tuna magari kuna wengine wanayo wengine hawana,

Hakuna jamii wenye kulingana vipato, ndiyo maana pia kuna hotel za five star na lodge za buku tano kila mmoja anapata kutokana na uhitaji wake na uwezo wake,

sasa ukisema ndege hazimnufaishi masikini kwanza unakosea sana, mapato yanayopatikana kupitia shirika la ndege ndiyo yanaleta maendeleo kwenye sekta ya miundombinu mnajengewa barabara kwenye vitongoji venu, vijiji, kata, na mitaa ambapo masikini ananifaika kusafirisha biashara yake kwa unafuu, pia hapo hapo mapato ya ndege yanamfanya mtu masikini apate elimu bure, usiwe unafikiri chini ya kiwango waza kwa mapana
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu.
Na comment hii ifutwe.
 
Imeishia apo[emoji116]
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu.
faida ya watanzania wote ni pale bei itakapokuwa nusu au robo tatu ya mashirik mengine.
 
Kila jambo na wakati wake. Subiri wakati wa kampeni, litakuwa midomoni mwa wahusika hata kama hizo ndege zikiwa zimeegeshwa hakuna wa kuzipanda. Si ajabu akazitumia kupita nazo kwa urukaji wa chini ili watu wazione anapokwenda kufanya kampeni mkoa fulani, na mkusanyikoni kuongelea kuwa mliiona ndege, hatukuwa nazo miaka iliyopita.
 
Hiii biashara ilishafeli ni suala LA muda tuuu!! Ndio maana hata CAG haruhusiwi kugusa huko ni aibu
 
Stori ya ndege kwisha habari yake.Habari mpya midomoni mwa watendaji ni Tanzania kupanda daraja hadi uchumi wa kati. Sielewi maisha ya mtanzania pale pale, matembele pale pale. Nachukia hii dhihaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…