Chama ambacho hata viongozi hakina kamwe hakiwezi kuwa na mafanikio yoyote yale na pia chama ambacho kimekubali kutumika na chama kilichopo madarakani ili kukisaliti chama kikubwa cha upinzani nchini pia kitakuwa kinasuasua tu na hatimaye kujifia tu. Tangu tuanze kuisikia ACT ni zaidi ya mwezi wa tatu sasa, lakini hadi hii leo chama hiki kimeshindwa kutangaza safu yake ya Viongozi wa juu wa chama hicho huku wakishindwa kutoa hata sababu ya hali hii imesababishwa na nini. Kuanzisha chama si lelemama.