el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,074
Leo katika safari yangu ya Dar es salaam to Dodoma kama kawaida nikakata siti ya dirishani.Mara ghafla kama maombi yangu kama yalikuwa yanasikilizwa akaja mtoto mmoja mzuri sana sema alikuwa amedress kawaida.Na mimi nikasema yeees leo mpaka tukifike Dom nitapiga hata mashuti 50 On target nikaandaa vifaa vya mashambulizi sasa.
Kwa mbwembwe nikachomoa Iphone5 yangu niliyoipata kwa kuungaunga kama gia fulani ya kunipush kwa mtoto kushangaa demu nikaona katoa zake Iphone6 + wala hana hata habari na mimi.
Nikasema huyu manzi vipi mbona anataka kunipiga knockout mapema hivi wakati nafikiria hayo nikaona isiwe kesi niendelee kupata azam embe yangu kucheki tena demu kumbe alikuja na savanna zake kama mbili nikashindwa kutupa kiazam embe changu ikabidi nikimalizie.
Tumefika Gairo nikanunua maindi mawili nimpatie na yeye moja kumuuliza manzi katikisa kichwa kuashiria hataki.Kumcheki tena manzi akachomka Pringles zake akawa anakula taratibu na kuniacha mimi na mahindi yangu yamoto.
Nikaamua kufanya maamuzi magumu ya kulala kwa lazima maana kila mbwembwe niliyotaka kufanya alikuwa akinilipa mara mbili,kabla sijalala nikawa nafkiria tactic ya kuanzisha ili nipate hata namba nikamuona yupo zake na Ipad4 yake anaangalia video.
Kusema za ukweli nilimchukulia poa sana ndo maana nilitegemea kasimu changu kuwa kanawza kuanzisha move ya kumpata mwisho wa siku niliishia kuaibika simu yangu nikaificha kwa aibu na bado hata mambo sikupata.
Mbwembwe safarini hazifai.