Mbwana Samatta Man of the Match achemka kutema Ung'eng'e


Mwambie huyo
 

Acha zako mbona aliongea English safi kabisa kwanza?
 
Nia na madhumuni ya huu UZI sio kuuonyesha Umma kuwa Samatta hajui Ung'eng'e la hasha
ni kutizama njia ambaya Vijana hawa kupatiwa masomo ya Ziada hasa kozi za kingereza ili waweze kujieleza kwa watu na kupata marafiki kote duniani
Pia itasaidia kuepuka mikataba mibovu
hilo ndilo dhumuni la Uzi huu, Samatta ni mtu maarufu kwa sasa anatakiwa ajengewe kujiamini na huwezi jiamini kama lugha haipandi
ni vyema wapewe kozi hasa za lugha itawasaidia
akhsante kwa kunielewa
 

"Shukrani kwa nyerere alicheza utazani pele kuendeleza kiswahili mikoani na mbelembele tunamfagilia mzungu(ung'eng'e) wakati tuna shida tele kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele"--Langa(Apepe)
 
Naomba uache kuwa mtumwa wa akili yako huitaji kujua kiingereza kama kipimo cha ujuzi wa fani yako. Kinachohitajika hapa ni mawasiliano kukamilika. Samatta amejitahid sana na ameonyesha ikomavu alipoamua kuongea lugha yake mama.
 
Samata ni mzalendo. Wewe ulitaka alaximishe kuongea asichojua?. big up ms.
sawa inawezekana ni mzalendo lakini jua kwamba , mtanzania yeyote akiwa anaongea kiingereza ujue angalau ukungu wa kielimu kautoa , ingawa mbele tunakoenda haita kuwa hivyo , samantha hakusoma na ndiyo hivyo
 

Wewe lazima utakuwa kilaza unaona kujua kiingereza ndio kuwa professional. Hivi ukiangalia UEFA Champions League magazine wachezaji wote huwa wanaongea kimombo? Hivi mwbana akiongea Kiswahili una pungukiwa nini haya sio mashindano ya kuongea kingereza. Hii ni soka...Mijitu mingine bwana
 
Kiingereza na mpira wapi na wapi?hvi mwombeki wa simba na elimu yake ya marekani anamzidi nni samatta..?kujua lugha. Katika futbal ni uamuzi wa mtu tu.. kama unajuakuucheza hata mkalimani ataletwa..
 
Wwe unaejua kiingereza unacheza namba ngapi?kama vipi nenda kaojiwe wwe...!!
 
lugha sio taaluma/ujuzi-wachezaji kibao wa EPL wanahojiwa kwa lugha za kwao mfano ni mchezaji wa Man City Abbromovich mara kibao huzungumza lugha yao, Rais wa Brazil aliwahi kusema hataman hata kukisikia achilia mbali kujufunza kimombo

Hebu mwambie mkuu maana tumechoka na ushamba huu
 

MOM Samatta?No way,shoul have been Mrisho bana.
 
jamani nipeni matokeo mwenzenu nipo huku Israel haifa. Sijui lolote kuhusu mechi yetu na Uganda na nipo tumbo joto kweli. Ngapi ngapi?
 

Lugha ya taifa kwanza.
 

Weweee acha kuwa mtumwa wa lugha za kigeni, kumbuka mwacha mila ni mtumwa. Samata hongera kwa kuzingatia matumizi ya lugha yako.
 
Kuwa professional na kizungu hakuna uhusiano wowote, kwanza namsifu kwa kukataa kuongea kizungu. Hata maraisi wengine wakija hapa wanaongea lugha ya kwao hata kama kizungu wanakijua fika! Hapo kwenye Blue mwenyewe umeandika sivyo.....
 
Nampongeza samata kwa kuchagua kiswahili kwani ndio lugha yake. Uwezo wake mkubwa kusakata gozi inaonesha ujuzi na maarifa haitegemei kingereza. Samata bila kingereza ana elimu kubwa ya soka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…