Mbwana Samata wa Aston Villa hana tofauti na Yikpe wa Utopolo

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,834
Niwazi ligi ya uingereza ni mziki mnene na maji marefu Kwa mtanzania mwenzetu Mbwana samatta maana Hadi sasa Kwa kiwango anachoendelea kuonyesha pale villa park Hana tofauti na mchezaji kutoka utopoloni YIKPE !!

Ushauri samatta aombe kwenda kucheza Kwa mkopo katika ligi kama za uturuki ,ugiriki ,ufaransa na hata ureno maana huko nahisi kabisa atarudisha makali yake.

Lakini mpaka sasa ujio WA samatta katika EPL hauna tofauti na ujio wa YIKPE ndani ya UTOPOLO.
 
Dah sisi mashabiki zake tunampongeza kwa hatua alio fikia ata kama kiwango hakiko timamu, mwingine akija ataendeleza alipo fikia ndo mpira huo.

Harafu msimfananishe na raia za utoporo fc ambao wanaweza kushuka kucheza ligi za mchangani cup
 
Angalia hapa.

Alienda Mazembe akakuta kuna mtu ana namba, akampindua na kuimiliki namba.

Akaenda Genk akakuta kuna mtu ana namba yake tayari, akampindua akaimiliki namba.

Kwanini huoni kwamba hata Aston Villa ataweza? Ighalo na Samata kama watabaki ligi kuu wote wawili nina uhakika Samata atarudia mtindo wake.

Atapindua na kumiliki namba.
 
Angalia hapa.

Alienda Mazembe akakuta kuna mtu ana namba, akampindua na kuimiliki namba.

Akaenda Genk akakuta kuna mtu ana namba yake tayari, akampindua akaimiliki namba.

Kwanini huoni kwamba hata Aston Villa ataweza? Ighalo na Samata kama watabaki ligi kuu wote wawili nina uhakika Samata atarudia mtindo wake.

Atapindua na kumiliki namba.
Ila mpaka sasa Hana tofauti na zuchu WA wcb..ngoja tusubiri
 
Mna haki ya kukosoa Ila msimvunjie heshma Samata. Samata ni mchezaji mzuri ila yeye na timu yake wanapitia wakti ngumu ila anahitaji muda akae sawa. Samata ni fahari ya Tanzania, kufanikiwa kwake EPL Kuna fungua Imani kwa Mawakala juu ya wachezaji kutokea Tanzania.
 
Kama unafuatilia mpira utaelewa ninachomaanisha, msimu wa kwanza Ronaldo kwenda Man U haukua mzuri sana, baada ya hapo amekua moto.
Mkuu Ronaldo Wakati anafika man u alikua kinda mchezaji ambae bado alikua hajafikia kilele cha ubora wake so alihitaji muongozo mzuri ili afikie kilele cha ubora wake ,

Mbwana samatta amekua katika ubora wake Kwa takribani misimu mitano amefika katika ligi ya uingereza akiwa ameshafikia kilele cha ubora wake Kwa hiyo Aston villa wamemnunua sababu waliamini nimchezaji ambaye ataenda kuleta mabadiliko moja Kwa moja katika safu ya ushambuliaji lakini Hilo halijatokea pengine Kasi na mazingira ya ligi ya uingereza si rafiki Kwa style yake ya uchezaji ila sioni nafasi ya yeye kubadilika pale EPL...usilinganishe EPL na ligi ya Congo na ubelgiji mzee utakua unafeli mbovu kama utopolo
 
Tatizo Samatta ameikuta Aston Villa inapitia kipindi kigumu sana,
Samatta alichukuliwa kuiokoa Villa kushuka daraja,So ni kama alikua anacheza under pressure,hope akitulia atarudia makali yake,Ukijua umejua tu,ni kama ukijua kuendesha Baiskeli vile.
 
Umemvunjia heshima sana samata kumfananisha na mchezaji kutoka utopoloni. Tofautisha kushuka kiwango na kutokujua. Huyo Yikpe hajui mpira sio kwamba kiwango kimeshuka. Samata pia hajashuka kiwango ila hiyo ligi mpaka sasa kwake ni ngumu, na yeye sio wa kwanza kukutana na huo ugumu, kuna akina falcao, morata, shevchenko n.k wote hawa walitoka huko wa moto ila walipofika epl hamna kitu.
 
hata akishindwa poa tu ila ametutoa kimasomaso wtz.hiyo ligi wameshindwa akina macheda,saldado,pogba,guendoz nk we umemwona samata tu,? samatta mdogo wangu jipange msimu ujao ututoe kimasomaso,huyu mtoa mada ndo anakupa hamasa upambane uwaumbue wanaokubeza
 
Umri umri umeisha mtupa mkono, ni bora atafute ligi nyepesi nyepesi akamalizie soka lake
 
Back
Top Bottom