Mbwa daima si huwa na mmiliki wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwa daima si huwa na mmiliki wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dopas, Mar 27, 2011.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WanaJF salam

  Ninavyofahamu kati ya wanyama wafugwao, mbwa hufugwa kwaajili ya ulinzi. Mbwa mlinzi mzuri huwafahamu mabosi wake, kwa kawaida mbwa huwafahamu wakazi wote wa nyumba kupitia kwa bosi wake. Kama mbwa anakuwa rafiki wa kila afikaje nyumbani sio tena mbwa mlinzi, bali 'pet'.

  Ikiwa mbwa anambwekea mgeni na hata kumng'ata mgeni il hali bosi wake anatazama tu, wa kulaumiwa kwa kawaida si mbwa bali ni bosi wake.

  WanaJF wiki yote tumeshuhudia matusi ya UVCCM hususan yaliyoelekezwa kwa baadhi ya wazee wa chama chao. Lawama nyingi tumewatupia hao vijana kwa kukosa adabu hiyo. Hapo hatuzunguzumzii waliyosema kuhusu upinzani hasa Chadema. Pengine tungeona hiyo ni kawaida, tumezoea.

  Kweli matusi wanayowaelekezea wazee wao hadharani ni bure? Hiyo UVCCM ndiyo chombo cha juu katika uongozi wa CCM? Kama sio chombo cha juu hayo matusi wanayotoa mabosi wao wameridhia? Kama hawajaridhia mbona hatuoni hata moja akiomba walau msamaha kwa niaba ya hao vijana waoliopotoka? Kama hawajapotoka, na wanachofanya ni sahihi nani kawatuma? Wanapata nguvu wapi ya kuwatukana wazee wa nyumbani mwao hadharani? Je, kama wamefanya hayo kwa wazee wa nyumbani mwao- tena waasisi wa chama chao, itakuwaje kwa vyama vingine?

  WanaJF, ndiyo maana sasa naanza kuamini walichosema katika kikao chao cha Dodoma kuwa wanajipanga kuwa kila hali kupambana na Chadema.

  Tutashangaa nini kwa chochote kutoka kwa hao vijana ambao wameonesha utovu wa adabu hadharani dhidi ya wazee wao, wakiwafanyia chochote Chadema?

  Nadhani inatosha kuwalaumu hao vijana. Inafaa kumtambua aliye nyuma yao. Kwa bahati mbaya yeyote ambaye yuko nyuma yao hatambui anaongeza mgawanyiko ndani ya chama chao na kuharakisha kifo chake. Leo ni zamu ya Sumaye na Sita kutukanwa, kesho itakuwa zamu yake. Anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga. Tusubiri...

  Tutafakari haya kwa mtazamo wa siasa, na sio vinginevyo.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  upumbavu wao wafanyie hukohuko CCM.

  Kabla ya kukishughulikia chadema na wafuasi wake, ambao ni sisi, wanapashwa kujua jambo moja muhimu:

  Chadema siyo chama cha wazee. Kwa hiyo wasiseme kireja-reja ati watatushughulikia. Tutashughulikiana. Wala wasitarajie mteremko katika hilo. we are ready, they can pull the trigger if they mean business. waachane na kuchonga kwenye microphone za media. shenz kabisa.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mimi sisomi tena threads zinazohusu UVCCM na CCM...... naomba mlete za katiba mpya,Dowans na umeme.....
   
 4. D

  Dopas JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unajua inavyoonekana wana mpango wa kuanza kuleta tena fujo kama za mwaka jana na kusema ni sisi Chadema. Nadhani kwa sasa hawatafanikiwa kwani tumeona nia na azma yao mapema. Ila namsikitikia huyo aliye nyuma yao. Atajuta
   
 5. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Babu wao Makamba ndio mwanza anawashangilia kwa kupiga miluzi na kuwahamasisha watoto wawatukane wazee wao,hakika busara za wazee wengine hupungua kwa jinsi muda wa kukaa duniani unavyozidi kuwa mdogo,ukiwa na kiongozi sampuli ya Makamba unategemea nini?yeye anajifanya eti anamsemea mwenyekiti wake
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Msishau kuwa nyuma ya hao vijana wapo Makamba na Nundu.
   
 7. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  ni MZIMU WA BABA WA TAIFA UNAANZA KUWAANDAMA CCM KWA KUKIUKA WOSIA WAKE.naomba kuwakilisha.....
   
 8. haibreus

  haibreus JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 296
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  na Zantel to Airtel na Sheraton to Movenpick!
   
Loading...