Mbuzi wapanda miti wa Morocco

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
mbuzi%202%20may%2030.jpg

Mti huu wenye miiba, huzaa matunda ya msimu yenye kokwa linalozungukwa na ganda huwavutia sana mbuzi kuyala kutokana na ladha yake na umuhimu wake kiafya licha ya kuwa matunda hayo yanaota kwenye miti yenye miiba na nchani.

Mvuto huo wa asili ni kwamba huwavutia mbuzi kwa kiasi kikubwa na kujikuta wakilazimika kujitosa kuyafuata bila ya kujali kuwa wanahatarisha maisha yao kutokana na hali halisi ya ukubwa na uzito wao ikilinganishwa na matawi wanayopanda na kwato zao.

Wanyama hao, hujipenyeza na kusimama katika matawi ambayo ni hatari sana kwa maisha yao. Lakini kikubwa kinachowaongoza kufanya hivyo ni shauku ya kuyala matunda hayo yanayozalishwa kila mwaka msimu wake unapofika.

Wakati mwingine hutokea ,sio mbuzi mmoja tu anayevutiwa kupanda katika mti au tawi la mti huo. Wakati mwingine huwa ni kundi la mbuzi
Kama inavyoonekana katika baadhi ya picha mbuzi hao hupanda na kusimama kwenye matawi ambayo ni hatari sana kwa usalama wao kama tu kufanya hivyo kutawahakikishia kuyapata matunda hayo ya msimu.

Inavutia zaidi unaposhuhudia mbuzi sio mmoja tu anayepanda mti ni kundi la mbuzi linalovutiwa na matunda hayo hivyo hufanya juhudi wasiyakose.

Wakulima wenyeji huchukua juhudi ya kulima miti hiyo na pindi yanapoanza kukomaa, hujitahidi kuwapeleka mbali na miti hiyo wanyama hao ili kuyapa fursa ya kukomaa na kuwaruhusu wayasogelee .

Faida nyingine wanayoipata kutokana na malisho ya mbuzi hao ni kwenye kinyesi chao. Baada ya mbuzi kumaliza kula matunda na karanga kwenye mti, huachia mbegu katika kinyesi chao ambao ni rahisi kuziokota mbegu hizo na kuzikamua mafuta yaitwayo Argan oil. Mafuta ya argan, hutumika kwenye kifungua kinywa au kutengenezea mafuta ya urembo (cosmetics)

Kwa bahati mbaya, kwa vile mti mbuzi mti unaweza kabisa kuwa na faida kwa wamiliki wao, mbuzi zaidi na zaidi wameingizwa katika eneo hilo na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa miti hiyo ya Argania nchini Morocco.

Chanzo: BBC
 
Ni wachache sana wataoelewa na wataelewa baada ya kuona comment za watu.
Yahitaji kuwa na moyo mgumu sana.kwani huo mti umejichimbia mizizi sana na mizizi yake mingine haionekani na haijulikani ila lengo litabakia pale pale kuchukua/kupata unachokihitaji.

Asante kwa kutumia fasihi
 
Sasa unatuletea habari bila video jaman doh!!!!!!!
 
mbuzi%202%20may%2030.jpg

Mti huu wenye miiba, huzaa matunda ya msimu yenye kokwa linalozungukwa na ganda huwavutia sana mbuzi kuyala kutokana na ladha yake na umuhimu wake kiafya licha ya kuwa matunda hayo yanaota kwenye miti yenye miiba na nchani.

Mvuto huo wa asili ni kwamba huwavutia mbuzi kwa kiasi kikubwa na kujikuta wakilazimika kujitosa kuyafuata bila ya kujali kuwa wanahatarisha maisha yao kutokana na hali halisi ya ukubwa na uzito wao ikilinganishwa na matawi wanayopanda na kwato zao.

Wanyama hao, hujipenyeza na kusimama katika matawi ambayo ni hatari sana kwa maisha yao. Lakini kikubwa kinachowaongoza kufanya hivyo ni shauku ya kuyala matunda hayo yanayozalishwa kila mwaka msimu wake unapofika.

Wakati mwingine hutokea ,sio mbuzi mmoja tu anayevutiwa kupanda katika mti au tawi la mti huo. Wakati mwingine huwa ni kundi la mbuzi
Kama inavyoonekana katika baadhi ya picha mbuzi hao hupanda na kusimama kwenye matawi ambayo ni hatari sana kwa usalama wao kama tu kufanya hivyo kutawahakikishia kuyapata matunda hayo ya msimu.

Inavutia zaidi unaposhuhudia mbuzi sio mmoja tu anayepanda mti ni kundi la mbuzi linalovutiwa na matunda hayo hivyo hufanya juhudi wasiyakose.

Wakulima wenyeji huchukua juhudi ya kulima miti hiyo na pindi yanapoanza kukomaa, hujitahidi kuwapeleka mbali na miti hiyo wanyama hao ili kuyapa fursa ya kukomaa na kuwaruhusu wayasogelee .

Faida nyingine wanayoipata kutokana na malisho ya mbuzi hao ni kwenye kinyesi chao. Baada ya mbuzi kumaliza kula matunda na karanga kwenye mti, huachia mbegu katika kinyesi chao ambao ni rahisi kuziokota mbegu hizo na kuzikamua mafuta yaitwayo Argan oil. Mafuta ya argan, hutumika kwenye kifungua kinywa au kutengenezea mafuta ya urembo (cosmetics)

Kwa bahati mbaya, kwa vile mti mbuzi mti unaweza kabisa kuwa na faida kwa wamiliki wao, mbuzi zaidi na zaidi wameingizwa katika eneo hilo na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa miti hiyo ya Argania nchini Morocco.

Chanzo: BBC
Nilijua Morocco Kinondoni nilikuwa natafuta hayo maeneo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom