Mbuzi kafia kwa muuza supu

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Hapa ni mbuzi kafia kwa muuza supu...

Hivi uliwahi kukutana na challenge ya kuwakosea au kuwakera wanajeshi...au ukaingia kambi yao kimakosa...?

Nikupe tu Hint...
Endapo ukaingia kimakosa kambi ya jeshi alafu wakakuona wakakuita alafu ukajifanya unakimbia...watakuua simama tu nenda wasikilize umalizane nao...wale kesi zao hazifikagi mbali...

Mimi nilikuwa natoka harakati zangu za maisha maeneo ya tegeta...nikashuka mwenge nitafute magari ya kuelekea maeneo ya kimara(maeneo ya home)...nikawa nimeshuka kwenye foleni mbele ya lile daraja jipya...

Nikasema hebu nivukie hapa hapa niende upande wa pili...sikuwa najua kama hawaruhusu kukanyaga ile bustan yao pale...mimi nikapita tu bila wasiwasi...

Nilivyofika upande wa pili kuna jamaa alikuwa kavaa kiraia kwenye vile viti vya bar vinavyotengenezwa pale mwenge...akanambia wewe unaenda wapi...nikamwambia nawahi hapo masjid mara moja kuswali...nimechelewa sana...(nikashtuka haraka hapa bado nipo lugalo barrack, nikasema nisijifanye mjuaji kuwa tu mpole)...jamaa alivyosikia msikitini...akafikiriaaaaa...akanambia kwanini umekatiza pale...? Nikamwambia nilikuwa sijui...ila mimi nimeshuka kwenye foleni niwahi swala...AKANAMBIA HAYA NENDA KASWALI...ILA USIRUDIE TENA KUPITA HAPA...

Nikasema alhamdulillah...la sivyo ningeongezewa shift ya jioni pale jeshini...

Hebu eleza yako...
zembwela-20190611-0001.jpeg
 
Hebu eleza yako...View attachment 1124887
Hivi ni Kweli tumejijengea Woga huo kwa wanajeshi wetu??
 
Kuna wanajeshi wakorofi Sana ila baadhi...... Na wapo ambao hawapendi uonevu.... Miii asilimia kubwa nliokutana nao hawapendi uonevu hawapendi wanafunzi waonewe na makondakta( hi nmeishuhudia nikiwa na soma na hata baada ya kumalizia pia nmeishuhudia)....

Ukiwa karibu nao Kuna lugha sio za kuongea lugha chafu chafu zile alaf pia uache kiherehere.....

Wanacheza wenye tabu tabu nadhani Ni Hawa ambao cjui ndo makurutaaa au jkt wale ambao hata ajira hawana
 
N binaadamu kama wewe wale wako na hisia pia kama wewe, uwoga wako ndio utakufanya uboronge kutoa maamuzi kwa mtu yeyote lazima akulipue ukizingua.
 
Kuna wanajeshi wakorofi Sana ila baadhi...... Na wapo ambao hawapendi uonevu.... Miii asilimia kubwa nliokutana nao hawapendi uonevu hawapendi wanafunzi waonewe na makondakta( hi nmeishuhudia nikiwa na soma na hata baada ya kumalizia pia nmeishuhudia)....

Ukiwa karibu nao Kuna lugha sio za kuongea lugha chafu chafu zile alaf pia uache kiherehere.....

Wanacheza wenye tabu tabu nadhani Ni Hawa ambao cjui ndo makurutaaa au jkt wale ambao hata ajira hawana
Yes Makuruta ndio sifa ila wenye vitengo vyao wako peace
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom