Mbunge wangu Leonidas Gama Songea mjini

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
1,002
955
Jimbo lako limekuwa likiongoza kwa ukatwaji umeme ghafla na ukirudi unarudi hovyo na kuunguza vitu vyetu.Kwa siku umeme unakatika hata mara 20 bila taarifa.

Fahamu sisi wana Songea ni masikini wenye saloon na mashine za wedding. Ukatwaji huu umeme unaleta hasira kwa TANESCO na hasira kwako mbunge wetu ambaye upo kimya na hujaonesha jitihada zozote kwa hilo.

Katika ziara ya Waziri Mkuu kama kawaida yenu mliufanya umeme kuwa wa uhakika na alipo ondoka mkaanza kukata hovyo hovyo. Songea mjini ipo hovyo ikilinganishwa na Mbinga kwa hali ilivyo ni bora TANESCO isiwepo tujue moja.
 
Fahamu sisi wana Songea ni masikini wenye saloon na mashine za wedding. (Mwisho wa kunukuu)
 
Kaeni kimya,kwani hamjui flana,vilemba,kanga na kofia mlizopewa,ndo mnaisoma namba hivyo!
 
Kaeni kimya,kwani hamjui flana,vilemba,kanga na kofia mlizopewa,ndo mnaisoma namba hivyo!
Na kiitikio chao cha
...na wavimbe wa pasuke,
watajijua wenyewe,
acha waisome namba eeeeh
 
Back
Top Bottom