Mbunge wa upinzani kutoa zawadi kwa wagonjwa ni kosa?

Hata hivyo akili na mioyo ya watanzania inashuhudia ukatili huu, serikali hii inazidi kujichimbia laana badala ya baraka.
Mimi wala sikushangaa nilipoiona hiyo habari, kila mtu sahivi anaogopa akionekana akishirikiana kwa namna yoyote ile na upinzani ataambiwa msaliti, na kama ni mtumishi wa umma hata kibarua chake kinaweza ota nyasi...!

Hilo tukio linachukuliwa kama ni la kufanya siasa hospitalini kwa sababu tu ni mtu wa upinzani ndo anahusika.., ila kama angekuwa mbunge au kiongozi yeyote wa ccm kafanya kitu hicho hicho nina uhakika wala kusingetokea kizingiti chochote na angefanya shughuli yake bila tabu.....!

Ndipo tulipofika hapo!!
 
Upo sana tu kasoro kigenge kidooogo cha wapigaji fedha za ruzuku za cdm psle UFIPA ndo hiwa wanasumbua humu ndani. Huwezi kuvuruga utaratibu wa kuwaona wagonjwa kisa unapeleka zawadi.vitu vyenyewe inasemekana ni biskuti na sabuni za magwanji..
Asante mkuu. Ningependa kujuw dini lako. Ili tuende sawa.
 
Magufuli ni mtu mbaya sana,anatutenga sana ndani ya nchi yetu,haya mambo ya kubaguana yameshika kasi ndani awamu yake,yeye anajenga nchi ya CCM tu anachukia sana upinzani hasa CDM
Unaweza niambia ww kama ww kakutenga na nani ktk jamii yako?Leo nimetoka kula sikukuu na jamaa ambaye ni mfuasi wa chama flank damu na tumeinjoy sana.Ebu nipe huo ushahid ukianza na ww jinsi gani umetenganishwa na saiz unachuki na watu flani ktk jamii yako kisa siasa.
 
Juma punda maharage anatengeneza siasa za kibaguz sana ila mm huwa najiuliza wale wenzetu kule vjjn wanaomshangilia kwenye mikutano yake Hv Wao hawajaathirika na Huyu mtu
 
Ngosha kiukweli ametugawa sana,, imefikia wakati sasavi mtanzania hadi anafurahia kifo cha mwingine,,jamaa ana roho Mbaya
Habar za kufurahia vifo hazijaanza leo kwa jpm.Ukiwa na kumbukumbu utaelewa.Kwa machache sana,2015 vilitokea vifo vya wanasiasa kama Selina Kombani na Mtikila.Upinzani ulishangilia sana na wengi walikua wakiimba ooh walimtukana lowasa.Akapata ajari nape,upinzani ulifurah sana hadi kufikia hatua kuombea afe.Hii ya watu kufurahi matukio mabaya yakiwakuta wanaccm haijaanza kwa jpm na hii tabia imeendelea hivohivo akifa wa ccm utasikia albadili na kejeli kibao.Niseme tu uchaguz wa mwaka 2015 uliwafanya watu wawe wehu bila sababu za mcng.Licha ya hivo Haya yote yameendelea kuwa kelele za kwenye mitandao tena ya wanasiasa kwa wanasiasa. Sijasikia huku mtaani mtu akifariki watu wanahoji ni chama gani,zaid Haya sana yako jf na mda mwingine huwa naona huu mtandao kuna watu wamegeuza jukwaa la propaganda chafu.Huwez kuhubir watu wametangana mitaani bila kuja na series ya matukio.
 
Hii dhambi ikiachwa iendelee kutendeka itatutafuna kama taifa. Viongozi wa dini walazimisheni watawala watubu kama alivyo anza kakobe

sisi wengine ambao hatuja jengewa misikiti na hatuli meza moja na viongozi tukiyasema haya moja kwa moja tutaitwa magaidi-kwa hili bora nyie wenzetu afazali mkiyanena hua kubwa zaidi uambiwa si raiya wa inch hii ila huku kwetu ni ugaidi au segerea tunaogopa bora nchii izame ila tupo kimya-dhambi ya ubaguzi haija acha inch salama yaoneni sasa
 
Upo sana tu kasoro kigenge kidooogo cha wapigaji fedha za ruzuku za cdm psle UFIPA ndo hiwa wanasumbua humu ndani. Huwezi kuvuruga utaratibu wa kuwaona wagonjwa kisa unapeleka zawadi.vitu vyenyewe inasemekana ni biskuti na sabuni za magwanji..
Vitu hivyo ni Lulu kwa wagonjwa, hasa walio na kipato cha chini
 
Tutakuwa hatuombani maji sasa.
Heri ya Christmas,

Naangalia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, ITV.
Mbunge wa viti maalum(CHADEMA) Roda Kanchela, amekataliwa kuingia kwenye hospitali ya Wilaya ya Katavi. Alikwenda hapo kwa minajili ya kusalimia wagonjwa kwenye wodi ya kinamama.

Imelazimu kinamama hao kutolewa nje ili wakapokee zawadi. Wauguzi wamekataa kutoa sababu.
Mshikamano na undugu baina yetu uko shakani kwa sababu ya siasa chafu. Sina hakika kama ni amri toka juu.
 
Unaweza niambia ww kama ww kakutenga na nani ktk jamii yako?Leo nimetoka kula sikukuu na jamaa ambaye ni mfuasi wa chama flank damu na tumeinjoy sana.Ebu nipe huo ushahid ukianza na ww jinsi gani umetenganishwa na saiz unachuki na watu flani ktk jamii yako kisa siasa.
Kwani humu tunajadili nini kwa sasa???
 
Huyo mbunge namfahamu na mtu wa dini ukiondoa siasa, sema nani ange ruhusu mama aonekane mwema ndani jimbo hili wakati anatoka CDM
 
Watanzania kwa awamu hii ili limekuwa funzo kubwa si kila mtu anafaa kushika nyadhifa kubwa kama hizo, mzee Kingunge alisema watu waka mpuuza matokeo yake ndio haya ubaguzi kila kona. Ila ili uonekane mzuri kaa chini ya miguu ya mfalme uendelee kupiga makofi na kushangilia bila ya hivyo utainekana kuwa ni adui wa mfalme.
 
Back
Top Bottom