WANALIZOMBE
Member
- May 18, 2011
- 50
- 14
Wana Jimbo wenzangu wa Jimbo la Ukonga, mbunge wetu Yupo likizo? Wana nchi tunakero nyingi sana, hatukuoni jimboni wala mjengoni?
Wana Jimbo wenzangu wa Jimbo la Ukonga, mbunge wetu Yupo likizo? Wana nchi tunakero nyingi sana, hatukuoni jimboni wala mjengoni?
Wana Jimbo wenzangu wa Jimbo la Ukonga, mbunge wetu Yupo likizo? Wana nchi tunakero nyingi sana, hatukuoni jimboni wala mjengoni?
Duh, kichekesho mimi mwenzako nilikuwa simjui hata jinsia yake. Maana wakati wa uchaguzi sikuwa bongo. Nilisikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba CCM wameshinda Ukonga. Yaani mimi huwa naamua tu kumtafuta Jerry Silaa, angalau huwa anaweza akasikiliza japo inaweza kuwa ngumu sana kwa baadhi ya mambo kuyashughulikia yeye, maana yanakuwa nje ya eneo lake la utawala. Lakini huwa natumia advantage ya umeya wake kumfanya ashughulikie na kwingine. Mwita Maranya, wewe unaishi Kitunda? Mimi nipo Gongo la mboto. Itabidi tutafutane mkuu, tupange mikakati ya 2015. Ikiwezekana tukupe jimbo mkuu. Au unataka kurudi kugombea ubunge Mara?Mkuu Lukolo itabidi tutafutane kumbe tuko mtaa mmoja!?
Huyo mama yuko busy na biashara zake za Tumaini zilizoko Kitunda na Kerezange(shule za nursery, msingi na sekondari).
Nadhani ameamua kutumia vyema fursa ya kuwa mbunge kuziboresha shule zake ili itakapofika 2015 anapoachia ngazi basi shule zake ziwe katika viwango vya juu.
Kuna siku moja daraja la Mongolandege lilikuwa limesombwa na maji, nikajaribu kumpigia simu lakini hakutaka kupokea, na wananchi wengi kila walipojaribu kumpigia simu alikuwa hapokei. Pamoja na kuwa tukio lile lilitangazwa katika vyombo vya habari na wananchi walifanya juhudi za kumpata Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala na Mhandisi wa Manispaa ya Ilala na wakafika eneo la tukio kujionea hali halisi na kuchukua hatua za kulitatua, lakini mbunge hakuwahi kuonekana wala kukanyaga eneo la tukio japo kusaidiana na wananchi kuhakikisha kwamba linajengwa daraja la kudumu na imara.
Baada ya kuona hapokei simu nikaamua kumuandikia sms, lakini ajabu na kweli ni kwamba alikuja kujibu sms yangu baada ya siku tatu!!! na hakutaka kujua hali ilikuwaje. Huyu mama ni bure kabisa kwani tangu atangazwe kuwa mbunge wa Ukonga hajawahi kuitisha japo mkutano wa hadahara mmoja tu ili kuzungumza na wananchi. Ndio maana hata bungeni hazungumzi kwakuwa hana cha kuzungumza kwakuwa hakutani na wadau wa jimbo lake...
Hivi katiba inaruhusu wananchi kumkataa ubunge? Je mbunge anaweza kupoteza nafasi yake ya ubunge pale inapotokea kwamba wannachi wamemkataa? Hebu wanasheria tusaidieni hapa.Hapana mbunge wenu hayuko likizo kwani yeye kama mtumishi hawezi kwenda likizo bila kibali cha mwajiri wake ambaye ni nyie wapiga kura. Kwa hiyo kimsingi nyie wapiga kura ndiyo mko likizo siku mkimaliza likizo yenu na kurudi kazini mtumishi wenu atachapaka kazi kwa bidii kwani hawezi kukubali kupoteza kibarua chake kwa sababu ya uzembe.
Tumpe Mwita Maranya, kama hatakuwa tayari; basi mimi nitagombea kwa tiketi ya CHADEMA.Jimbo letu la ukonga nan yupo tayari na anafaa kwa mwaka 2015 ???
Duh, kichekesho mimi mwenzako nilikuwa simjui hata jinsia yake. Maana wakati wa uchaguzi sikuwa bongo. Nilisikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba CCM wameshinda Ukonga. Yaani mimi huwa naamua tu kumtafuta Jerry Silaa, angalau huwa anaweza akasikiliza japo inaweza kuwa ngumu sana kwa baadhi ya mambo kuyashughulikia yeye, maana yanakuwa nje ya eneo lake la utawala. Lakini huwa natumia advantage ya umeya wake kumfanya ashughulikie na kwingine. Mwita Maranya, wewe unaishi Kitunda? Mimi nipo Gongo la mboto. Itabidi tutafutane mkuu, tupange mikakati ya 2015. Ikiwezekana tukupe jimbo mkuu. Au unataka kurudi kugombea ubunge Mara?
Hivi katiba inaruhusu wananchi kumkataa ubunge? Je mbunge anaweza kupoteza nafasi yake ya ubunge pale inapotokea kwamba wannachi wamemkataa? Hebu wanasheria tusaidieni hapa.
Tumpe Mwita Maranya, kama hatakuwa tayari; basi mimi nitagombea kwa tiketi ya CHADEMA.
Haha, umenichekesha sana uliponambia kwamba wahudumu wanafanya kazi ya kupiga ramli kutokana na ukosefu wa vifaa. Poleni sana wakuu. Ndiyo Tanzania yetu hii. Mkuu, huyu Jerry Silaa si kwamba alinisaidia kutatua tatizo, bali alinijibu on time japo kwa ahadi, na kutoa ufafanuzi wa tatizo lilikuwa linatukabili. Lakini hakusolve chochote. Anautafuta ubunge hivi sasa? Nafikiri yeye abaki kwenye nafasi ya umeya. Ubunge atuachie CHADEMA kwa sasa. Nipo mkoani kikazi kwa muda, nikirudi Ukonga nitakupm ili tupeane namba ya simu tutafutane. Mikakati ya ushindi inatakiwa ianze mapema.Kamanda Lukolo mimi nipo Mongolandege.
Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa kama kuna mambo umejaribu kumtumia yakafanikiwa basi una bahati nzuri.
Mimi niliwahi kumfuatilia sana kuhusu ufunguzi wa zahanati ya Mongolandege, ambayo ujenzi wake ulikamilika mwishoni mwa mwaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu lakini haukuwahi kutoa huduma kwa takribani mwaka mzima hadi pale wananchi walipopiga kelele sana.
Baada ya kubana nae, nakumbuka alinijibu siku moja kuwa kuendesha manispaa kubwa kama ilala ni sawa na kuendesha meli, kwakweli nilicheka tu kimya kimya. Nikajiuliza kama Jery alikuwa anatambua ukubwa na uzito wa kazi ya umeya aliyokuwa anaililia.
Anyway, hata hivyo zahanati imefunguliwa mwaka jana, ingawa haina vifaa tiba, wameleta wauguzi na manesi kama watatu au wanne ambao wanatibu kwa "kupiga ramli" kwakuwa hakuna kifaa chochote cha kufanyia kipimo, hata kipimo cha maleria hakuna. Na kichekesho zaidi ni kwamba zahanati hiyo inafunguliwa Jumatatu hadi Jumamosi, na siku za Jumapili inafungwa!!! Sasa jiulize kama jumapili watu hawaumwi ama hawahitaji matibabu???... eti meya aliyeshindwa kazi naye anafanya kampeni za kutaka kuwa mbunge.
Btw, tutafutane weekend moja tuone ni namna gani tunaweza kuunganisha nguvu na viongozi wa Chadema jimbo la Ukonga ili tuhakikishe kuwa 2015 hatupotezi jimbo kwa kuliacha kwa wauza sura wa magamba, ambao wamethibitika pasipo shaka kuwa hawawezi kutukwamua kamwe.
I agree! Na hilo ni iwapo kutajitokeza wagombea wengi. Lakini kama atajitokeza mmoja kama ambavyo mara nyingi huwa inakuwa, basi haitakuwa shida kusema fulani endelea.Mkuu Lukolo demokrasia ndani ya chama chetu ndiyo itakayoamua nani atapeperusha bendera yetu mwaka 2015.