huyu bwana anamatatizo masaa ma4 yote yapotee kwanini asiseme watakaokutwa maeneo machafu wachukuliwe hatua ?
masaa 4 ni mengi sana sana halafu isitoshe jumamosi waliowengi wanakuwa majumbani lets say una site yako unajenga manunuzi uanze kufanya saa 4 ndo ufanye safari ya kwenda site huu ni upiotezaji wa muda wa watanzania .................
nonesense
Hahahaha, mambo mengine ni ya kuchekesha sana, hebu tupate opinion ya LizaboniNaungaMkono hoja ya Mbunge, Mie kwny Pharmacy yangu nami natakiwa kufungua saa 4 asbh jmosi, sasa Wagonjwa wanohitaj dawa kwa Haraka wafe kwa kuwa kuna watu muda huo wanatakiwa kuwa wanazibua Mifereji, Ni upuuzi kusimamisha Jiji ili watu wachome Makaratasi na kufagia mitaro
Wanafikiri tunafanya usafi na camera kama wao, wanarundikana kwenye skwea mita 8 watu 40 na mafagio hadi wanakanyagana. Usafi mi kwangu nafanya na wife dakika 45 tunachoma majani tunahamia ndani.huyu bwana anamatatizo masaa ma4 yote yapotee kwanini asiseme watakaokutwa maeneo machafu wachukuliwe hatua ?
masaa 4 ni mengi sana sana halafu isitoshe jumamosi waliowengi wanakuwa majumbani lets say una site yako unajenga manunuzi uanze kufanya saa 4 ndo ufanye safari ya kwenda site huu ni upiotezaji wa muda wa watanzania .................
nonesense
Siku zote alikua wapi... mana Makonda hajachaguliwa jana... aache unafik, aoneshe sasa atachukua hatua gani kupinga watu kufanya usafi jumamosi na maduka yafunguliwe mapema..MBUNGE APINGA AMRI YA RC MAKONDA
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili wafanye usafi.
Amesema amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.
Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni batili na haipaswi kuendelea kuwapo.
Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.
Mbunge huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususan wa mjini unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo yao.
Katika mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.
“Mimi naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na ni batili.
“Ninachotaka kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.
“Hivi mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani, huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge huyo na kuongeza:
“Watendaji lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu” alisema Waitara.
Katika hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa wananchi.
Badala yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa waaminifu katika jamii.
Mkuu Liza hatoi maoni kwenye uzi kama huu.... yeye ana uzi zake fulani fulani...hasa zikihusu chadema na EL...Hahahaha, mambo mengine ni ya kuchekesha sana, hebu tupate opinion ya Lizaboni
Mwenzenu ana shahada ya umbea na udaku hivyo kwake ni taaluma.Mada ngumu hii hawezi kuchangia. Kazoea udaku na umbea wa lumumba
MBUNGE APINGA AMRI YA RC MAKONDA