Mbunge wa Ukonga ampinga Makonda kuhusu wafanyabiashara kufanya usafi kila siku ya Jumamosi

Yeye hajali shughuli za watu maana analipiwa kila kitu na serekali hivyo maisha ya wengine kwake sio kitu ili mradi mteuzi wake anamsifia. Utakuta yeye huko ofisini hata kikombe cha chai haondoi mezani eti kuna mtu wa usafi!!
 
Unajua vitu vingine tunavyohamasisha tuwe tunaangalia kwa sababu gani, suala la usafi linafaa lizingatiwe kila siku tukisema mtu fulani kaweka sheria fulani ya kufanya usafi mpaka siku fulani hiyo pia itakuwa inampa mtu mwanya wa kuchafua mazingira siku zingine ili usafi ufanyike kila siku iliyopangwa, labda hii ingekuwa inapangwa kwa maeneo tu yaliyokwisha chafuliwa awali ili suala hili lisijitokeze tena kwa siku zijazo.
 
alichosema mbunge ni sahihi kuliko mkuu wa mkoa. huyu ni mwakilishi wa wananchi na kachaguliwa kihalali...
 
mtu yoyote akikata leseni ya biashara hulipia na pesa ya usafi,
hizi pesa mnapeleka wapi??
Mkuu, pesa wanapeleka wapi??? (Wana matumbo hayashibi)
BTT:-
Kikawaida ukiona mtu mjinga anatoa amri za kijinga na watu wajinga wanakaa kimya huku wakishabikia ujinga ule na kuukubali tambua aliyetoa amri hiyo na wanaoitii wanafanana akili. (sio uchochezi maana hawachelewi...)
Hebu tufikirie na kujiuliza:-
  1. Huyo anaetoa amri je huwa ananunua sukari ya kibaba au maandazi kila siku kwa ajili ya familia?
  2. Je mtaani kwake ananunua dawa katika kijiduka kidogo cha dawa kila anapojisikia vibaya?
  3. Je unga wa uji wa mwanae ananunua robo robo kila uchao kulingana na kipato chake?
  4. Je vile vizahanati vya mtaani ambavyo husaidia wagonjwa kupata huduma ya kwanza na kupunguza foleni katika mahospitali yetu vina faida gani ya kuendelea kuwepo? (maana kuugua hakuchagui muda) Na tufe tu!!!
  5. Je ni lini wanafanya rejea ya matokeo ili kutambua amri hazitekelezeki na si rafiki na raia au mazingira husika?
  6. Je yale majitaka tiririfu Kariakoo, City Centre na kwingineko ni lini yataundiwa amri ili kipindupindu kitokomee Dar es Salaam?
  7. Je ni lini yale magari takataka ya kubeba taka yatadhibitiwa ili uchafu, taka na harufu mbaya visiendelee kuwa kero kwa walipa ushuru na kodi? (Maiko Jakisoni aliposema Dar kunanuka WTz walimlaani hili leo ndio wanajua Dar inanuka baada ya mtu kuwa sambamba na lori lile kwenye mataa!!")
Sitaki kuzungumzia pesa za tozo za usafi zinazofanywa na Halmashauri wala hizo adhabu za 50,000/= wanazotozwa wakaidi amri. Bali najiuliza ule msingi tuliojengewa shule kuwa usafi ni kuanzia saa moja kamili (baada ya kuwahi namba saa moja kasorobo) hadi saa moja na nusu ulikuwa na maana gani? Ni usafi upi unaofanyika masaa mawili kwenye kiduka cha vocha mtaani? (au wanapiga deki hewani pia!!?) Je ni wabunge wangapi zaidi ya Mh. Waitara walioona athari na kuikataa ili kuwaokoa wananchi na adha mbaya za amriccm ambazo si rafiki na kada ya chini?

Nawatakia wikiendi njema.
 
Back
Top Bottom