Mbunge wa Ukonga ampinga Makonda kuhusu wafanyabiashara kufanya usafi kila siku ya Jumamosi

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,663
2,000
MBUNGE APINGA AMRI YA RC MAKONDA
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili wafanye usafi.

Amesema amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni batili na haipaswi kuendelea kuwapo.

Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.

Mbunge huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususan wa mjini unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo yao.

Katika mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.

“Mimi naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na ni batili.

“Ninachotaka kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.

“Hivi mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani, huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge huyo na kuongeza:

“Watendaji lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu” alisema Waitara.

Katika hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa wananchi.

Badala yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa waaminifu katika jamii.
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,296
2,000
huyu bwana anamatatizo masaa ma4 yote yapotee kwanini asiseme watakaokutwa maeneo machafu wachukuliwe hatua ?

masaa 4 ni mengi sana sana halafu isitoshe jumamosi waliowengi wanakuwa majumbani lets say una site yako unajenga manunuzi uanze kufanya saa 4 ndo ufanye safari ya kwenda site huu ni upiotezaji wa muda wa watanzania .................

nonesense
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,481
2,000
NaungaMkono hoja ya Mbunge, Mie kwny Pharmacy yangu nami natakiwa kufungua saa 4 asbh jmosi, sasa Wagonjwa wanohitaj dawa kwa Haraka wafe kwa kuwa kuna watu muda huo wanatakiwa kuwa wanazibua Mifereji, Ni upuuzi kusimamisha Jiji ili watu wachome Makaratasi na kufagia mitaro
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,686
2,000
huyu bwana anamatatizo masaa ma4 yote yapotee kwanini asiseme watakaokutwa maeneo machafu wachukuliwe hatua ?

masaa 4 ni mengi sana sana halafu isitoshe jumamosi waliowengi wanakuwa majumbani lets say una site yako unajenga manunuzi uanze kufanya saa 4 ndo ufanye safari ya kwenda site huu ni upiotezaji wa muda wa watanzania .................

nonesense

Kwanza hili suala ni la serikali za mitaa kuweka sheria ndogondogo za kuhakikisha maeneo yote ndani ya mipaka yake ni masafi na salama 24/7.

Hakuna sababu ya kuangalia usafi siku y ajumamosi asubuhi tu wakati siku zingine zote maeneo yamejaa uvundo.

Kwanz akwa nini wamezuia mashine za takataka zilizokuwa zimeagizwa na CHADeMA Kinondoni kam akweli wana maanisha usafi?

Ninadhani akienda kwenye mihadhara ya kero, huyu mkuu wa mkoa aulizwe hili suala. Kwa nini wanazuia nyenzo za usafi salama na endelevu kwa hila huku wakisisitiza usafi hatarishi?
 
Ndalama

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
8,791
2,000
NaungaMkono hoja ya Mbunge, Mie kwny Pharmacy yangu nami natakiwa kufungua saa 4 asbh jmosi, sasa Wagonjwa wanohitaj dawa kwa Haraka wafe kwa kuwa kuna watu muda huo wanatakiwa kuwa wanazibua Mifereji, Ni upuuzi kusimamisha Jiji ili watu wachome Makaratasi na kufagia mitaro
Hahahaha, mambo mengine ni ya kuchekesha sana, hebu tupate opinion ya Lizaboni
 
Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,125
2,000
huyu bwana anamatatizo masaa ma4 yote yapotee kwanini asiseme watakaokutwa maeneo machafu wachukuliwe hatua ?

masaa 4 ni mengi sana sana halafu isitoshe jumamosi waliowengi wanakuwa majumbani lets say una site yako unajenga manunuzi uanze kufanya saa 4 ndo ufanye safari ya kwenda site huu ni upiotezaji wa muda wa watanzania .................

nonesense
Wanafikiri tunafanya usafi na camera kama wao, wanarundikana kwenye skwea mita 8 watu 40 na mafagio hadi wanakanyagana. Usafi mi kwangu nafanya na wife dakika 45 tunachoma majani tunahamia ndani.
 
yekini

Senior Member
Jan 11, 2015
146
225
MBUNGE APINGA AMRI YA RC MAKONDA
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili wafanye usafi.

Amesema amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni batili na haipaswi kuendelea kuwapo.

Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.

Mbunge huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususan wa mjini unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo yao.

Katika mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.

“Mimi naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na ni batili.

“Ninachotaka kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.

“Hivi mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani, huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge huyo na kuongeza:

“Watendaji lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu” alisema Waitara.

Katika hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa wananchi.

Badala yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa waaminifu katika jamii.
Siku zote alikua wapi... mana Makonda hajachaguliwa jana... aache unafik, aoneshe sasa atachukua hatua gani kupinga watu kufanya usafi jumamosi na maduka yafunguliwe mapema..
 
Miss Madeko

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
4,212
2,000
Yalinikuta
Nimekurupuka kwenda kkoo saa 2 niko maduka yote yameweka Padlock nilikoma mwenyew

Niltamani nimwone mwenye amri nimng'ate kwa meno yangu mawili
 
kulwa MG

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
1,289
2,000
kwan pesa wanayoitoa kwa ajili ya usafi ktk manispaa za jiji zianenda wap?..ama kweli,makonda wote sio wa dar,arusha hata mara akili zao ni sawa!!!
 
DomieLe

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
809
1,000
MBUNGE APINGA AMRI YA RC MAKONDA
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili wafanye usafi.

Amesema amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni batili na haipaswi kuendelea kuwapo.

Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.

Mbunge huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususan wa mjini unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo yao.

Katika mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.

“Mimi naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na ni batili.

“Ninachotaka kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.

“Hivi mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani, huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge huyo na kuongeza:

“Watendaji lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu” alisema Waitara.

Katika hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa wananchi.

Badala yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa waaminifu katika jamii.

ISSUE NI USAFI KWENYE MAENEOYAO YA BIASHARA.MASWALI SASA YANAKUJA:

1. JE KAMA MTU ANATENGA MUDA WAKE, SAY NUSU SAA KILA SIKU BAADA YA KAZI AU KABLA YA KAZI KUFANYA USAFI ENEO LAKE AACHANE NA UTARATIBU HUU AFANYE BIASHARA KWENYE UCHAFU HADI IFIKE JUMAMOSI?

2. NA KWA WALE WALIOAMUA USAFI WAO UFANYIKE HIYO JUMAMOSI KUNA UBAYA GANI KAMA WATAAMUA KUTOA AJIRA HIYO KWA WATU WENGINE WASIO NA KAZI NA WAO KUENDELEA NA BIASHARA ZAO. KUFUNGA BIASHARA KUNAATHIRI MAPATO BINAFSI NA HIVYO HIVYO MAPATO YA TRA
 
hardboy

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
794
1,000
Naomba kuuliza.Hiyo amri ya Makondakta ipo kisheria au anajishaua huyo kondakta?
 
Mama_Aheshimiwe

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,716
2,000
Amesahau na Jumapili tufunge tukamwabudu Mungu

Baba'ake alisema ameokoka hakuweza kumpiga Warioba
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom