Mbunge wa TEMEKE, Abdallah Mtolea (CUF) alala Korokoroni, Bima ya gari yamponza

Mwandishi wa habari hajafanya utafiti, maana kapewa taarifa za upande mmoja - polisi. Unajua taarifa za polisi huwa zinakanwa mahakamani?
TRUE.nimemsikia mtolea alichozungumza ni tofauti na alichoongea huyo mkuu wa polisi....
 
YEYE Mbunge aliondoka na kudharau police, umeelewa kilichoandikwa? Huenda angesikiliza police angepigwa faini tu ya kuendesha gari bila insurance, sasa kuwaacha traffic police ni kuwadharau na kudharau sheria za barabarani.

Lazima tuwe fair sana ktk kutii sheria, mbunge mzima anaendesha gari bila INSURANCE? Halafu anasimamishwa anahojiwa anawadharau police anaondoka zake?

Hii ni dharau sana na kuvunja sheria, Lazima tuwe makini while judging mtu akifanya kosa.

Dhana ya kuona wapinzani wanaonewa tu ni kosa..
Baada ya MV kuondolewa sasa wamehamia kwenye bima
 
Mwendesha gari mwenye mafunzo timamu kuendesha gari bila bima ni kosa kubwa sana.Ikitokea ajali umekwisha.
Tuache siasa.
Hilo kosa ni sawa na kosa lingine la barabarani isipokuwa kuua mtu. Ukitaka kujua ni sawa na kosa kama la kuendesha gari bovu, angalia adhabu yake.

Vv
 
“Atafikishwa mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.
Chanzo: Mwananchi
Sina tatizo na kusimamia sheria. Nina tatizo na jinsi zinavyosimamiwa kwa kuchagua wapi sheria ifanye kazi wapi ifumbiwe macho

Tuliambiwa ma DC, RC, Wabunge n.k. hawakaguliwi vyeti kwasababu si 'watumishi wa umma'
Kauli hiyo ilikuwa tofauti na ya Ngeleja aliyesema 'amekuwa mtumishi wa umma' kwa miaka kadhaa

Kama sheria haichagui mbona ilitengenezwa kitu kukwepesha DC na RCs kukaguliwa vyeti
Sheria ingefuata mkondo bila kujali nafasi kuna mkoa usingekuwa na RC

Ile kesi ya kuvania clouds imeishia wapi? Mbona sheria haikufuata mkondo

Tusitumie sheria kukidhi haja za matamanio yetu, tutumie kama zilivyo bila kubagua
 
YEYE Mbunge aliondoka na kudharau police, umeelewa kilichoandikwa? Huenda angesikiliza police angepigwa faini tu ya kuendesha gari bila insurance, sasa kuwaacha traffic police ni kuwadharau na kudharau sheria za barabarani.

Lazima tuwe fair sana ktk kutii sheria, mbunge mzima anaendesha gari bila INSURANCE? Halafu anasimamishwa anahojiwa anawadharau police anaondoka zake?

Hii ni dharau sana na kuvunja sheria, Lazima tuwe makini while judging mtu akifanya kosa.

Dhana ya kuona wapinzani wanaonewa tu ni kosa..
Kama alifanya hivyo basi Ni dharau na Ni makosa.

Lakini Je, ndivyo ilivyotokea?
 
Hilo kosa ni sawa na kosa lingine la barabarani isipokuwa kuua mtu. Ukitaka kujua ni sawa na kosa kama la kuendesha gari bovu, angalia adhabu yake.

Vv
UA MTU halafu gari haina bima.
Ua MTU gari INA bima. Adhabu ni sawa?
Mh ujuaji huponza.
 
  1. Huenda aliwajibu vibaya Polisi, mbona wengi hufanya kosa kama hilo, nakumbuka joka la makengeza liliposababisha kifo kwa akina dada wawili kwenye babaj miaka kadhaa iliyopita, lilitajwa kuwa lilikuwa linadrive chombo chenye expired insurance, wala halikulala rumamnde.
  2. Na huyu mwandishi wa Mwananchi, mbona amerudiarudia sana maneno, haoni kama ana matumizi mabaya ya wino na kuisababishia kampuni hasara!!
Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.
Dar es Salaam. Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda.
Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.
Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda wake
.
 
Mbunge wa Temeke alala rumande

Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.

Dar es Salaam.Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda.

Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda wake.

“Askari wa usalama barabarani walipomhoji aliamua kuwapuuza na kuondoka zake,” amesema.

Amesema polisi walimfuatilia na kumkamata na sasa anaendelea kuhojiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.

“Atafikishwa mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
Hakuna sababu ya kumtia ndani badala yake wangehuzunika na kumsitikia madhara atakayopata endapo atapata ajali Kwa kukosa BIMA ambayo ni tahadhari kwake sio polisi
 
YEYE Mbunge aliondoka na kudharau police, umeelewa kilichoandikwa? Huenda angesikiliza police angepigwa faini tu ya kuendesha gari bila insurance, sasa kuwaacha traffic police ni kuwadharau na kudharau sheria za barabarani.

Lazima tuwe fair sana ktk kutii sheria, mbunge mzima anaendesha gari bila INSURANCE? Halafu anasimamishwa anahojiwa anawadharau police anaondoka zake?

Hii ni dharau sana na kuvunja sheria, Lazima tuwe makini while judging mtu akifanya kosa.

Dhana ya kuona wapinzani wanaonewa tu ni kosa..
Kuendesha gari isiyokuwa na insurance siyo kosa km utakuwa na cash, kwani ata sheria haikulazimishi kukata insurance endapo unauwezo wa kulipia tatizo lolote utakalo kuwa umesababisha.
Yaani ni muhimu kuwa na bima,lkn si lazima.
Mfn: Kila raia ni muhimu kuweza kuwa na bima ya afya ili uweze kurahisisha kupata matibabu bure, lkn si lazima km una uhakika wa kuwa na pesa ya matibabu muda wote.
Ni muhimu kuwa na bima ya nyumba, lkn si lazima. Ila police wetu wanachukulia kila mtu mwenye gari lazima awe na bima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge wa Temeke alala rumande

Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.

Dar es Salaam.Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda.

Akithibitisha kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.

Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda wake.

“Askari wa usalama barabarani walipomhoji aliamua kuwapuuza na kuondoka zake,” amesema.

Amesema polisi walimfuatilia na kumkamata na sasa anaendelea kuhojiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.

“Atafikishwa mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

======

Mtolea amshukuru Mungu

"Alhamdulillah nimemalizana na Polisi ktk kesi ya kupikwa na mahakama imeridhia nilipe shilingi laki 3 tu.

Pesa imelipwa na niko huru. Kuendelea na mapambano baada ya kulala rumande siku 1.

Matukio haya ya kutukamata na kutuweka ndani hayatapunguza harakati. Bado tutamkosoa yoyote yule tena kwa kumtaja jina bila woga.

Asante wote mliojitokeza na mlio mbali kwa dua zenu".
Yaani ufanye kosa la wazi, ukutwe na hatia na kutozwa faini ya shilingi laki 3 na mahakama afu uje kulialia kuwa kesi ya kupikwa...
 
Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.
Tena usilete utani na bima...haikulazi ndani pekee bali kuna kifungo jela kinaweza kukuhusu cha hadi miaka mitatu. Inategemea hilo kosa la bima limetokea katika mazingira gani pia.
Subiri siku upate ajali ndogo au usisimame kwenye zebra na una gari lisilo na bima ndo utaujua utamu wake.
 
Sipendagi kurumbana na polisi maana wanaweza kukulaza ndani ili wakuoneshe wao wanaweza kufanya hivyo.
Na ndio maana huwa wakinikamata nawaambia waniandikie au wachukue rushwa, kupotezeana muda kisa 30000 hapana

Tujitahidi kuwa makini maana hawa watu wana hasira na sifa juu
Kukubali kuandikiwa Mara kwa Mara kunaweza kuwa na athari kwenye leseni yako, usishangae Sikh ukienda kurenew leseni ukaambiwa huna sifa za kurenew leseni kutokana na makosa mengi ya barabarani. Njia ya pili ulioichagua inaweza ikawa nzuri lakini ya hatari. Lililo bora zaidi ni kujitahidi kuepuka makosa ya barabarani, na pia wasikukute na kosa wanapokusimamisha kukukagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Kamanda!! Kama hujui inabidi ujue sasa!! Mnatafutwa kwa hali yeyote!!! Jitahidi uwe kwenye mstari maana kosa , jinai kuwa upande wa 2 awamu hii......sijui hata mmekosa nini kuwa upande wa 2?? Kosa lipi?? Visasi hadi mtapewa kesi za uhujumu au mauaji ! Nchi yetu sote!! Ukifanya ma visasi kwa faida ya nani? Ili iweje siku ukitoka na watu wako wakakomeshwa huoni ni upuuziii??? Watumishi Mungu maombi yao hayafiki kwa Mungu upewe busara japo kijiko kidogo cha chai??? Busara!!!!!!
 
Sina tatizo na kusimamia sheria. Nina tatizo na jinsi zinavyosimamiwa kwa kuchagua wapi sheria ifanye kazi wapi ifumbiwe macho

Tuliambiwa ma DC, RC, Wabunge n.k. hawakaguliwi vyeti kwasababu si 'watumishi wa umma'
Kauli hiyo ilikuwa tofauti na ya Ngeleja aliyesema 'amekuwa mtumishi wa umma' kwa miaka kadhaa

Kama sheria haichagui mbona ilitengenezwa kitu kukwepesha DC na RCs kukaguliwa vyeti
Sheria ingefuata mkondo bila kujali nafasi kuna mkoa usingekuwa na RC

Ile kesi ya kuvania clouds imeishia wapi? Mbona sheria haikufuata mkondo

Tusitumie sheria kukidhi haja za matamanio yetu, tutumie kama zilivyo bila kubagua
Kama wakati unaomba kazi ulitakiwa upeleke cheti fulani kama requirement basi unastahili kukaguliwa baadae kama kuna mashaka. Kama hakukuwa na requirement kabla ya kupewa hiyo kazi, logic yakutaka ukaguzi wa cheti utailetaje?
 
Hivi kutokuwa na bima ni kosa kisheria? Sheria ipi ya usalama barabarani inavunjwa? Vipi kuhusu bima za nyumba na Afya? Mwenye uelewa mpana alete jibu tafadhali.
 
Back
Top Bottom