Mbunge wa Serengeti(Chadema) Chacha Marwa ahoji uhalali wa Tume ya Uchaguzi(NEC)

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Mbunge wa Serengeti (Chadema) Chacha Marwa amesema Tume ya Uchaguzi (NEC) haiwezi kuwa huru kwa kuwa wakurugenzi ambao kimsingi ndio wasimamizi wa uchaguzi, waligombea ubunge na kushindwa, hawajawahi kujiuzulu uanachama katika vyama vyao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Septemba 4, 2018 wakati akiuliza swali ya nyongeza bungeni.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ofisa wa NEC hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

“Lakini wakurugenzi wengi ni wanachama wa CCM, wengi waligombea ubunge. Walioshindwa wameteuliwa lakini hawajajiuzulu ubunge. Matokeo yake wananyimwa fomu ama wanajificha wakati wa kurudisha fomu, “ amesema.

Amesema walinzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) maarufu green guard wamekuwa wakiwateka wapinzani wakati wa mikutano ya kampeni, hata yeye amewahi kukumbwa na jambo hilo.

“Hivi ndio tume huru ya uchaguzi? Huku tunapoenda mnataka hadi damu imwagike?” Amehoji Marwa na kukatizwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Ndugai amemueleza mbunge huyo kuwa maswali yake mawili yanatosha, anakoelekea anaweza kuzungumza kauli za kichochezi.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde amesema NEC inapimwa kutokana na majukumu yake kikatiba yalivyoainishwa katika ibara ya 74 ya Katiba.

“Ibara ya 74 ya Katiba imeainisha majukumu ya tume yakiingiliwa ndio tume inakosa uhuru. Sitaki kuamini kuwa tume sio huru,”amesema.

Kuhusu kutekwa, Mavunde amesema suala la kutekwa si la NEC bali ni kosa la kijinai na kwamba anatakiwa kuripoti polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio wanajua leo...... Kiama kinakuja 2020, wakizidi sana watakuwa wabunge 5 tu kutoka opposition kuingia bungeni
 
Alicho jibiwa na Spika ni kwamba isingekua huru wewe leo hii ungekuepo bungeni? na hilo jibu kuna mchangiaji mmoja jana alichangia humu kwamba endapo akiuliza swali hilo basi atarajie jibu kama hili na kweli ndicho kilichotokea.
 
Bahati mbaya sana, viongozi wetu wamekuwa wakificha ukweli wa vitu vingi sana, hata yanayolalamikiwa ni ya kweli. ndiyo maana nchi yetu haiendi mbele. ili nchi iende mbele yatupasa kwanza tukubali kuwa kuna maeneo hatuko sawa.
 
Mtukufu ameshapigilia msumali wa moto."Nimekuteuwa,nakulipa mshahara,halafu mtangaze mpinzani mshindi".Nafikiri amri hii ya amiri jeshi mkuu kwa aliowateuwa ndiyo MSIBA wa demokrasia.
Naamini spika atamwandikia barua mtukufu ili atenguwe kauli yake.
 
Mbunge wa Serengeti (Chadema) Chacha Marwa amesema Tume ya Uchaguzi (NEC) haiwezi kuwa huru kwa kuwa wakurugenzi ambao kimsingi ndio wasimamizi wa uchaguzi, waligombea ubunge na kushindwa, hawajawahi kujiuzulu uanachama katika vyama vyao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Septemba 4, 2018 wakati akiuliza swali ya nyongeza bungeni.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ofisa wa NEC hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

“Lakini wakurugenzi wengi ni wanachama wa CCM, wengi waligombea ubunge. Walioshindwa wameteuliwa lakini hawajajiuzulu ubunge. Matokeo yake wananyimwa fomu ama wanajificha wakati wa kurudisha fomu, “ amesema.

Amesema walinzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) maarufu green guard wamekuwa wakiwateka wapinzani wakati wa mikutano ya kampeni, hata yeye amewahi kukumbwa na jambo hilo.

“Hivi ndio tume huru ya uchaguzi? Huku tunapoenda mnataka hadi damu imwagike?” Amehoji Marwa na kukatizwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Ndugai amemueleza mbunge huyo kuwa maswali yake mawili yanatosha, anakoelekea anaweza kuzungumza kauli za kichochezi.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde amesema NEC inapimwa kutokana na majukumu yake kikatiba yalivyoainishwa katika ibara ya 74 ya Katiba.

“Ibara ya 74 ya Katiba imeainisha majukumu ya tume yakiingiliwa ndio tume inakosa uhuru. Sitaki kuamini kuwa tume sio huru,”amesema.

Kuhusu kutekwa, Mavunde amesema suala la kutekwa si la NEC bali ni kosa la kijinai na kwamba anatakiwa kuripoti polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Point of Correction, haitwi CHACHA MARWA Bali ni MWL.MARWA RYOBA CHACHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom