R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
SHIRIKA la Umoja Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo jijini Mwanza (SHIUMA), limetoa siku 14 kwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA), aombe radhi baada ya kubainika kwamba, alighushi barua aliyodai imeandikiwa na shirika hilo kwa ajili ya kumkataa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mbele ya uongozi wa SHIUMA pamoja na walezi wake, Mwenyekiti wa SHIUMA, Enest Masanja, alisema shirika hilo limesikitishwa na kitendo cha Mbunge Wenje, kuwaambia wananchi katika mkutano wake wa hadhara alioufanya katika Viwanja vya Sahara na kusema kwamba, SHIUMA wameandika barua kwake wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amwondoe madarakani Kabwe ndani ya siku 14, vinginevyo wamachinga wataandamana kumkataa.
Masanja alisema kwamba, SHIUMA imesikitishwa na kufedheheshwa na kitendo kilichofanywa na Wenje, kwani kililenga kuchonganisha SHIUMA na viongozi wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
Alisema kwamba, taarifa hiyo ni ya uongo, kwani wamachinga hawana ugomvi wowote na uongozi wa Jiji la Mwanza, kwani wamekuwa wakishirikiana muda wote na kwamba hawawezi kumtumia Wenje kuwasilisha kero zao hata kama zipo kwa kuwa wao si sehemu ya wanasiasa.
Hakuna barua yoyote tuliyoandika kwa Wenje na hakuna tamko lolote au mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina ya SHIUMA na Wenje.
Kuanzia leo tunatoa siku 14 kwa Wenje kuomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa kuudanganya umma kuwa tumewasilisha malalamiko kwake dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, sisi sio daraja la watu kama kina Wenje kutaka kutumia jina letu kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa, alisema.
Wanasiasa wa aina hii wamekuwa ndiyo chanzo cha mpasuko na mgawanyiko kwa wamachinga, kwa kuwa kauli zao ni za ndumila kuwili zilizojaa chuki, husuda na tamaa ya madaraka.
SHIUMA haiko tayari kutumiwa na wanasiasa na vyama vya siasa, SHIUMA itaendelea kushirikiana na Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa katika harakati za maendeleo ya kijamii ya wamachinga katika Jiji la Mwanza.
Kwa hiyo, nasema SHIUMA iko tayari kutii na kutekeleza kwa vitendo maelekezo yote kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza pamoja na uongozi wa Manispaa ya Ilemela.
Naye Mlezi wa SHIUMA, Alfred Wambura, alisema Wenje anapaswa kuchunga kauli zake ambazo amekuwa akizitoa zikiwa na lengo la kuchonganisha wananchi.
Alivishutumu vyombo vya dola kwa kushindwa kumchukulia hatua, ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kwa uchochezi anaouendeleza kwa wananchi wa Mwanza.
SHIUMA siyo chombo cha wahuni kama ambavyo anafikiria, ni vigumu kutoa taarifa zozote nzito kama hizo bila viongozi wa ngazi za juu kushirikishwa na ndiyo maana tumempatia siku 14 aombe radhi na kama akishindwa kufanya hivyo, tutamchukulia hatua ili iwe fundisho dhidi ya uropokaji wake, alisema Wambura.
Wenje alipotafutwa jana kupitia simu yake ya mkononi, hakupokea na badala yake akapokea mtu mmoja aliyejitambulisha kwamba ni msaidizi wake.
Mtu huyo alisema kwamba, Wenje asingeweza kupokea simu jana kwa sababu alikuwa kwenye vikao vya maandalizi ya harambee ya Vuguvugu la Mabadiliko M4C, iliyotarajiwa kufanyika jana jijini Mwanza.
Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika juzi katika Viwanja vya Sahara, Wenje alisema shirika la wamachinga limeandika barua kwake na kutoa siku 14 kwa Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Pinda, amwondoe Kabwe jijini Mwanza kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi ipasavyo.