Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA) adaiwa kughushi barua

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
SHIRIKA la Umoja Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo jijini Mwanza (SHIUMA), limetoa siku 14 kwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA), aombe radhi baada ya kubainika kwamba, alighushi barua aliyodai imeandikiwa na shirika hilo kwa ajili ya kumkataa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mbele ya uongozi wa SHIUMA pamoja na walezi wake, Mwenyekiti wa SHIUMA, Enest Masanja, alisema shirika hilo limesikitishwa na kitendo cha Mbunge Wenje, kuwaambia wananchi katika mkutano wake wa hadhara alioufanya katika Viwanja vya Sahara na kusema kwamba, SHIUMA wameandika barua kwake wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amwondoe madarakani Kabwe ndani ya siku 14, vinginevyo wamachinga wataandamana kumkataa.

Masanja alisema kwamba, SHIUMA imesikitishwa na kufedheheshwa na kitendo kilichofanywa na Wenje, kwani kililenga kuchonganisha SHIUMA na viongozi wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

Alisema kwamba, taarifa hiyo ni ya uongo, kwani wamachinga hawana ugomvi wowote na uongozi wa Jiji la Mwanza, kwani wamekuwa wakishirikiana muda wote na kwamba hawawezi kumtumia Wenje kuwasilisha kero zao hata kama zipo kwa kuwa wao si sehemu ya wanasiasa.

“Hakuna barua yoyote tuliyoandika kwa Wenje na hakuna tamko lolote au mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina ya SHIUMA na Wenje.

“Kuanzia leo tunatoa siku 14 kwa Wenje kuomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa kuudanganya umma kuwa tumewasilisha malalamiko kwake dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, sisi sio daraja la watu kama kina Wenje kutaka kutumia jina letu kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa,” alisema.

“Wanasiasa wa aina hii wamekuwa ndiyo chanzo cha mpasuko na mgawanyiko kwa wamachinga, kwa kuwa kauli zao ni za ndumila kuwili zilizojaa chuki, husuda na tamaa ya madaraka.

“SHIUMA haiko tayari kutumiwa na wanasiasa na vyama vya siasa, SHIUMA itaendelea kushirikiana na Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa katika harakati za maendeleo ya kijamii ya wamachinga katika Jiji la Mwanza.

“Kwa hiyo, nasema SHIUMA iko tayari kutii na kutekeleza kwa vitendo maelekezo yote kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza pamoja na uongozi wa Manispaa ya Ilemela.

Naye Mlezi wa SHIUMA, Alfred Wambura, alisema Wenje anapaswa kuchunga kauli zake ambazo amekuwa akizitoa zikiwa na lengo la kuchonganisha wananchi.

Alivishutumu vyombo vya dola kwa kushindwa kumchukulia hatua, ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kwa uchochezi anaouendeleza kwa wananchi wa Mwanza.

“SHIUMA siyo chombo cha wahuni kama ambavyo anafikiria, ni vigumu kutoa taarifa zozote nzito kama hizo bila viongozi wa ngazi za juu kushirikishwa na ndiyo maana tumempatia siku 14 aombe radhi na kama akishindwa kufanya hivyo, tutamchukulia hatua ili iwe fundisho dhidi ya uropokaji wake,” alisema Wambura.

Wenje alipotafutwa jana kupitia simu yake ya mkononi, hakupokea na badala yake akapokea mtu mmoja aliyejitambulisha kwamba ni msaidizi wake.

Mtu huyo alisema kwamba, Wenje asingeweza kupokea simu jana kwa sababu alikuwa kwenye vikao vya maandalizi ya harambee ya Vuguvugu la Mabadiliko M4C, iliyotarajiwa kufanyika jana jijini Mwanza.

Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika juzi katika Viwanja vya Sahara, Wenje alisema shirika la wamachinga limeandika barua kwake na kutoa siku 14 kwa Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Pinda, amwondoe Kabwe jijini Mwanza kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi ipasavyo.
 

Kichuli

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
320
0
Wamezoe viongozi wote wa cdm ni mabingwa wa kugushi nyaraka na barua kwa sababu ya kutafuta sifa ila sasa wameanza kuumbuka mmoja mmoja cha msingi wamachinga wampeleke mahakani ili liwe fundisho kwa watu wanao fanana na viongozi wa chadema!
 

gagonza

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
309
225
tusiwe na haraka ya kuhukumu tusubiri upande wa pili watakachotuambia,ili tuweze kubalance story
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,579
2,000
VIONGOZI Njaa wa SHIUMA washapewa 2,000 na Nape watoe Hilo Tamko
Kwanini wasingeto hilo tamko siku ileile Wenje alivyosoma ile Barua.
Na Magamba mtaicheza sana ngoma ya CDM
Peopleessssssssssssssssssssssssssssssssssss
 

Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
250
Gambaz in action....danganyeni watu waliombali na Mwanza si sie banang'wanza. Kebwe ni kweli kimeo na chingaz wala hatummind hata kidogo!
 

Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
2,000
Any way tusubiri kweli upande wa pili kwamba naye ana maoni gani kwa hili

Tatizo siku hizi humu JF imeingia mijitu inayotumia sehemu ya chini ya kupumulia kufikiri. Hata akitokea kichaa leo akatangaza jambo lolote linaloonekana baya kwa CDM yenyewe yanakwenda nyumbani kwao kufanya pati ya kujipongeza pasi na kuchunguza kwanza ukweli wa habari yenyewe. Hii ni mijitu ya ajabu sana! Na huenda hata huko Magambani a.k.a kwa "Wazee wa meno yua Tembo" hayapewi chochote! Yanaleta ushabiki kama wa simba na yanga humu.
 

kingukitano

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,971
0
Tatizo siku hizi humu JF imeingia mijitu inayotumia sehemu ya chini ya kupumulia kufikiri. Hata akitokea kichaa leo akatangaza jambo lolote linaloonekana baya kwa CDM yenyewe yanakwenda nyumbani kwao kufanya pati ya kujipongeza pasi na kuchunguza kwanza ukweli wa habari yenyewe. Hii ni mijitu ya ajabu sana! Na huenda hata huko Magambani a.k.a kwa "Wazee wa meno yua Tembo" hayapewi chochote! Yanaleta ushabiki kama wa simba na yanga humu.

Acha utani wewe ,mbunge anaropoka wewe unasema eti watu wnasherekea ,jambo baya kuhusu chadema cha msingi kwa nini anawasingizia wamachinga na wmekataa kutumika kipuuzi ungekua na akili ungesumbua ubongo wako hata kumuliza mbunge wako kuwa kwa nini anawasingizia,na kwa amefoji barua ?ninyi ndo mmelogwa hamuamini upuuzi unaofnywa na viongozi wenu mnakimbilia kutukana kila atakayeonesha uhyawani wa hao mnaowaona malaika ,uongozi wote wa machinga mwanza kuanzia mwenyekiti ,katibu na wajumbe wamelaani uhuni wa mbunge huyu ,wewe unaona kaonewa mbona hajitokezi kukanusha? Umelewa ushabiki wewe ,hii imekua janja ya wanasiasa wengi kuwagombanisha wananchi na serikali ili wao wapate madaraka upuuzi kabisa huu ,kwa hiyo unataka kutuambia kuwa mwenyekiti wa wamachinga ni kichaa? wewe ndo umenza kuonesha ukichaa kwa kudhani wabunge wako wako perfect na wakifanya upuuzi wasisemwe
 

lutome

Senior Member
Apr 18, 2012
148
195
Tatizo cdm hawatofautishi kampeni za siasa na uhamasishaji maendeleo wao kila siku porojo zilizojaa uanaharakati wa kijinga jinga, Imekuwa mazoea Wenje kuhubili uongo na chuki,alianza na kufitinisha madiwan wenziye sasa kahamia kwa machinga na Mkurugenzi,hakika ukivuma haraka utapotea haraka.
 

ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,985
2,000
Mzee mwenyewe hajitambui katika kuropoka kwake mbele ya wandishi wa habari akadai hakuna mtu alie juu ya sheria zaidi ya rais pekee,. Ebu pima uelewa wa huyo masanja
 

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,730
0
wenje kapewa siku 14 aombe radhi wa machinga,lakini kama kweli Wenje alitumia jina la wamachinga kwa lengo la kisiasa basi siasa ya Tanzania ina hatari ya kuwa ya kihuni na kitapeli
 

Elizabeth Dominic

Platinum Member
Dec 7, 2007
4,556
2,000
CCM Mwanza hawana chao labda wamebaki kushikiliwa na Wafanyabiashara wakubwa tu sioni vipi bado Wamachinga wawe na mahaba na CCM
 

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,639
2,000
Wamezoe viongozi wote wa cdm ni mabingwa wa kugushi nyaraka na barua kwa sababu ya kutafuta sifa ila sasa wameanza kuumbuka mmoja mmoja cha msingi wamachinga wampeleke mahakani ili liwe fundisho kwa watu wanao fanana na viongozi wa chadema!

Kichuli

Umesema "Wamezoe viongozi wote wa cdm ni mabingwa wa kugushi" au mimi tu ndiyo sijakuelewa. Hiyo kali ya mwaka, hebu tusaidie vitu viwili, mifano isiyo na shaka na kwa nini hamjawachukulia hatua kwa sababu kughushi ni jinai. Tuambientu kisha tukupatie zawadinya kusema ukweli, la sivyo unastahili zawadi ya kinyume chake.
 

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,451
1,170
Kwani umesahau kuwa huyu anayejiita Kiongozi aliwahi kuwageuka wenzake na wakataka kumpelekea kipigo baada ya kuhongwa na ccm ili akanushe kile walichokuwa wamekubaliana kwenye kikao chao!!
 

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
0
"UMOJA wa Shirika la Machinga jijini hapa (Shiuma) jana wameipinga kauli iliyotolewa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, aliyoitoa Novemba 28, kwa vyombo vya habari ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumfukuza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa sababu ya kutokuwa na imani naye. Akisoma tamko hilo mwenyekiti wa Shiuma, Ernest Matondo jana alisema kuwa umoja huo umesikitishwa na umefedheheshwa na taarifa ya Wenje na kusema haina ukweli wowote ndani yake kwa sababu wao hawajakaa na mbunge huyo kujadili kile ambacho alikisema." (MWANANCHI TAREHE 2 DEC 2012
 

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,688
1,500
hapo kuna jambo, maana wakati tamko linatolewa wamachinga walikuwepo, na wengine wakatoa shuhuda zao,
kwenye msafara wa mamba na ....
 

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
0
huyo kujadili kile ambacho alikisema."Kwa pamoja Shiuma inasema kuwa kauli hiyo ni ya uongo na ilikuwa inalenga kuleta uchonganishi kati ya Shiuma na Serikali na kati ya Serikali na wamachinga wa Jiji la Mwanza," alisema Matondo.

Alisema kuwa wanalaani kitendo cha mbunge huyo kutumia jukwaa la siasa kutoa taarifa za uongo kwa wananchi ili hali akitambua kuwa Shiuma si chama cha kisiasa na mbunge huyo hakuwa na mazungumzo yeyote na chama hicho katika kipindi alichotoa kauli hiyo.

"Tunapiga marufuku mtu yeyote hasa wanasiasa kuitumi Shiuma kama daraja la kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa umma, wanasiasa mara nyingi wamekuwa ndiyo chanzo cha mpasuko na mgawanyika kwa wamachinga kwa kauli zao na tumewagundua kuwa ni ‘ndumilakuwili,' "alisema Matondo alipokuwa akisoma tamko hilo.

Aliendelea kwa kusema kuwa Shiuma, haijihusishi na harakati za kisiasa na haipo tayari kutumiwa na wanasiasa kwa ajili ya masilahi ya vyama vya siasa na kudai kuwa umoja huo utafanya kazi zake katika misingi ya sheria za nchi hii kama kilivyosajiliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom