Mbunge wa Nkenge aendelee na ziara jimboni

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mbunge Jimbo la Nkenge Mhe. Florent Kyombo ameendelea na ziara yake jimboni, leo tarehe 22 Julai, 2023 amefanya mkutano na kuzungumza na wananchi wa kata ya Gera, iliyopo Wilaya ya Missenyi Mkoa wa Kagera.

Mhe. Kyombo amefanya kikao na viongozi wa CCM kata ya Gera katika kikao hicho aliwapatia Vitendea kazi ikiwemo Bendera za Chama, Vazi (T- shirt), Peni, Karatasi (Ream paper) na Mpira kwa ajili ya Michezo.

Pia Mhe. Kyombo amempokea Mhe. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati alipofika kukagua maendeleo ya Ujenzi wa mnada wa Kimataifa wa Mifugo ambao upo mpakani mwa Tanzania na Uganda ambao mnada huo unajengwa kwa thamani Shilingi milioni 350 lakini mpaka sasa milioni mbili zimeshatumika na mnada unaendelea kujengwa.

Pia Mhe. Ulega amekuja kuongea na Wafugaji kusikiliza changamoto zao za mnada huo kulinganishwa na minada miwili iliyopo upande wa Uganda ambao unafanya kazi sambamba na mnada huo.

Mhe. Ulega ameendelea kupokea maoni kutoka kwa wafugaji ni kwa nini mnada wetu haufanyi vizuri ukilinganisha na upande wa Uganda.

Wafugaji wameeleza kuwa kwa upande wa Uganda ng'ombe moja unalipishwa kwa kiasi cha shilingi elfu kumi ya uganda kwa thamani ya Tanzania ni takribani Shilingi elfu Saba lakini kwa upande wa Tanzania ngombe moja unalipishwa shilingi elfu thelathini na mbili, hivyo wafugaji wamekuwa wakitorosha mifugo kwenda upande wa Uganda kuuza ili mtu apate faida zaidi.

Mhe. Ulega amehaidi kulifanyia kazi suala hilo kwa sababu malipo ya awali ya tozo ni kwa mujibu wa sheria.View attachment 2696653View attachment 2696654View attachment 2696655View attachment 2696656View attachment 2696657View attachment 2696658View attachment 2696659
IMG-20230722-WA0309.jpg
 
Back
Top Bottom