R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood, ameng'ara mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, baada ya kufanikisha mradi wa uchimbaji wa visima vya maji 23 kwa ajili ya maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Kinana alizindua mradi huo wa maji ya visima mjini hapa juzi, wakati akiangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kupokea kero za wananchi ambapo alitumia nafasi hiyo kuzindua visima hivyo ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh milioni 363.
Akizungumzia zaidi miradi ya visima hivyo, Kinana, alisema mbunge huyo ameonyesha dhamira ya kweli ya kazi ya uongozi ambayo ameamua kuifanya kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wake.
Alisema umuhimu wa viongozi kuwatumikia wananchi ambao wameamua kuwachagua kwa ajili ya kuwatumikia na uchimbaji wa visima hivyo ni wazi kuwa kazi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM inafanyika vizuri na hilo ni jambo jema.
Alisema lengo la CCM ni kuona tatizo la maji linapata ufumbuzi na kilichofanywa na Abood ni moja ya mambo muhimu wakati Serikali nayo ikiendelea kuwatumikia wananchi wake, hasa kwa kuzingatia kuwa CCM ndiyo iliyoshika dola na Ilani yake ndiyo inatekelezwa.
Abood ameonyesha wazi kuwa anajali wananchi wake, anatambua wajibu wake na hii ndiyo sifa ya uongozi. Naamini kwa kazi hii atakuwa mbunge wenu kwa kipindi kirefu ndani ya jimbo hilo. Kila ninakopita naona anashangiliwa na wananchi wake na wanampenda, alisema Kinana.