Mbunge wa Kahama Mjini aishauri Serikali ifute tozo ya maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Michango ya Wabunge ya kuchangia maoni mbalimbali juu ya bajeti kuu ya Serikali imeendelea bungeni jijini Dodoma ambapo mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga,Jumanne Kishimba maarufu kwa jina Prof.Kishimba ameitaka serikali kufuta tozo la Maiti kwenye chumba cha kuhifadhia maiti [Mortuary]

Mhe.Kishimba ameshangaa kufuta na kusamehe tozo kwenye unga wa ngano huku tozo la Maiti kwenye Mortuary ambayo ni Tsh.Laki tano ikiwa inaendelea hivyo ameishauri serikali kurudisha tozo ya keki na kuweza kufuta tozo ya maiti.

Mhe.Kishimba amesema ni jambo la kushangaza kwa watu wanaofariki kwa waganga wa jadi hawadaiwi bili yoyote na hupewa huduma ikiwa ni pamoja na sanda lakini mtu anapofariki akiwa hospitalini anadaiwa bili kubwa hivyo ni vyema serikali ikaangalia upya suala hilo kwani hali hiyo husababisha baadhi ya maiti hukosa ndugu wa kuichukua hospitalini kwa kukwepa kulipa bili na tozo ya Mortuary kutokana na hali ngumu ya Maisha na kusababisha kuzikwa ovyo.

“Mnajua waheshimiwa wabunge sisi ni marehemu watarajiwa ,kasoro itakuwa muda,tarehe na wakati,tumesamehe tozo ya keki lakini kwenye tozo ya maiti inabaki palepale,haiwezekani mtu apoteze mtu halafu atozwe bili na fedha ameitoa wapi”Amesema.

Mbunge Kishimba amesema yawezekana watengeneza Bajeti wanaishi Osterbay hawajui hali ngumu za watanzania kwa kufuta tozo ya keki ambayo kwa watanzania walio wengi amedai haina tija kwao na hivyo kuna haja ya serikali kurudisha tozo hiyo na kufuta tozo ya Maiti kwenye Mortuary.

Aidha ,Mhe.Kishimba ameiomba serikali iruhusu wananchi pindi wanapoenda kutibiwa ikiwa hawana fedha waende na mifugo yao hospitalini kama dhamana ili kutibiwa haraka na kuokoa Maisha yao kwani bado kuna dhana ya baadhi ya jamii kanda ya ziwa kutokuwa na uelewa juu ya bima kwani hudhani kuwa kukata bima ni kujitakia ugonjwa au kifo na elimu inatakiwa itolewe zaidi.

Sambamba na hayo,Mhe,Kishimba amesema kuna haja kubwa ya serikali kupunguza tozo za X-RAY ili watu wengi wanunue na kupekeka hospitalini hali itakayosaidia kupata huduma za X-Ray kwa bei nafuu.
 
Kishimba ni 'creative' ana akili za ajabu za biashara. Kaongea halo halisi anatakiwa wampe kazi awashauri.
 
Bunge live wengi wangefaidi mchango wake, nadhani kuna haja kurudisha bunge live maana na CCM inao wabunge wenye uwezo was kutoa michango mizuri. Msukuma sio mbaya asipo ingia kukandia upinzani nae anauwezo wa hoja.
 
Miongoni mwa Wabunge wachache wa CCM wasiopelekwa na upepo(wanaojitambua). Maana CCM kuna makundi matano ya wabunge
1.Fuata upepo
2.Wasema chochote(wa kubwabwaja)
3.Maji kupwa maji kujaa.
4.Mabubu.
5.Wanaojitambua.
 
Ameongea point sana,kuna msiba ulitokea wa jirani yetu Muhimbili daah aisee acha kabisa,sikia tu
 
Labda ni kwa sababu wanajua fika kwamba bila CCM kuiba kura wasingekuwa hapo inashangaza yule was Buyungu Kigoma, was Kinondoni nk.
 
Hivi serikali ikifuta tozo zote itapata wapi pesa ya kuendesha shughuli zake! Maana unasikia tozo zifutwe, kodi ziondolewe, VAT ipunguzwe, sasa serikali itapata wapi hela?
 
Mheshimia Jumanne Kishimba', mbunge a Kahama Mjini akichangia bungeni ameshangazwa na serikali kutochukua hatua za kushughulika na kero kwa wanyonge ambao wanalazimishwa kulipia gharama za matibabu baada ya wagonjwa wao kufariki.

Aidha Hospitali zingine zinaenda mbali kabisa na kuzuia maiti.

Kwa kweli jambo hili ni kinyume cha mila zetu sisi waafrika na watanzania
Tumsaidie Mh. Kishimba kupaza sauti jambo hili likome.

Kama la taulo za kike limewezekana, la tohara ya wanaume imewezekana- tunashindwaje hili la maiti?
 
Unaposema ni kinyume na mila na desturi zetu unamaanisha nini?

Suluhu ni serikali kuhakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya not otherwise.

Wakiruhusu kutoa maiti kabla ya malipo nani atalipia gharama?
 
Unaposema ni kinyume na mila na desturi zetu unamaanisha nini?

Suluhu ni serikali kuhakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya not otherwise.

Wakiruhusu kutoa maiti kabla ya malipo nani atalipia gharama?
"mvuv, nani analipia tohara bure ya wanaume?
wewe umekulia kwenye uzungu hata kama hujaishi ulaya -rejea kwenye mchango wa Mh. Kishimba aliyekumbusha kuwa kwa desturi mtu akifia kwa mganga alikokuwa anamtibu- madai ya gharama za matibabu yanasitishwa. Aidha mganga anajiunga kuhakikisha maiti anazikwa kwa stahili zinavyotakiwa kwa mjibu wa mila na desturi.
Sasa hizi hospital ambazo zinasema zimegundua mgonjwa anaumwa malaria, zinatoa dawa ya malaria, na mgonjwa anakufa halafu bila aibu zinataka zilipwe- hii siyo sawa
Nakubaliana na wewe kuhusu suala la gharama na nani alipe- napendekeza serikali ilipe.
Hospitali zipeleke madai serikalini walipe- kwa hela kutoka wapi?- tutendeneze utaratibu basi.
Kwa kweli hiki ndicho kipimo cha serikali sikivu
 
Inategemea na gharama zenyewe.
Kuna dogo alipata ajali jana akafa Leo ndugu zakewanakwenda wanaambiwa wanadaiwa laki 5 za matibabu.
Unaposema ni kinyume na mila na desturi zetu unamaanisha nini?

Suluhu ni serikali kuhakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya not otherwise.

Wakiruhusu kutoa maiti kabla ya malipo nani atalipia gharama?
 
Back
Top Bottom