Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel(CHADEMA) ajivua wadhifa huo na kuhamia CCM

Kama ilivyo katika mapenzi, kuwa si kila mmoja huwa ni mpenzi bali wengine huwa ni wapenzi watazamaji!!!
Mniwie radhi kwa kauli hii kuwa nchi yetu bado haijatunukiwa wanasiasa wakomavu na wenye kusimamia nia njema ya chama chao, wengi wapo ku struggle ili wapate chochote. Mtu anapoacha ubunge kwa kigezo cha kumuunga mkono rais huyo ni muongo kwasababu kufanya uchaguzi ni gharama kuliko hata kumuunga mkono rais!!!
Watu wa namna hii nashauri hata utendaji wa kata wasipewe, maana ni wanafiki wanadhani wanakisaliti chama na wakati wanawasaliti wananchi walio wachagua.
Nyerere na wapigania uhuru wetu wangekuwa na fikra mbovu Kama hizi za kutamani tamani nadhani mpaka Leo tungekuwa colony la mwingereza, wazee wetu hawa hawakuikimbia TANU kwenda kumuunga mkono gavana Richard Turnbull. Walisimamia Nia yao moja na wakaridhika na kidogo walichokuwa nacho hatimaye tukafanikiwa kupeperusha bendera yetu na kutambulika kama Taifa.
*ANGALIZO KWA CCM*
Kuweni makini sana na wanademokrasia uchwara kama hawa.
Chama kisijivune kurusha vyavu katika dimbwi kubwa la samaki. Kumbukeni si vyote vinavyokuja ni samaki, kuna vyura na kenge pia.
Watu hawa wasio na misimamo wala uchungu na Taifa maskini kama hili, wanaoacha majimbo yao ili hela ambayo ingefanya shughuli zingine za maendeleo ikafanye uchaguzi wa marudio ktk majimbo yao ni wa kuogopa kama ukoma!!
Nashauri CDM wasikatishwe tamaa na hawa wanaharakati hewa.
*Ni maoni tu wapendwa *
ingetungwa sheria asiruhusiwe kugombea angalau miaka 5.msemo wa mwl aliyekula nyama mtu hataacha ataendelea.huko nako akikosa anayotaka cii atahamia kwingine
wangekuwa wanaohama ni wananchi wa kawaida ningestuka.ila hawa viongozi wala hainipi shida. kama ccm wana uwezo watununue wananchi

Kupanga watu anayewataka yeye kushika nafasi katika chama na kumkaribisha Lowassa na kumpinga Dr Slaa.

Mfano;
Nafasi ya katibu mkuu ilipaswa ateuliwe Mnyika na siyo Mashinji.

Kuzuia harakati ndani ya chama.
Mfano; UKUTA.

chama ni cha kwetu sisi wananchi.hawa wanaohama tuliwachagua sisi. usiwe na hofu
 
Laana ingeanza kwa Nyalandu ungeeleweka
Mkuu mimi nalisema hili kwa waheshimiwa wote wanaohama vyama vyao na kujiuzulu nafasi zao kabla muhula haujaisha. Mimi sikusema Nyarandu yuko sahihi, wewe ndo unaleta propaganda za vyama. Hoja yangu ipo kwenye matumizi mabaya ya fedha za umma kwa sababu zisizo za msingi. Muhula ukiisha mtu ahamie anakotaka. Wanasahau kuwa wanatuumiza Watanzania bila sababu za msingi.
 
Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ajiuzulu nafasi hiyo pamoja na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Disemba 14, 2017.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa ameshindwa kuukataa ukweli huu kuwa hivi sasa uongozi wa nchi yetu chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umedhihirisha wazi kupigania rasilimali za nchi na kwa kuwa niliomba ridhaa ya Ubunge kwa ahadi ya kupigania rasilimali za nchi nimejikuta sina namna nyingine zaidi ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu Ubunge wangu ili niungane na CCM katika jukumu hili muhimu kwa Taifa.

Nimefanikiwa kuipata barua yake ya kujiuzulu na kujivua uanachama wa CHADEMA;

Video




Jamani hawa watu ni washamba! Sasa dekokrasia ni nini?
 
Naamini ipo shida ndani ya chama hata kama tutaendelea kukimbia kivuli chetu kwa maneno waache waende chama kitabaki,ndio kitabaki je kubaki kwake ni kama nld au chaumma,ni ukweli usiopingika kuna ukandamizwaji mkubwa wa demokrasia ndani ya chama hakuna Uhuru wa mawazo wala mashauriano kwenye ujengaji wa nyumba iliyo imara kila mmoja apatapo fursa anaona bora aende zake kwa namna yyt kama ni kuhongwa kama tunavyojifariji au ni matashi ya mtu binafsi,wengi tuliomo humu ni mashabiki wala hatujui kinachoendelea mjengoni lkn ni mambo ya ajabu yanaamliwa na viongozi na kuwa msimamo wa pamoja hata kama mtaonekana kituko moja ya matukio kujiziba plasta,fujo zisizo na msingi,

kususa bila mpango kutengeneza matukio yasiyo na kichwa wala miguu ili jamii iwaonee huruma lkn kwa wanaojielewa wanaona upuuzi mtu mzima nashikiwa akili kujiziba plasta,mara kugoma,kuponda kila kitu hata tulichoshauri muda uliopita kikatekelezwa siruhusiwi kusifia kisa mpinzani kusema mabaya tu hakuna jema,mwisho wa siku anayejielewa kama Dr. Anaachia kwa namna yyt kuliko kuburutwa na mtu hata cheti hana kisa mamlaka,

zitto si wa aina hiyo kisa cha kuitwa msaliti upinzani haendeshwi na mihemko ya upinzani anasimamia anachoamini ndio maana alikuwa akiona leo kuna ujinga hafiki kabisa kikaoni kuliko kushushwa akili,

Sasa Leo lema amekuwa kama msemaji was chama kutengeneza tension kwa watu ooooooh Leo kuna mtu kanunuliwa ataondoka ili mradi ikitokea ionekane mfalme njozi, inafikia muda ndani ya nyumba wote kama familia ya panya baba, mama, watoto wa kike/kiume wote sharubu,ukijaribu kuchunguza mbunge kama silinde michango yake anatulia na wanaelewa anachokisimamia si mtu wa kukurupuka kama kusoma ameelimika sio kusogeza idadi ya madarasa si ajabu akaonekana msaliti,ifikie muda chama kijitathmini atabaki mmoja kwa tamaa/ujinga wa wachache.
Mdomo wa bata.
Umejenga hoja vizur sana. Kwa ufupi tu ni kwamba CDM inatakiwa kujitathimini sana na kukiri makosa. Wanafanya mambo ya hovyo wakitegemea madhaifu ya CCM yatawajenga. Umemzungumzia mtu kama Silinde my School mate huyu Mh. anajielewa sana na kwa trend hii for sure sidhan kama itavuka 2020 bado akiwa CDM. Time will tell!
 
hawa watu ndio wanachochea watu kukatana mapanga kwenye chaguzi za marudio
 
wewe ndio ninakuona akili yako ipo mbali-kwa nadharia ya ununuzi na uuzaji wa kitu chochote huwa hamna kulazimishana lakini kuna upande moja unakuwa na advantage kutokana na uhitaji wa upande mwingine kwa kujibu hoja husika viongozi wa upinzani hushawishiwa na wingi wa fedha wanazopewa,na fedha hizo hizo zinavyotumiwa vibaya na upande mwingine ndio ushawishi mkubwa-so fedha ndio hulaimisha wote wana makosa ila mwenye makosa zaidi ni anayetumia upungufu wa mwingine kwa kutotenda mema.
Ushawah jiuliza viongoz wa ccm wanawapata vip viongoz wa chadema had mazungumzo ya biashara yanaanza? swakli hili halina matinki maana kila mtu anajua popote penye ununuzi wa kitu fulani hapakosi sehemu ya kubadilishana huduma
Mkuu,ukishasema kushawishiwa tayari neno kulazimisha halipo.Na nashukuru kwa kujua kuwa chadema sasa ni soko na mnunuaji ccm anajua atapata bidhaa.Kimsingi ktk biashara hakuna kulazimisha.Mnunuaji atatumia utashi wowote ule kumlainisha muuzaji na pindi muuzaji akiona inalipa kulingana na maslai yake biashara ufanyika.Biashara ni maelewano,so biashara ya ccm na chadema ni ya maelewano.Hakuna anayeonewa wala kusema kuna mtu analazimishwa.NI JUKUMU LA MWENYE DUKA KUFUNGA DUKA LAKE kama ishara ya kuonesha biashara hakuna.NI WAKATI WA CHADEMA KUWEKA UZALENDO MBELE NA KUEPUKA MAZINGIRA YOYOTE YATAKAYOMFANYA MTEJA CCM KUJA KUWANUNUA.Watu huenda kwenye DUKA lililowazi sio lililofungwa.NI AIBU CHADEMA KULIA ETI MNANUNULIWA,HOW?MMEKUA NYANYA?
 
Mkuu,ukishasema kushawishiwa tayari neno kulazimisha halipo.Na nashukuru kwa kujua kuwa chadema sasa ni soko na mnunuaji ccm anajua atapata bidhaa.Kimsingi ktk biashara hakuna kulazimisha.Mnunuaji atatumia utashi wowote ule kumlainisha muuzaji na pindi muuzaji akiona inalipa kulingana na maslai yake biashara ufanyika.Biashara ni maelewano,so biashara ya ccm na chadema ni ya maelewano.Hakuna anayeonewa wala kusema kuna mtu analazimishwa.NI JUKUMU LA MWENYE DUKA KUFUNGA DUKA LAKE kama ishara ya kuonesha biashara hakuna.NI WAKATI WA CHADEMA KUWEKA UZALENDO MBELE NA KUEPUKA MAZINGIRA YOYOTE YATAKAYOMFANYA MTEJA CCM KUJA KUWANUNUA.Watu huenda kwenye DUKA lililowazi sio lililofungwa.NI AIBU CHADEMA KULIA ETI MNANUNULIWA,HOW?MMEKUA NYANYA?
unafurahisha hivi kati ya chadema na CCM chama kipi ni cha kizalendo-hivi CCM anayetumia kodi za wananchi kununua wabunge wa upinzani ndio mzalendo?.halafu unaposema CDM afunge afanye nini huku unajua fika CCM inatumia fedha za umma kufanikisha shughuli hiyo
 
Hawa Watu watakuwa wanarogwa si bure,kwa Mtu mwenye utimamu haewez lifanya hili
Wa kumlaumu Nyalandu yeye ndie alianza mchezo wa kujivua ubunge na kwenda chama kingine na alipofanya hivyo hatukusikia kelele zote hizo bali alionekana shujaa,ila wengine wakitumia haki yao wale wavuka mto Mara huja na kejeli na matusi kibao,basi hata Nyalandu atakuwa amerogwa
 
nyie mliohama wote ni wasaliti,

Kama CCM inavutia,ndio mlitakiwa mpigane ndani ya chama chenu, muweke strategies mpya kuwaatract wanachama wapya,sio kuhama,

Nawashangaa sana,mnataka turudi kwenye serikali ya chama kimoja,sidhani kama lipo duniani?????????????!!!!!!!!!!,

Tanzania haitawasamehe kwa hili,

wapinzani wapo kucreate balance,at least serikali inawork within boundaries,sasa mkicreate chama kimoja huoni kama mnmapa Rais afanye anavyotaka?????? akifanya lolote la hovyo mtakua na audacity ya kumkosoa ???demokresia ndio bye bye kulinda matumbo yenu!
 
Back
Top Bottom