TANZIA Mbunge wa Chalinze (Said Bwanamdogo) afariki dunia

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267


Source: EA Radio

Mbunge wa Chalinze (CCM) Mh. Said Bwanamdogo amefariki Dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupa MOI, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ofisi ya Bunge inaendelea na Taratibu za mazishi/maziko baada ya kuwasiliana na ndgu wa marehemu



NB: Tafadhali msiniulize ugonjwa maana haujasemwa
 
Apumzike kwa Amani...
Mh Said Bwanamdogo..
Yeye katangulia sisi tutafuata...
 
RIP mheshimiwa
Poleni ndugu jamaa marafiki na wananchi wa Chalinze
 
Mbunge wa Chalinze (CCM) Mh. Said Bwanamdogo amefariki Dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupa MOI, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ofisi ya Bunge inaendelea na Taratibu za mazishi/maziko baada ya kuwasiliana na ndgu wa marehemu

R.I.P Mh
 
Mwanga wa milele umwangazie e BWANA YESU mtanzania mwenzetu Said bwana mdogo waislamu waseme AMENI Wakristo Ameni
 
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze (CCM) Said Ramadhani Bwanamdogo amefariki dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupo ya MOI alipokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mbele yake, nyuma yetu.

Source East Africa radio
 
Mungu aiweke roho yake mahali inapostahili kutokana na matendo yake hapa duniani .
 
Ina-LiLLah Waina iLayhi Rajioun... kila nafsi itaonja mauti. Mwenyezi Mungu amlaze pema.AMIN
 
Poleni sana wafiwa.

Ila uchaguzi lini?
Maana jimbo liko wazi.
 
imekuaje kafia bongo( Taasisi ya Mifupa MOI )!!?.haya ni maajabu kuwahi kuyashuhudia kwa kiongozi aliyewakilisha chama kubwa na tajiri-CCM.RIP BWANA MDOGO.
 
Amefariki kipindi ambacho Operation pamoja daima inaingia tutegemee vifo kama hivi kwa magamba kuwa vingi wakati wa hii operation itakavyoanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…