Mbunge wa CCM atangaza mapema kupinga bajeti

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,074
Reaction score
34,844
1442.jpg

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, amesema hataiunga mkono bajeti ya serikali ya 2013/2014 kwa sababu haina jipya ikiwamo kukosekana kwa vyanzo vipya vya mapato na nidhamu katika upangaji wa matumizi.

Mpina akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, alisema baada ya kuisoma kwa makini bajeti hiyo amebainikuwa ina mapungufu mengi ikiwamo kutotengewa fedha za kutosha kwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

Pia sababu nyingine ilikuwa ni matumizi ya kawaida hususani matumizi mengineyo-OC kutengewa fedha lukuki.

“Nimepitia kwa kina bajeti na kugundua kuwa bajeti hiyo haipishani sana na bajeti zilizowahi kuwasilishwa miaka ya nyuma kutokana na sababu mbalimbali sitaiunga mkono kama serikali haitachukua hatua ya kuirekebisha,” alisema.

Alizitaja sababu za kutoiunga mkono bajeti hiyo kuwa ni matumizi mengineyo kuendelea kutengewa fedha nyingi badala ya matumizi mengineyo kupungua kama ambavyo serikali imekuwa ikiahidi mara kwa mara.

Alisema katika bajeti hii matumizi mengineyo yameongezeka toka Sh. trilioni 4.07 hadi Sh. trilioni 4.5 hii ni ongezeko la Sh. bilioni 430 sawa na ongezeko la 10.7%.

“Hali hii haiwezi kuendelea kukubalika fedha za umma kuendelea kutumiwa na wajanja wachache katika posho, semina huku Watanzania wengi wakiendelea kuteseka katika lindi la umasikini, miradi ya maendeleo kukosa fedha za kutosha,” alisema.

Kwa mujibu wa Mpina, katika mjadala wa bajeti unaoendelea baada ya serikali kubanwa na wabunge ikakubali kupunguza matumizi mengineyo kwa kiasi cha Sh. bilioni 283.5 na fedha hizo kupangiwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Maji, Uchukuzi, Viwanda, Vijana.

Kuhusu misamaha ya kodi, Serikali imekuwa ikiahidi kuchukua hatua ya kupunguza misamaha ya kodi katika hotuba za bajeti za serikali za tangu 2008/2009. lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika hadi kufikia ju Sh. trilioni 1.8 ikiwa ni 4.3% ya pato la taifa.

Kwa upande wa Deni la Taifa, limekua toka Sh. trilioni 20.27 (Machi 2012) hadi Sh. trilioni 23.67 (Machi 2013) ikiwa ni ongezeko Sh. trilioni 3.40 sawa na 17%.

Katika mwaka wa fedha 2012/2013 kiasi cha Sh. trilioni 2.7 kilitengwa kulipia deni la taifa wakati mwaka wa fedha ujao 2013/2014 kiasi cha Sh. trilioni 3.3 zimetengwa.

“Swali la kujiuliza ni kwanini Deni la Taifa likue kwa kasi kiasi hicho wakati kila mwaka tunatenga fedha kulipa deni pamoja na riba zake?” alihoji.

CHANZO: NIPASHE

Afazali muwe na concious kidogo. Maana at times unaweza kufikiri kuna zinjanthropuses ccm and not fully developed homo sapiens!
 
...mwisho wa siku...itapita kama zilivyopita nyingine...ni kuweka "balance" tu ionekane kuna watu wanapinga....
 
Naamini alikuwa anatafuta kulitangaza jina lake kwenye Media. haya tumesha muona ngoja tuone vitendo ndani ya nyumba.

Choo cha shimo hakiachi kunuka!
 
Kama ni kweli atakuwa miongoni mwa wabunge wanaowajali watu wao. Siyo kama mbunge mmoja nadhani viti maalum kutoka Rukwa ambaye jana alitumia dakika 5 kuhubiri kwa kutumia maandiko kutoka Biblia, kisha akatumia dakika 4 kumsifu rais pamoja na serikali yake, halafu akatumia dakika 1 kuzungumzia barabara na walimu wa Rukwa, na kisha akaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Hii ilikuwa ni kabla ya kuishukuru serikali kwa kutumia trilioni 18 mwaka huu badala ya zile 15 za mwaka jana. Sasa mtu unajiuliza, 'tunahitaji wabunge wa namna hii kweli?' Watu ambao IQ yao ni so low? Yaani nilimwangalia nikatamani kulia. Hata hivyo ninataka kumkumbusha kuwa tunatakiwa tuwatii wanaotuongoza kwa kila jambo jema tu. Siyo leo kiongozi aagize kuua watu wasio na hatia halafu wewe useme 'hewala bwana'. Acha kupotosha maandiko kwa faida yako wewe mbunge.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Yule mbunge wa jana wa viti maalum anaita ABIA NYABAKARI.. Kasifia sana bajeti.. Kampongeza sana jk kalalamika saana jimboni kwake hakuna maendeleo.. Mwishoni 100-100%
Kama ni kweli atakuwa miongoni mwa wabunge wanaowajali watu wao. Siyo kama mbunge mmoja nadhani viti maalum kutoka Rukwa ambaye jana alitumia dakika 5 kuhubiri kwa kutumia maandiko kutoka Biblia, kisha akatumia dakika 4 kumsifu rais pamoja na serikali yake, halafu akatumia dakika 1 kuzungumzia barabara na walimu wa Rukwa, na kisha akaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Hii ilikuwa ni kabla ya kuishukuru serikali kwa kutumia trilioni 18 mwaka huu badala ya zile 15 za mwaka jana. Sasa mtu unajiuliza, 'tunahitaji wabunge wa namna hii kweli?' Watu ambao IQ yao ni so low? Yaani nilimwangalia nikatamani kulia. Hata hivyo ninataka kumkumbusha kuwa tunatakiwa tuwatii wanaotuongoza kwa kila jambo jema tu. Siyo leo kiongozi aagize kuua watu wasio na hatia halafu wewe useme 'hewala bwana'. Acha kupotosha maandiko kwa faida yako wewe mbunge.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Anaongea tu huyo hana lolote anajeuri ya kupinga?
 
Mimi na mwamini mpina kwani ni mbunge wa kizazi kipya.ngoja tusubiri tuone.
 
labda kuwe na utaratibu wa kupiga kura bungeni
lakini sio ule wa ndiooooo au sioooo kisha spika kuamua.
kwa karne ya 21 bado tuko katika mfumo ndio sio bila kura kuhesabiwa.
 
Hongera Kijana naona "Kivuli" cha kuota kuwa Naibu Waziri wa Fedha kinakutesa Pole sana Kijana.

Uwaziri hautafutwi kwa namna hiyo na ile Suit uliyoishona kwa ajili ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha wewe endelea kuivaa wala usione aibu.

Sasa ulitaka kuwa Naibu Waziri wa Fedha ukafanye nini kwenye Wizara hiyo unayoieleza ni hatari?

POLE SANA KIJANA.
 
Mwisho wa yote, ataiunga mkono kwa 100%.

Itakapofika wakati wa kupiga kura kwa kuitwa majina atatakimbia kikao cha Bunge. Hana lolote huyo anatafuta hurua ya wa-Kisesa mwaka 2015. Janja yake kwisa gundua huyo asitutishe!!!
 
Back
Top Bottom