Mbunge wa Busanda (CCM) soma hapa

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,089
Madam Lauwrencia Masele Bukwimba, madam nakuheshimu sana ndio maana nikaamua kuandika kukukumbusha kuwa barabara katika jimbo lako ni mbovu .

Mfano barabara ya Kutoka Nyarugusu kwenda kwenu Nyabulolo kupitia s/msingi Kanyalu ni mbovu kabisa, magari yanakwama njiani kwa makorongo na mchanga uliojaa bara barani.

Fanya hima itengenezwe, pia umeme umeletwa lakini hauja pitishwa kwenda s/msingi Kanyalu kwenda Nyabulolo umekomea Nyarugusu mjini, kumbuka CCM inatekeleza mradi wa UMEME VIJIJINI (REA).

Unapocheza faulo kama hii ndio unawapa fursa wapinzani kufunga magoli maana haya matatizo ya maji,barabara na umeme ni kero kubwa kwa wananchi wa jimbo lako la Busanda. Bado unayo fursa jipange utatue kero hizi mbunge wangu.

Ningekuwa na e-mail yako ninge kutumia ila sikuwa na njia mbadala zaidi ya kutumia mtandao wa kijamii.

Kama viongozi wa kata na jimbo wanakuambia mambo safi wanakudanganya dada yangu mambo si shwari nenda ukajionee, toka Dar es salaan utaniamini ninachosema.
 
Huyu mbunge wa Busanda ni member was jf? Au ndo kama JK ana mgogoro na wafanyakazi halafu anaongea na Wazee wa Dar es salaam.
 
Mbona mbunge huyu aliisha waaga akasema msimjuejue na hatoi msaada tena uchaguzi ujao wala hagombei na anaeenda kuishi Dar kwa mumewe, wewe mtoa mada ulikuwa wapi wakati anaaga?
 
Nashauri tuwajumuishe Mkurugenzi wa wilaya na madiwani zinakopita hizo barabara mbovu
 
Mbona mbunge huyu aliisha waaga akasema msimjuejue na hatoi msaada tena uchaguzi ujao wala hagombei na anaeenda kuishi Dar kwa mumewe, wewe mtoa mada ulikuwa wapi wakati anaaga?

si razima kila mada uchangie ndugu, wewe unaweza ukaniambia aliaga kupitia media gani? Gazeti lipi? Radio ipi? Au unajua kila kitu siasa? Kweli humu kuna vichaa na hii ikiendelea itakuja kuwa kama facebook! Usimpakazie mtu kwa kuwa si chama chako treat people equally with dignity and not with bias.
 
Nashauri tuwajumuishe Mkurugenzi wa wilaya na madiwani zinakopita hizo barabara mbovu

Hayo ndio mawazo mazuri, sio kukimbilia uchama hapa wakati suala linagusa maisha ya kila mwananchi. Tuwe fair mambo ya chama weka pembeni ndio jamii forum itaheshimika sana. Angalia hoja na si chama wala dini.
 
si razima kila mada uchangie ndugu, wewe unaweza ukaniambia aliaga kupitia media gani? Gazeti lipi? Radio ipi? Au unajua kila kitu siasa? Kweli humu kuna vichaa na hii ikiendelea itakuja kuwa kama facebook! Usimpakazie mtu kwa kuwa si chama chako treat people equally with dignity and not with bias.

Umeamua tu kuwa huna adabu lakini akisema kabisa huko nyuma naona wewe hukusikia ulikuwa chooni unajisaidia
 
Mbunge kazi yake nikuwakilisha tatizo kwa watatuzi ambao ni serikali. Serikali inaendeshwa kwa sera na ilani ya chama ambacho kwa kuchakaa watendaji wamebumaa na ni mizigo. Kuna lile la maji safi na salama kwa wtz wote kwa umbali usiozidi mita 400 ifikapo 2015 likoje Busanda? Dreva anapozembea kuendesha gari lako, fukuza, ukisubirisha ni kulikuta gari hilo juu ya mapipa. CCM iondoe na mshauri aende chama kingine kitakachokuwa kikimsikiliza. Ni mzuri!
 
Kwani mbunge anahusika vipi na ujenzi au shughuli nyingine za maendeleo? Tuna haja ya kufahamu kazi za wabunge kabla hatujaanza kuwatupia lawama.
 
Kwani mbunge anahusika vipi na ujenzi au shughuli nyingine za maendeleo? Tuna haja ya kufahamu kazi za wabunge kabla hatujaanza kuwatupia lawama.

kazi ya mbunge ni kuwasilisha kero ya wananchi hasa wa jimbo lake, sasa jimbo lina kero kubwa ya maji, umeme, bara bara lakini mama wa watu bungeni hasemi. Muda unayoyoma, bara bara hazipitiki hasa za mtaa ndio hazitamaniki kabisa! Sasa kama hausiki kuzisemea basi labda barozi wa nyumba kumi anahusika? Au mimi sijui kazi ya mbunge maana mambo haya magumu jamani!
 
Back
Top Bottom