Mbunge viti maalum aibiwa baa!

hakutia saini, akome

Umekosea

Sema mlevi kaporwa baa! Wabunge hawaendi bar. They go to five star hotels. Kama Maige anaweza kununua Nyumba ya $ 400,000 za Kimarekani na Form alijaza za maadili then hatuna serikali. Hayo ni maneno ya Mbunge wa Katavi. Ndiyo maana amekuwa nanga wala ripoti ya Kamati hakuisoma who cares!
 
Nafikiri wakiendelea kufanyiwa tuvitendo km utwo basi watapunguza starehe na kuwa makin huku wakitambua kuwa wao ni kioo cha jamii.
Sijui kama kama makabrasha wanayopewa kama wanayasoma kwani asubuhi utaona bunge jeupe,kumbe wanakuwa wanakesha kwenye starehe hadi usiku wa manane na ndio maana wengi wao hulala usingizi mjengoni hadi mpaka washitulie na kelele za ndioooooo hiyo imepita ,ukiuliza imepita nini hawajui hawa ndio wabunge wetu siku hizi kila mbunge au waziri hutembea na dola waendeapo kwenye starehe,yaani hivyo ni vijisenti tu
 
Mhe. Mbunge anashangaa hali ya ujambazi katika Manispaa ya Dodoma wakati huu ambapo viongozi wengi wapo hapo mjini. Kwa hilo anataka kutueleza kuwa usalama ni kwa viongozi tu na siyo kwa raia. Jeshi la polisi ni kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao na si kwa viongozi kama anavyofikiri yeye. Kitu cha kujifunza hapa ni kwamba mara tu waondokapo hao viongozi, polisi wanazembea kwa vile pamoja na ukweli kuwa wao ni walinzi wa raia lakini wanawajibika zaidi kwa viongozi. Jeshi hilo halina budi kufanya kazi kwa ajili ya wananchi wote vinginevyo ile dhana ya polisi jamii ni usanii mtupu.
 
Back
Top Bottom