Mbunge Vedasto Ngombale (CUF) ''ahenyeshwa" na Magufuli Somanga

Hii ni sawa na kujitekenya mwenyewe then ukaanza kucheka mwenyewe......ni sawa na kutoa pesa mfuko wa shati na kuita press conference kuhamisha pesa hizo kwenda mfuko wa suruali.
 
Nasari huwa anatoa hela zake mfukoni kutekeleza miradi ya maendeleo? Kiongozi kuwajali wananchi kutoa pesa zake mfukoni kutekeleza miradi ya umma ndio utaratibu? Ukipata kiongozi muuza unga kwa mtindi huo utamlaumu nani? Rais yeye yuko juu ya sheria hatuwezi kumhoji, huyo mkurungenzi katoa hiyo 10m toka wapi? Atakuwa hauzi unga kweli?
Sasa Nasary huwa anatoa wapi hela zake?

Hapo anapozitoa ndio ilitakiwa na huyo mbunge atoe hapo!
 
Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi, amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajali wananchi wa Somanga!

Wananchi walipoomba zahanati, Magufuli ametoa 20 millioni, Mkurugenzi 10 millioni na mbunge ametoa 0 millioni!

NB:
Wapinzani mjiandae, Operesheni Funika Upinzani Imeanza!


Mbunge aliyepita alifanya jitihada gani kuleta hospital?
 
Hii ni sawa na kujitekenya mwenyewe then ukaanza kucheka mwenyewe......ni sawa na kutoa pesa mfuko wa shati na kuita press conference kuhamisha pesa hizo kwenda mfuko wa suruali.
Ccm wanataka kutudanganya
 
Kwani Mbunge alichaguliwa ili atoe michango kwenye hadhara ili kuifurahisha jamii?

Unajuaje kama hizo pia ni nyodo kama ahadi zake za kuwatetea wanyonge huku akigeuka moto mkali katika kuwaunguza wanyonge alioahidi kuwatetea?
Mkuu hakumwambia atoe pesa yake mfukoni bali zile anazolipwa na Serikali za kuendeleza jimbo. Ingawa kiukweli pale mkuu alimfanyia rafu kidogo mheshimiwa Mbunge.
 
Halafu ikifika 2020 wakishindwa uchaguzi wanaanza kulialia eti tume ya uchaguzi sio huru.

Muda huu baada ya kuutumia katika kuumiza kichwa kwenye kuyagusa maisha ya watu wa hali ya chini, wao wanahangaika na vyeti vya Makonda. Hii nchi imerogwa na mchawi ameshafariki siku nyingi zilizopita, mbaya zaidi hatujui kazikwa kaburi gani ili twende tukalitembelee.
Habari haijakaa sawa, kama huyo mkuu wa nchi atatoa kwenye mshahara wake ni sahihi kumsema mbunge, hata huyo mnayemuita mkurugenzi zikitoka katika mshahara wake nitaamini kweli wana nia ya dhati zaidi ya hapo ni ubabaishaji. Kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kutoa huduma kwa wananchi wake kwa kuwa inakusanya kodi. Ikifikia hatua kazi zinazotakiwa kufanyika wanafanya watu binafsi tena kutoka Serikalini ujue hatuna Serikali bali ubabaishaji. Lakini zaidi kama huyo mkurugenzi badala ya kujenga kituo cha afya kupitia halmashauri anayoingoza anasubiri Mhe. Rais aanzishe hakuna haja ya kuwa nae. HATUFAI leo, HATATUFAA kesho na atakuwa hajawahi KUFAA.
 
Mkuu hakumwambia atoe pesa yake mfukoni bali zile anazolipwa na Serikali za kuendeleza jimbo. Ingawa kiukweli pale mkuu alimfanyia rafu kidogo mheshimiwa Mbunge.
Kama nivyo ilivyokuwa basi kuna shida kuliko kawaida. Mfuko wa jimbo si uamuzi wa mtu mmoja, kama ilivyo kwa DED kuamua kutoa fedha bila kupitishwa katika kikao cha madiwani labda atoe za kwake mfukoni.
 
Pesa aliyotoa Magufuli ni kodi zetu watanzania, huyo Mkurugenzi ametoa pesa kwenye fungu la Halmashauri ya wilaya. Je, mbunge atatoa pesa kwenye taasisi ipi au ulitaka atoe mfukoni mwake ili wanawe wafe njaa? MaCCM bhana, hooooovyo!


Mbona Rais alikuwa clear tu..Ni kwenye Pesa za mfuko wa Jimbo
 
Ni kutoka kwenye source gani hiyo hela?
Mfuko wa jimbo mkuu
Wabunge wanapewa kila mwaka mfuko wa jimbo kwa ajiri ya maendeleo ya jimbo lake magufuli alikuwa sahihi kumuuliza amezigawanyaje?
Isijekuwa wanapewa harafu wanafanyia mambo yao tu
 
Rais na mkurugenzi walitoa hizo pesa kutoka katika akaunti za familia zao? Sio pesa za wananchi wenyewe? Umasikini na Ujinga, unaitafuna hii nchi.
Asilimia kubwa ni kodi za watanzania wakiwamo walioahidi
 
Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi, amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajali wananchi wa Somanga!

Wananchi walipoomba zahanati, Magufuli ametoa 20 millioni, Mkurugenzi 10 millioni na mbunge ametoa 0 millioni!

NB:
Wapinzani mjiandae, Operesheni Funika Upinzani Imeanza!



sasa huyo mkurugenzi 10m amezipata wapi ? kwa mshahara anaweza kutoa ? tusidanganyane wao wanapiga madili
kwani wao wametoa mfukoni ? si kuna mfuko wa rais ?
mbunge mshara wenyewe 2m na mpaka posho kuwe na vikao..
na kutoa sio lazima atoe akiwa na rais yeye yupo jimboni anafanya kazi na watu wake kila siku....Huko lindi wanajielewa sanaaaa ...zahanati na hospitali kujenga ni wajibu wa serikali inayo kusanya kodi ...
 
Back
Top Bottom