ChamaDola
JF-Expert Member
- Dec 23, 2016
- 3,431
- 2,804
Wakuu,
Katika ziara ya Mhe Rais katika Mkoa wa Lindi, amefanya mengi!
Ila moja la kufurahisha ni kumbwaga chini mbunge wa eneo husika katika kuwajali wananchi wa Somanga!
Wananchi walipoomba zahanati, Magufuli ametoa 20 millioni, Mkurugenzi 10 millioni na mbunge ametoa 0 millioni!
=======
Rais John Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale (CUF) baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi jana. Wa pili kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Picha na Ikulu
Rais, ambaye alitumia hafla tatu za jana kusisitiza umuhimu wa wananchi kutumia vyema mvua zilizoanza kunyesha ili wasijeibuka na kilio cha njaa mwakani, alilazimika kuanzisha harambee hiyo ya ghafla baada ya mkazi mmoja aliyepewa kipaza sauti kulalamika kuwa tatizo lao kubwa ni kituo cha afya.
Baada ya kilio hicho, Rais Magufuli, ambaye alikuwa amesimama juu ya gari, alimuita Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale (CUF), ili kumuhoji kuhusu fedha za mfuko huo na kiwango anachoweza kuchangia kwa ajili ya ujenzi wa kituo.
Rais: Wameshakulipa shilingi ngapi hadi sasa?
Mbunge: Za mfuko wa maendeleo ya jimbo? Mfuko wa maendeleo ya jimbo safari hii nimepata milioni 34 na laki nane.
Rais: Tangu uingie bungeni zimeshafika ngapi?
Mbunge: Hii ni mara ya pili
Rais: Kwa hiyo ni shilingi ngapi?
Mbunge: Kama milioni sabini hivi
Rais: Umeshapewa milioni sabini?
Mbunge: Ndio
Rais: Hapa umeachia ngapi, hapa Somanga?
Mbunge: Hapa Somanga nimeachia milioni tatu, lakini pia nimeachia shilingi milioni moja ya Shule ya Msingi Malendego na nyingine katika kata nyingine.
Rais: Sasa kwa nini usilete milioni 10 au 20 za hospitali ya hapa?
Mbunge: Mheshimiwa Rais, niahidi (kwa ajili ya) mwakani (anakatishwa)
Rais: Unazipeleka wapi hizo milioni sabini zote, unaleta milioni tatu. Ulete milioni 15 ili kusudi na mimi nichangie hapa? Tumalizane hapahapa leo.
Mbunge: Mheshimiwa Rais, niahidi kwa bajeti ya mwaka ujao (anakatishwa)
Rais: Ah, mimi nasema hizo ulizopewa milioni sabini, si bado zipo? (anakatishwa)
Mbunge: Hapana zimeshatumika (Rais anaendelea)
Rais: Unachangia milioni tatu tu, leta basi milioni 15 hapa na mimi nichangie. Jamani si mnataka na mimi nichangie? Sasa na mbunge achangie. Aseme anazipeleka wapi hizo?
Wakati akisema hayo mbunge huyo alishuka kutoka eneo ambalo alikuwa amesimama pembeni ya gari huku Rais akiendelea kuzungumzia umuhimu wa hospitali na baadaye kumtaka tena mbunge arudi alipokuwa amesimama ili atoe ahadi yake.
Rais: Hebu sema basi na mimi nisiondoke kabla sijachangia hapa.
Mbunge: Mheshimiwa Rais, pesa za meaendeleo ya mfuko wa Mbunge zimekuja mara mbili, mwaka jana 2015/16 na mwaka huu (rais anamkatisha).
Rais: Mheshimiwa mbunge unazungumza maneno mengi. Umesema umepewa milioni sabini, si ndio jamani. Sasa nataka utoe percentage (asilimia) tu kidogo, tuzimwage hapa na mimi nimwage.
Mbunge: Mheshimiwa Rais, msemakweli mpenzi wa Mungu (Rais anamkatisha)
Rais: Haya, unatoa milioni 15?
Mbunge: Si kwa bajeti ya mwaka huu, kwa sababu nilishazigawa. Na jimbo langu lina kata 13, hivyo pesa nyingine nimepeleka kata nyingine. Sasa nikisema nitazileta hapa Somanga, nitasema kitu ambacho sitaweza kukitekeleza.
Rais: Sasa wewe umetoka Dar es Salaam unapitia hapa Somanga, unaenda unazitoa (fedha) tu huko na hapa wana shida ya hospitali? Huoni kama unawaonea? Sasa mimi ngoja nijitolee mwenyewe, ila wananchi wanajua.
Baada ya kauli hiyo, Rais aliahidi kutoa Sh20 milioni na baadaye kumtaka mkurugenzi wa halmashauri atoe ahadi yake. Mkurugenzi huyo alisema kwa kuwa Rais ameahidi kutoa Sh20 milioni, halmashauri itatoa Sh10 milioni. Rais alianza ziara ya mikoa hiyo kwa kuzindua ujenzi wa kiwanda cha vigae Mkuranga mkoani Pwani ambako alirudia kauli yake kuwa hatatumia maneno matamu kwamba hakuna mtu atakayekufa njaa, akisisitiza kuwa asiyelima wala kufanya kazi atakufa njaa.
Rais alisisitiza ujumbe huo pia katika mikutano iliyofanyika Somanga na Nangulukulu.
Ujenzi wa kiwanda hicho cha kampuni ya Goodwill utagharimu dola 50 milioni za Kimarekani utakapokamilika.
Kauli ya Rais Magufuli kuhusu njaa imekuja siku moja baada ya taasisi ya Twaweza kutangaza matokeo ya utafiti yanayoonyesha kuwa takriban kaya 50 kati ya mia zinakabiliwa na upungufu wa chakula, ikiendelea mjadala ulioibuka mapema mwaka huu kuhusu tishio la njaa, huku Serikali ikisema ni baadhi ya maeneo tu yanayokabiliwa na upungufu wa chakula. Jana Rais Magufuli aliwataka wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha kwa kilimo badala ya kulia njaa. Rais alisema “hakuna vya bure” na kuwataka watu wafanye kazi kujitafutia chakula.
“Tumezoea kuambiwa maneno matamu kwamba hakuna mtu atakayekufa kwa njaa. Mimi nawaambia usipolima utakufa na njaa. Usipofanya kazi utakufa na njaa. Lazima niwaambie ukweli. Mlinichagua niwaambie ukweli,” alisema Rais huku akishangiliwa na wafanyakazi wa Goodwill.
“Hakuna vya bure, Serikali haitatoa cha bure. Na ukisubiri vya bure kwa miaka minne iliyobaki si utakufa?”
Mkuu huyo wa nchi aliwataka wanasiasa kutoogopa kusema ukweli kwa kuhofia kutochaguliwa, badala yake waseme ukweli wakati wote ili kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.
Rais alirejea ujumbe huo wakati akiwa Somanga ambako aliwaambia wananchi kuwa wanatakiwa kuzitumia mvua vizuri ili wasije kulalamikia baadaye suala la njaa.
“Tutumie ardhi hii na mvua hii kulima. Tulime ufuta, tulime korosho, tulime mahindi, tulime, mihogo, tulime tikitimaji, tulime kila kitu. Ili kusudi siku nyingine tusije kulalamika njaa,” alisema Rais.
Kauli ya “hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa” ilitolewa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete Julai 2014 akiwa ziarani Masasi, Mtwara baada ya wananchi wa kijiji cha Mwena kumlalamikia kuwa kulikuwa na tishio la njaa baada ya mazao yao kuharibiwa na mvua.
Hata hivyo, Rais Magufuli aliwataka wananchi wa Mkuranga kulinda amani katika maeneo yao ili kuvutia zaidi wawekezaji ambao wanazalisha ajira nyingi kwa Watanzania na kulipa kodi Serikani.
Rais pia alimtaka balozi wa China nchini kuachana na wazo la kujenga viwanda vya vigae nchi nyingine badala yake wajenge Tanzania na kuviuza katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na nchi za kusini mwa Afrika.
“Soko la bidhaa zenu lipo hasa kwa sababu Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ina watu milioni 165 na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) yenye idadi ya watu milioni 400. Kwa hiyo, hamna haja ya kwenda nchi nyingine,” alisema.
Alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni nafasi ya pekee kwa wananchi wa Mkuranga kwa sababu kitaajiri watu 1,000 mpaka 1,500. Aliipongeza Serikali ya mkoa huo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza ujenzi wa viwanda.
Awali, akizungumza katika uzinduzi huo, katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Adelhem Meru alisema tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madaraki mwaka 2015, miradi ya viwanda 2,163 imesajiliwa.
Dk Meru alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba malighafi hazisafirishwi kwenda nje ya nje badala yake bidhaa zisafirishwe kwa wingi ili kuongeza pato la Taifa na kutafuta masoko nje ya nchi.
“Tunataka mikoa yote nchini itenge maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda. Mkoa wa Pwani unafanya kazi nzuri ya kuvutia uwekezaji wa viwanda kama Rais alivyoahidi wakati wa kampeni mwaka juzi,” alisema.
Rais Magufuli pia alisisitiza agizo alilotoa la kupiga marufuku kusafirisha nje mchanga unaochimbwa migodini na kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kusimamia suala hilo.
Alisema Tanzania imekuwa ikiibiwa rasilimali zake na kunufaisha mataifa mengine badala ya kunufaisha wananchi. Alisisitiza kwamba mchanga ubaki Tanzania na kutafutiwa namna ya kuchemshwa hapa nchini kwa viwango vinavyokubalika. “Tuna madeni mengi nje ya nchi, yangekuwa yameisha. Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana. Sitaki kusikia mchanga unasafirishwa kwenda nje, wakitaka waanze kuchemsha huo mchanga hapa hapa nchini kwa ‘boiling point’ zilezile, inawezekana,” alisema.
Tishio la amani mkoani Pwani
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda, mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema serikali ya mkoa inapambana na vikundi vya watu vinavyotishia amani katika mkoa huo na kuhatarisha maisha ya watu na mali za wawekezaji.
Alisema kikosi maalumu cha Jeshi la Polisi kipo katika operesheni maalumu kuhakikisha waharifu hao hawapati nafasi ya kuharibu amani katika mkoa huo. Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi zitakazosaidia kuwakamata watu hao.
Rais Magufuli pia alifika katika Jimbo la Kilwa Kusini katika jimbo linaloongozwa na Mbunge wa CUF, Selemani Bungara ‘Bwege’.
Akizungumzia hali ya jimbo hilo, Bwege alisema linakabiliwa na tatizo la uvuvi haramu ambao umekuwa kero kubwa kwao.
Mbunge huyo alimuomba Rais asaidie wapate boti ya mwendo kasi ili kupambana na wavuvi haramu.
Pamoja na mambo mengine, Rais aliagiza wananchi waliovamia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi Nangurukuru, kuhama mara moja ili kuruhusu uje.
NB:
Wapinzani mjiandae, Operesheni Funika Upinzani Imeanza!