Mbunge Regina Ndege Aitaka Serikali Kufanya Tathmini ya Kina ili Kukabiliana na Athari za Maporomoko na Mafuriko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944

MBUNGE REGINA NDEGE AITAKA SERIKALI KUFANYA TATHMINI YA KINA ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA MAPOROMOKO NA MAFURIKO KWENYE MIUNDOMBINU

"Kuna mpango gani wa dharura wa kuzikarabati barabara za Vijijini zinazoharibiwa na mvua za Elinino katika mkoa wa Manyara?" - Mhe. Regina Ndege Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara

"Serikali imeshaanza kukarabati barabara za Vijijini zilizosababishwa na mvua za Elinino. Kiasi cha Shilingi Milioni 498 kimepelekwa TARURA Mkoa wa Manyara kwaajili ya kurekebisha uharibifu ikiwemo kuondoa matope barabarani, kuchonga barabara, kuweka changarawe, kuchimba na kusafisha mifereji na kurekebisha mikondo ya mito" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Naishukuru Serikali kwa namna walivyotukimbilia wananchi wa Manyara hususani Hanang tulipopata maporomoko ya matope. Nakushukuru Spika wa Bunge na Bunge lako kwa kutuletea misaada wananchi wa Hanang na Watanzania wote" - Mhe. Regina Ndege Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara

"Mvua za Elinino bado zinaendelea nchini hususani Mkoa wa Manyara, fedha zilizotengwa na Serikali ni kidogo ukizingatia athari tulizonazo. Je, Serikali haioni kuna haja ya kutoa fedha ya dharura kwaajili ya kukabiliana na hali halisi"? - Mhe. Regina Ndege Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara

"Maeneo mengi yameharibika, madaraja yamesombwa na wananchi hawana namna ya kupitia Maeneo mbalimbali. Je, Serikali haioni sasa kufanya tathmini ya kina ili kukabiliana na athari za maporomoko na mafuriko?" - Mhe. Regina Ndege Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara

"Milioni 498 iliyokwenda kwenye ukarabati wa miundombinu Hanang ni fedha ya dharura na siyo fedha iliyokuwa imetengwa na bajeti kwa TARURA Mkoa wa Manyara kwaajili ya kuhakikisha njia zinapitika wakati wote" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Tathimini ya kina inafanyika. Tayari TARURA imefanya Tathimini hadi kufikia mwisho wa Januari kuona athari za mvua Maeneo yote nchini na ni kiasi gani kinahitajika cha fedha kwaajili ya kukarabati barabara ili zipitike. Pia, Meneja TARURA nchini ameshatoa maelekezo" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
 

Attachments

  • GFFSMXpW4AA849X.jpg
    GFFSMXpW4AA849X.jpg
    90.8 KB · Views: 0
  • maxresdefaultqawsdcx.jpg
    maxresdefaultqawsdcx.jpg
    95 KB · Views: 0
  • maxresdefaultazxasw.jpg
    maxresdefaultazxasw.jpg
    84.9 KB · Views: 0
Back
Top Bottom