Mbunge na madiwani wa kariakoo tunamba ufafanuzi kuhusu hili

Speculator

Member
Mar 30, 2012
56
4
Wafanyabiashara wa kariakoo walio wengi wanatumia usafiri wa makontena kwa mizigo yao, nadhani ni sahihi kwa magari makubwa ya kontena kuzuiliwa kuingia katikati ya jiji sababu ya msongamano mabarabarani wakati wa mchana, wakapewa muda wa kushusha mizigo uwe usiku wakati ambao hakuna msongamano kabisa au kulipia ushuru(gharama za ziada) manispaa ili aweze kuruhusiwa kushusha mchana.(Tatizo letu ni usiku tu)
Swali letu na hasa chakushangaza tunaposhusha mizigo usiku bado watu wanajitokeza wa kila aina (manispaa,mgambo, polisi,TRA n.k) vitisho kibao ? Hamruhusi ? ni makosa ? kulipiswa faini ?
Je ni wakati gani muafaka na halali wa kushusha mizigo ya biashara ?
Je ushuru tunaopaswa kulipa ni kwa ajili gani ? usiku au mchana ?
Je ni kweli kuwa hakuna haki nchi hii kwa wafanyabiashara ? kwanini munawatoza mikodi kibao ?
Tukizingatia kuwa hizo ndizo shughuli za kiuchumi zinazowezesha serikali na wanachi wake kwani tunalipa kodi zote za TRA, Manispaa,n.k Halali kabisa toka huko nje hatupati shida hadi nyumba ndio taabu nyingi sana , rushwa nyingi , kila mtu mkubwa..
 
Back
Top Bottom