Mbunge Msigwa Chadema Iringa awa dawa ya michezo mashuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Msigwa Chadema Iringa awa dawa ya michezo mashuleni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]
  • Picha ya Kwanza: Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa mjini
  • Picha ya pili: Baadhi ya vifaa vya michezo alivyogawia timu za shule Iringa.
  Mbunge wetu achangamsha kongamano kwa kunukuu hotuba ya kaburu Botha ya mwaka 1985- pretoria, SA.

  Mbunge anafanyanini?

  Baaada ya shughuli ya uchaguzi kumalizika katika kata mbili za gangilonga na kitanzanini, Mh. Msigwa ameendelea na ziara mbalimbali katika jimbo la iringa mjini, amehudhuria katika sherehe za mahafari ya shule mbalimabali za sekondari na msingi na kugawa vifaa vya michezo. shule hizo nipamoja na IPOGOLO SEKONDARI, SEKONDARI YA WASABATO, SHULE YA MSINGI UGELE. PIA AMEGAWA VIFAA HIVYO KATIKA VILABU MBALMBALI IKIWEMO MSHINDO NA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA WANAWAKE. zoezi hili litaendele kwa kugwa jezi kwa timu zote za mpira wa miguu na netball.

  Pia hivi karibuni msigwa amefanya ziara katika maeneo mengine ikiwemo ofifisi za TRA, HOSPITALI YA MKOA, Ambako alitembelea wagonjwa na kuonana na watumishi katika hospitali, aliahidi kuchangia mashuka na net za mbu kwa Hospitali nzima. Ziara yake itaendelea katika maeneo tofauti ndani ya jimbo kabla ya kamati za bunge kuanza.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Wabunge wote wa ccm wapo wilaya ya kinondoni wanakula kuku!ndipo makazi yao yalipo
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Candid Scope bwana mbona hueleweki,juzi hapa ulikuwa unamponda jamaa na kumsifia Chiku Abwao. Kimekutokea nini mwenzetu au Mshiko?
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  ..asisahau kuwekeza kwenye ELIMU.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kigarama nilikuwa sijafahamu ideology yako, na kwa mtazamo wako kila linalokuja au kuletwa hapa utaliangalia kwa jicho la cheer na mleta mada utamwona kwa ideology hiyo hiyo

  Kwa taarifa yako jaribu kubadili mwono wako na kuniona mwanaharakati. Sishabikii mtu, sishabikii chama, sishabikii rangi ya chama. Mtazamo wangu ni wale awe nani na anatoka wapi mradi ana mlengo wa kimapinduzi katika kusukuma jitihada za kusonga mbele taifa letu nitamtangaza kwa nguvu zangu zote bila woga wala upendeleo. Mpaka hapo umenielewa? Sifungamani na mtu, wote wenye kutenda mazuri kwa nchi yetu nafungua moyo na akili yangu kuwatangawa kwa watanzania wengu na ulimwengu ujue mchango wao katika kujali maisha ya watanzania na taifa kwa jumla.  "Kushabikia mtu ni kujitumikisha nafsi yako na kujifungamanisha na unayemshabikia, si huru."

   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  safi sana mkuu.
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Luhanjo si alisema hawa jamaa wasielikwa kwenye sherehe za shule!
   
 8. D

  Dopas JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa maoni yangu ni sawa Mbunge au mtanzania yeyote kuchangia shughuli za jamii.
  Lakini sio kazi ya Mbunge. Hakuchaguliwa kwaajili ya kugawa misaada katika shule, hospitali au sijui wapi.

  Mbunge ni sauti ya watu. Ni sauti ya watu waliomtuma, wa jimbo lake, wa chama chake na watanzania wenye nia njema kwa ujumla.
  Kazi yao kubwa ni kufuatilia utendaji wa serikali iliyo madarakani kuhakikisha inawajibika kwa watu wake. Kwa upande mwingine kuhakikisha wananchi wanawajibika kujiletea maendeleo yao na pia kupata mahitaji yao msingi. Kuhakikisha kodi za wananchi zinatumika vizuri kwa maendeleo ya wananchi kama mwakilishi wa wananchi.
  Na mengine mengi. Tunafurahi tunaposikia kuwa halmashauri fulani imewawajibisha mafisadi, n.k.,

  Hilo la kuchangia shughuli mbalimbali za jamii ni sawa, ila wasijisahau wakabaki kwenye hilo tu. Hilo linaweza kufanywa na mtu yeyoye mwenye nia njema katika jamii.
   
 9. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeniwahi mkuu.
   
 10. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mh Msigwa kaza buti hakuna kurudi nyuma.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni dhahiri mbunge si ATM ya wapiga kura. Lakini tukumbuke kwa hali ilivyo Tanzania, serikali inayoundwa baada ya uchaguzi watumishi wake wanaanza rasmi likizo honey-moon. Wabunge ndio wanaoonekana kwa wananchi na wanaonekana kuelewa shida zao. Wanapoigeukia serikali kueleza matatizo yanayowakabili wananchi, inabadilika serikali kuongeza pamba masikioni athari yake kuonekana mbunge kama hawawakilishi vema wananchi, maana atakaporudi kuomba kura atakachoambiwa ni kwa nini ahadi za awali hajafanya. Pamoja na ule ubinadamu ambao wabunge wengi wameweka kando, wachache kama hawa wanaosaidia wananchi wanaonja taabu na machungu wanayopata wapigakura wao, na kumbuka wengi wao ni wazaliwa wa majimbo hayo, msukumo wa kifamilia na damu unawafanya wanachopata kushirikisha wapiga kura wao. Tunahitaji viongozi wetu kuwa na moyo huo, na huenda hawa wabunge wanaoleta mfano mzuri wa utendaji majimboni mwao wakishika nyadhifa za juu serikalini baadaye wanaweza kuwa chachu katika safu ya utendaji serikalini.
   
 12. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Bado tuko nyuma kweli ndo maana wabunge bado watabaki kulinda maslahi yao mfano nyongeza za mishahara nakutotozwa kodi.Itabaki hivyo kwani wanajua wakija majimboni lazima watoe fadhira kwa wapigakula wao na hapo mtu atasema rushwa kwenye chaguzi itaisha.
  Nadhani ingekuwa vyema leo tunaambiwa na Msigwa kuwa serikali kupitia wizara ya habari,utamaduni na michezo ameishinikiza mpaka ikatoa vifaa vya michezo kwa kila shule kwani kila Halmashauri ina idara ya utamaduni na michezo. Je wanafanya kazi na yeye amewaajibisha kivipi?
  Haadi ya kugawa net za kuzuia mbu hospitali ya mkoa ni kazi ya wizara ya afya.Je wizara imeshindwa au hakuna mtu makini wa kupaza sauti kuhusu hili na kuiwajibisha wizara?Tukienda hivyo basi itafika hata mabadiriko tunayo yataka kubaki kwenye makabrasha.Wananchi wengi kwakuwa wananjaa na elimu ya uraia haijatosha basi watabaki kumtegemea mbunge kuliko kuiwajibisha serikali na ndo hapo mtu atapiga kula kufuata kauli hizi ATATUPA NINI AU ALITUPATIA NINI!
   
 13. MALI YA BABA

  MALI YA BABA JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri kusaidia jamii kama mbunge Msigwa anavyofanya nampongeza kwa hilo!! Ila Mh.Msigwa pia ni vizuri baada ya hiyo ziara yako uwabane hao watendaji wa Halmshauri kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo kusudi wananchi wajue kodi zao zinatumikaje katika kuwaletea maendeleo jimboni kwao!
   
 14. O

  Omr JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si bora angenunua majembe, kuliko hivyo vijezi njaa vya kariakoo
   
 15. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Omr umeishiwa,vijezi vya k/k unajua vinahitajika kwa kiasi gani hapa nchini?achilia mbali vijezi ni wabunge wangapi wa ccm wameweza kutoa hata box moja la chaki kwa shule za kata zinazokosa mpaka pesa ya kununulia chaki na kufikia kuazimana wao na shule za msingi,unalijua hilo?

  Sasa usipoweza kukithamini kidogo katika mda muafaka hautaweza pia kukithamini kilicho kikubwa,mfano kuna Mbunge wa Sikonge,S.Nkumba ana miaka 11 sasa ni mbunge lakini hajawahi kutoa hata mpira 1 wa miguu kwenye shule iwayo wala kata yoyote achilia mbali vijezi vya k/k na huduma zingine muhimu

  Tunasema mazoezi na michezo ni njia mojawapo ya kupunguza maambukizi,kupunguza vitendo vya uharifu na sehemu ya ajira kwa sasa,sasa unapoamua kusaidia kwa upande huu inakuwaje tena huonekane mbaya?
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Waziri wa Chama cha magamba vigumu kukubali shinikizo toka mbunge wa Chadema kwa hoja za kushindana kiitikadi.
   
Loading...