R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Wakati wabunge wakiendelea kuijadili bajeti kuu ya serikali trilion 29.5, Mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani maarufu kama Maji marefu amesimama bungeni kuhoji sababu za serikali kusahau kuongelea suala la sukari katika bajeti yake.
Maji marefu amesema…>>>’Mmeacha bei ya petrol kama ilivyo, ningeomba mpandishe. Maana ya kupunguza bei ya mafuta inamaana wasafiri wapunguziwe gharama lakini hakuna mtanzania yeyote ambaye amepunguziwa gharama za nauli‘
‘Kwasababu hatufaidiki kwa lolote ningeomba mpandishe petrol mtupunguzie sukari, sukari hamjaiongelea hapa lakini sukari ni kitu muhimu sana kwa Watanzania.