Mbunge Mahawanga Janeth atoa tani tano za saruji kwa UWT wilaya ya Kigamboni

pitapiti

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
398
261
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth leo amekutana na Kamati ya Ujenzi na Uongozi wa Jumuiya ya Wanawake Wilaya ya Kigamboni na kukabidhi tani tano za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Kigamboni unaoendelea.

Mh. Mahawanga amefurahishwa na hatua nzuri inayofanywa na Kamati hiyo pamoja na uongozi mzima wa UWT Wilaya kwa kusimamia vyema zoezi hilo la ujenzi wa nyumba hizo za Watumishi unaoendelea katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa tani tano kwa kila wilaya ambapo alikwisha kabidhi katika Wilaya ya Temeke na Kinondoni na leo amekabidhi Kigamboni.

Aidha Mh. Mahawanga amesisitiza kuendelea kushirikiana nao kwenye kila hatua za ujenzi huo ili kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika kwa wakati lakini pia kuendelea kuungana pamoja kama Jumuiya kutekeleza jukumu hilo la ujenzi.

Mh. Mahawanga ametumia muda huo kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya ujao wa 2022 sambamba na kuwashukuru kwa kipindi chote ambacho wameshirikiana katika mwaka huu 2021 unaokwenda kuisha na kuahidi kuendelea kushirikiana nao pamoja kwa vipindi vinavyokuja mwakani kuhakikisha Jumuiya ya Wanawake ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam inazidi kuwa imara sambamba na wanafikia lengo kubwa la kumkwamua Mwanamke kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigamboni amempongeza Mh. Mahawanga kwa utekelezaji wa ahadi yake mapema na kumhakikishia kamati itasimamia vyema ujenzi huo na watazidi kushirikiana kama timu ili kuhakikisha lengo linatimi. Pia amempongeza sana kwa kazi nzuri anayofanya ya kuhakikisha fursa za kuwainua Wanawake zinazidi kuwafikia Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam sambamba na kutoa Elimu kuhusiana na vikundi, kuwakutanisha na Wadau mbalimbali ili kuweza kufikia lengo kuu la kuwainua na kuwakwamua wanawake kiuchumi.
 
Sema mifuko 100 ambayo amefadhiliwa sehemu bure
Thamani ya hiyo mifuko kwa bei ya rejareja14,500 kwa hiyo hako ka msaada kake huyo mbunge wa vitu maalumu kwa viongozi maalumu wa chama cha majambazi ni sh1,450,000 tuna
Wakati kwa mwezi anavuta 12m
 
Back
Top Bottom