Mbunge Kigua(CCM): Ujio wa Gwajima katika kamati ulikuwa wa dharau na kejeli uliopitiliza

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Dodoma.
Mbunge wa Kilindi (CCM) nchini Tanzania, Omary Kigua amesema ujio wa Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu shauri lake la kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge ulikuwa wa dharau na kejeli.

Kigua ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 31, 2021 wakati akichangia katika ripoti ya kamati hiyo kuhusu shauri la mbunge huyo.

Amesema wameshuhudia vituko katika kamati hiyo na kwamba vitendo vya mbunge huyo havifanani na nafasi aliyonayo katika Bunge.

“Shahidi (Gwajima) hakuitendea haki hakuwa na nidhamu, heshima na hata ujio wake katika kamati ulikuwa wa dharau na kejeli uliopitiliza,”amesema Kigua.
 
gC5ex.jpg
 
Haha mataga mnavurugana wenyewe.

Muambie huyu kibwetere wenu achague moja, kula posho au sadaka za misukule!
Definitely atachagua sadaka za mazombie... akiyadanganya anafufua wafu wanapiga makofi na vigelegele.... akiwaambia anawaletea treni wanatoa sadaka kwa wingi
 
Gwajima ana dharau ,kedi na dhihaka......

#SiempreCCM

HASHTAG CCM IMFUKUZE GWAJIMA
 
Siku hizi nimeacha kabisa kufuatilia Bunge kwa sababu hata Mbunge anayeniwakilisha huko si halali.

Hizi drama zinazoendelea nahisi wanajipanga kumfanyia impeachment mtu fulani....
 
Dodoma.
Mbunge wa Kilindi (CCM) nchini Tanzania, Omary Kigua amesema ujio wa Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu shauri lake la kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge ulikuwa wa dharau na kejeli.

Kigua ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 31, 2021 wakati akichangia katika ripoti ya kamati hiyo kuhusu shauri la mbunge huyo.

Amesema wameshuhudia vituko katika kamati hiyo na kwamba vitendo vya mbunge huyo havifanani na nafasi aliyonayo katika Bunge.

“Shahidi (Gwajima) hakuitendea haki hakuwa na nidhamu, heshima na hata ujio wake katika kamati ulikuwa wa dharau na kejeli uliopitiliza,”amesema Kigua.
watu wenyewe acha mdharaulike mliingia bungeni kwa mbinu haramu msitegemee heshima yoyote kutoka kwa mtu yeyote
 
Back
Top Bottom