Mbunge: Jitihada zinazotumika kukamata wavuvi ni kubwa kuliko zinazotumika kuwawezesha

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mhandisi Stella Manyanya amesema jitihada za Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kukamata wanaotumia nyavu zisizofaa au kwenye masuala yanayohusu ukusanyaji mapato ni kubwa kuliko zinazotumika kuwawezesha

Mbunge huyo wa Jimbo la Nyasa amehoji kwanini mikopo ya injini za boti isitolewe kwa mtu mmoja mmoja kuliko kupitia vikundi, jambo analosema linachelewesha ukuaji wa sekta ya uvuvi

Akimjibu, Naibu Waziri Abdallah Hamis Ulega amesema Ilani ya CCM inaelekeza Serikali kuhamasisha uanzishwaji wa Vikundi na Vyama vya Ushirika kwa lengo la kuwapa mtaji, ujuzi na vifaa ili kuongeza uzalishaji Ajira na kipato
 
Back
Top Bottom