Mbunge James Lembeli arudisha kadi ya CCM, kuhamia CHADEMA

Mbunge James Lembeli arudisha kadi ya CCM, kuhamia CHADEMA

MWAKATA KWETU

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
560
Reaction score
320
Mbunge James Lembeli anahamia CHADEMA. Akiwa Ofisi za CCM, amedai CCM inanuka Rushwa na hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uozo huo; hatogombea Ubunge tena kupitia CCM.

Kabla ya uamuzi huo, Lembeli amekuwa akilalamikia chama chake kubeba baadhi ya wagombea; kujenga makundi ya wanamtandao na kuanza kampeni kabla ya muda.

“Sitaki kuwa sehemu ya uchafu huu. Hivyo, nimeamua kutogombea ubunge kupitia CCM, ingawa nitagombea kupitia chama kingine,” ameeleza.

Amesema katika ziara zake jimboni amekuwa akipokea kadi nyingi ambazo zimetolewa na wagombea kinyume cha taratibu na taarifa hizo alizifikisha katika ofisi ya wilaya lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Mara baada ya kutoa shutuma hizo, Lembeli aliondoka katika ofisi hizo bila kusalimiana na katibu wa chama hicho wilayani Kahama ambaye alikuja kumsubiri ili amkabidhi fomu ya Kugombea ubunge tena.
 
Watu wengi utawasikia mimi ubunge ntawapa upinzani,
lakini Rais CCM. Ukiwauliza kwanini watakwambia ahaa
tunataka kuwe na wabunge wengi wa upinzani, ili CCM
wasiweze kupitisha mambo kirahisi, na kusiwe na habari ya
ndioooo.
Wapo sahihi lakini jambo wasilolijua ni kwamba kura unayo
mpa Rais ndio inayo tumika kuongeza idadi ya wabunge wa
viti maalum wa chama husika. Kwamfano ukimchagua
magufuli ujue kura yako imemchagua Wema Sepetu, Shishi
baby, na khadija kopa kwenye ubunge wa viti maalum.
Kwamaana hata ukimchagua mbunge wa upinzani jimboni
ujue kura uliyo mpa rais wa ccm imeenda kuwachagua
wabunge viti maalum wa CCM zaid ya 100.
Kwahiyo niwakati wako wa kuamua kua moto au baridi na
sio vuguvugu.
 
Kama huna rushwa ya kutoa ili upite kwenye kura za maoni ni bora ukimbie mapema
 
Never wako wakuhama ccm kwenda chadema,lowasas team ndiyo wahusika wakuu
 
Back
Top Bottom