Mbunge huyu wa Jimbo la Kilombero !!!!

Mbunge huyu wa Jimbo la Kilombero !!!!

Alex Mponela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
254
Reaction score
109
Siku za karibuni nilipata fursa ya kusafiri na msafara wa maiti kuelekea Ifakara kijiji cha Mngeta nikitokea Kilimanjaro hospitali ya KCMC.

Nilijionea uzuri na utajiri wa rasilimali mbalimbali ikiwemo ardhi yenye rutuba sana Wilayani Kilombero. Kilichonishangaza sana ni kuwa watu wa maeneo hayo wako nyuma sana kimaendeleo.

Ukosefu wa miundo mbinu ya uhakika ikiwem barabara, ndiyo sababu kubwa inayochangia haya yote.

Lami inaishia Ruaha darajani tu tokea mikumi na ilijengwa wakati wa M bunge aitwaye Gulamali na tokea hapo hakuna jitihada za makusudi zilizofanyika mpaka sasa kuboresha miundo mbinu hiyo.

Wenyeji wa huko wanalalamika sana kuwa licha ya Mngeta kuwa ni kitovu cha uzalishaji mpunga na licha ya umeme wa kihansi kupitisha nguzo kijijini hapo lakini hakuna umeme wala nini!!

Mbunge wao aitwaye Abdul Mteketa hana hata chembe ya jitihada kuboresha hali hii!!!! Anaona sifa kuimbwa kwenye vyombo vya muziki eti Pedejee Abdul Mteketa!!! Sasa wanasema wananchi wa huko kuwa asubiri 2015 !!!! Atakuwa pedejee zaidi!!!!
 
CCM Oyeeee 2015 Uchaguzi mkuu ni kusuka au kunyoa
 
Tanzania imerogwa sii bure hii haiwezekani...
 
mkuu hayo majimbo mawili jimbo la kilombero na jimbo la mikumi hakuna wabunge kabisa kwa sababu wanauwezo mdogo sana hawawezi tetea wananchi wao hata kidogo hilo jimbo la mikumi kuna mito chungumzima lakin hakuna maji hata kidogo mbunge amelala tu bungen
poor mteketa
poor sasi
poor ccm
 
mkuu hayo majimbo mawili jimbo la kilombero na jimbo la mikumi hakuna wabunge kabisa kwa sababu wanauwezo mdogo sana hawawezi tetea wananchi wao hata kidogo hilo jimbo la mikumi kuna mito chungumzima lakin hakuna maji hata kidogo mbunge amelala tu bungen
poor mteketa
poor sasi
poor ccm

Kuna yule mwingine Innocent Kallogeris bomu kweli kweli na mwingine wa Ulanga Magharibi Dr Mponda ni mizigo. CDM majimbo hayo
 
Kuna yule mwingine Innocent Kallogeris bomu kweli kweli na mwingine wa Ulanga Magharibi Dr Mponda ni mizigo. CDM majimbo hayo

ila sasa hivi hayo majimbo kuyapata tena ccm kazi wafanye
 
mkuu ccm hawataki poteza hayo majimbo mawil wanajua makamanda wakichukua hali itukuwa mbaya mana wanamaslahi yao kwenye hivyo viwanda hapo tangu nizaliwe sijawah sikia mbunge wa hayo majimbo anatetea maslahi ya wananchi kabisaa
 
mkuu ccm hawataki poteza hayo majimbo mawil wanajua makamanda wakichukua hali itukwa

Kuna unauhakika wa majimbo 5

Morogoro mjini

Kilombero

Ulanga magharibi

Jimbo la Kilosa

Jimbo lililo chini ya Innocent Kallogeris
 
Majimbo yote ya morogoro nadhani hakuna lenye afaadhali! Yote wabunge wanakoroma na usingizi mzito! Subirini mtapata muda wa kulala vizuri!
 
Kuna yule mwingine Innocent Kallogeris bomu kweli kweli na mwingine wa Ulanga Magharibi Dr Mponda ni mizigo. CDM majimbo hayo

Nadhani Mheshimiwa Celine Kombani ndiye at least kati ya wabunge wa mkoa wa Morogoro!
 
Celine ameendeleza sana jimbo lake. Kazi ya ziada inahitajika kule kwa wapogoro. Atachagulika si kwasababu ya chama chake
 
Mbunge wa Kilombero ni rafiki mkubwa wa akina Alex Massawe na Papaa Msoffe, wananchi wakadanganyika na mbembwe na kugawiwa vijihela, pole zao.
 
Siku za karibuni nilipata fursa ya kusafiri na msafara wa maiti kuelekea Ifakara kijiji cha Mngeta nikitokea Kilimanjaro hospitali ya KCMC. Nilijionea uzuri na utajiri wa rasilimali mbalimbali ikiwemo ardhi yenye rutuba sana Wilayani Kilombero. Kilichonishangaza sana ni kuwa watu wa maeneo hayo wako nyuma sana kimaendeleo.Ukosefu wa miundo mbinu ya uhakika ikiwem barabara, ndiyo sababu kubwa inayochangia haya yote.Lami inaishia Ruaha darajani tu tokea mikumi na ilijengwa wakati wa M bunge aitwaye Gulamali na tokea hapo hakuna jitihada za makusudi zilizofanyika mpaka sasa kuboresha miundo mbinu hiyo.Wenyeji wa huko wanalalamika sana kuwa licha ya Mngeta kuwa ni kitovu cha uzalishaji mpunga na licha ya umeme wa kihansi kupitisha nguzo kijijini hapo lakini hakuna umeme wala nini!! M bunge wao aitwaye Abdul Mteketa hana hata chembe ya jitihada kuboresha hali hii!!!! Anaona sifa kuimbwa kwenye vyombo vya muziki eti Pedejee Abdul Mteketa!!! Sasa wanasema wananchi wa huko kuwa asubiri 2015 !!!! Atakuwa pedejee zaidi!!!!

Kama hujui mambo usiwe muongo kaa kimya ..lami ilijengwa wakati wa kuninafrisha kiwAnda cha sukari na by then gulamali alikuwa kishakufa....halafu hata hivyo lami imo upande wa kilosa sio kilombero...mkome kuchagua ccm
 
Nakumbuka mwaka 2010 mwezi wa Oktoba, Mkuu wa Kaya alifika kijiji cha mngeta kwa ajili ya kutembelea mashamba ya Kilombero Plantations Limited. CEO wa kampuni hiyo alimueleza mkuu tatizo la barabara, na jamaa akaahidi kulishughulikia. Lakini mpaka leo, yakaribia miaka mitatu, hakuna lililotekelezwa katika uboreshaji wa barabara ya Ifakara - Mngeta (Mlimba)
CEO wa KPL alimwambia Kikwete kuwa ameshaahidiwa mara nyingi lakini hakuna utekelezaji na ameanza kupoteza imani na serikali ya TZ katika kutimiza ahadi.
Mpaka leo, mbunge ndo anazidi kunenepa (suruali anavalia tumboni), hakuna maendeleo yoyote jimboni.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Bwana Fredito unaonekana ni mpembuzi Yakinifu na umelitizama suala hili kwa jicho la uhakiki zaidi! Mkuu wa Kaya alienda kule Mngeta na akatoa ahadi kibao kwa wananchi wa kule akiwa na huyo mvalia suruali tumboni. Ilikuwa ni jukumu la huyo mbunge kufuatilia ahadi za rais ili zitimizwe lakini mpaka leo hajafanya hivyo na kazi ni kukesha kwenye shoo za Akudo impact! Mngeta inalima zaidi mpunga kuliko sehemu zingine za wilaya hiyo ikiwa na kampuni ya KPL ambayo kwa sasa ndiyo inayozalisha mpunga kitaalamu. Mlimba ndiyo ianayozalisha umeme wa kihansi ambapo ili mtu afike huko ni lazima apitie Mngeta. Mbingu ni mzalishaji mkubwa wa ndizi( tandale) na ni njia hiyohiyo ya Mngeta. Inatia huzuni sana tena sana kuona kuwa srikali ya CCM na wa bunge wake dhaifu leo hii hawajaona umuhimu wowote wa kuboresha miundo mbinu ikiwemo barabara na hata umeme kwa wanachi wa huko ili angalau nao wajione kuwa ni sehemu ya nchi hii. Badala ya mbunge kutoa hoja amekuwa akisimama bungeni kushabikia timu ya Simba kwakuwa alikuwa mchezaji huko. Toka aingie bungeni hajaweza kutoa hoja hata moja yenye nguvu kutetea jimbo lake! Kwakweli jimbo hili 2015 linaenda CDM!!!!!
 
Lami kuwa upande wa Mikumi pekee inaonyesha jinsi M bunge wa upande wa pili alivyodhaifu sana!!!Anashindwa nini mpaka sasa kuendeleza lami hiyo kuvuka pale Ruaha ikaenda mbele zaidi? Wewe unaonekana ni kada la CCM ndo maana una sympathize na situation iliyoko! Hamuoni huruma kwa Wa tanzania waishio kule? Au mpaka itokee siku watu wa Mngeta washikilie nguzo za umeme wa gridi ya taifa na kuziangusha ili wapate haki yao kama wanavofanya wanamtwara?
 
mie si mshabiki wa mteketa lakini kumrushia mtu lawama na kumponda bila facts si kitu chema.....

mix with yours
 
Back
Top Bottom