Mbunge Fatuma Jehow adai watamwibia kura Rais Ruto 2027

Mbunge Fatuma Jehow adai watamwibia kura Rais Ruto 2027

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mbunge wa Viti Maalum Kaunti ya Wajir, Fatuma Abdi Jehow, amenukuliwa na Buzzroom Kenya akisema kuwa endapo Rais William Ruto hatopata kura za kutosha mwaka 2027 katika eneo la Kaskazini Mashariki (North Eastern), basi watamwibia kura ili ashinde.

Katika kile kilichoonekana kama kauli ya mzaha lakini yenye uzito kisiasa, Jehow alisema:
“In North Eastern, if President William Ruto will not get enough votes in 2027, we will steal for him.”

Kauli hiyo imezua gumzo mitandaoni, huku watumiaji wengi wakieleza wasiwasi wao juu ya uaminifu wa mchakato wa uchaguzi na nidhamu ya viongozi wa umma. Wengine walichukulia kauli hiyo kama kejeli au utani usiofaa kutoka kwa kiongozi wa kisiasa.

Hadi sasa, Fatuma Jehow hajatoa ufafanuzi au kujibu kwa kina kuhusu kauli hiyo iliyonukuliwa na Buzzroom Kenya.

BuzzroomKenya​
 
Juba kubwaaa, lakini anaongelea wizi, mali zinatutia upofu.
 
Back
Top Bottom