MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Naona utakua Kingu wewe! Unajitekenya na kucheka mwenyewe. Kwanza rudisha zile pesa ulizokopa ukasababisha Viongozi wa dini wakatiwa ndani, Rudisha zile mil 90 ulizokula kule Igunga! Usidhani tumenyamaza hatujui uliyoyafanya Wakati wa kampeni, uliweka jimbo rehani kwa kukopa pesa ukawagawia Viongozi wa UVccm BODABODA kila kata ukawa unadaiwa kila kona ukawa unajificha,usitakae kujitaftia Kiki humu,Umesababisha uhasama kwa vijana wa Kinyaturu mpaka sana wanachukiana kwa sababu yako.Wa kukataa posho sio wewe Kingu tuna kujua.Uliutaka ubunge kwa ulaghai wote ulioufanya na Sasa tulia usiibue mengine hata JK anajua utapeli wako.Moja wa vijana anayemake headlines kwa sasa ni mbunge wa Singida Magharibi Ndg. Elibariki Kingu ambaye kwa mara ya kwanza kawa mbunge kutoka CCM anayepinga uwepo wa posho za laki 3 (300,000) kwa siku kama sitting allowance...
Mh. Kingu kafanya uamuzi huo ikiwa ni kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dr. John Magufuli kama moja ya njia ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na fedha zinazopatikana kupelekwa katika huduma kwa wananchi...
Mytake:
Kwa kauli moja lazima tumpongeze mbunge kama huyu. Tena anayetokana na chama cha mapinduzi... Huu ni uzalendo wa hali ya juu!...
Na kashauri kama wabunge wengine wanataka hizo posho kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wao basi wakubali fedha hizo zipelekwe moja kwa moja kutunisha mfuko wa jimbo.. Na sio kuwapa mkononi..