Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,429
MBUNGE CHEREHANI AISHUKURU SERIKALI UTEKELEZAJI WA MIRADI USHETU
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwakutoa kiasi cha Sh bilioni 196 iliziweze kusaidia miradi ya kimkakati iliyokuwa imeshindika kukamilika.
Cherehani amesema hayo Aprili 10,2025 Bungeni jijini Dodoma.
"Nikupongeza sana waziri wa maji Jumaa Aweso kwa kuweza kutupatia kiasi cha shilingi bilioni 44 iliziweze kukamilisha mradi wa maji na hii imetokana na yeye kufika jimboni kwangu nakuona akina mama wanavyoteseka kilimo cha maji kwani mradi kutoka ziwa Victoria kuja mji wa kahama umekaa zaidi ya miaka 19 bila kukamilika lakini leo umekuja kutibiwa na rais wetu,"
Pia, Amempongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuzunguka nchi nzima kuhamasisha vyama vya ushirika hadi sasa tayari vimeimarika kwani tangu kubadilishwa kwa jina la shileku hadi Simko kimefanikiwa hadi kupata mkopo zaidi ya bilioni 6 kutoka benki ya kilimo (TADB) na kununua pamba safi kutoka kwa wakulima na vyama vingine vikiendelea kunufaika.
Cherehani amempongeza pia Waziri wa Kilimo Hussein Obama kwa jitihada zake katika sekta ya kilimo kwani anakwenda kufanikisha kuzinduliwa kwa benki ya Taifa ya kilimo inayotajiwa kuzinduliwa Aprili 28 mwaka huu.
Ameongeza kuwa suala la upatikanaji wa mbolea na ruzuku limeimarishwa kwa kiasi kikubwa na tayari shilingi bilioni 13 zimekwisha tolewa kwa wakulima wa tumbaku na tayari wanunuzi 15 wapo nchini kununua tumbaku hiyo kwa wastani wa dola 2.
Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya barabarani kwakutoa Sh bilioni 18 zilitengwa ilikukamilisha ujenzi wa madaraja hayo na kuondoa vifo vya watu nakuomba kukamilishwa kwa barabara yenye kilometa 54 ambayo inatoka nyanekwa -Kahama kwani ndo kiungo muhimu cha wafanyabiashara.
Pia aliishukuru wizara ya nishati kwa kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi pamoja na mafuta.