PAMOJA na kusudio la kuongeza posho za wabunge kupingwa na vyama vya siasa, viongozi
wa dini na jamii, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) mkoani Rukwa, Anna Malack ameamua
kutetea kusudio hilo.
Mbunge huyo amesema kuwa wabunge walio wengi wanaishi maisha magumu kupindukia wanapohudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma kutokana na alichoita ukata mkali unaosababishwa na malipo duni wanayolipwa bungeni.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Mji wa Mpanda baada ya madiwani hao kutoa ombi kwa Serikali ifute kabisa posho mpya za vikao vya wabunge.
Madiwani hao katika ombi lao waliitaka Serikali, badala ya kuongeza posho za wabunge,
iboreshe posho za madiwani ambazo walidai ni duni na zimepitwa na wakati.
Wakati wa kujadili suala hilo, baadhi ya madiwani walilaani uamuzi wa wabunge kutaka kujiongezea posho ya vikao wawapo bungeni kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000 wakidai kuwa ni uamuzi wa kilafi, tamaa na ubinafsi unaowasukuma wabunge hao.
Hata hivyo, baada ya madiwani hao kutoa ombi hilo na maneno ya kulaani kusudio hilo, Mbunge huyo aliamua kueleza alichoona kuwa ndiyo hali halisi.
Kama si kulima vitunguu mie na mume wangu, ningetegemea mshahara wa bungeni, ningekuwa nimeadhirika ile mbaya baadae mtu unajuta kwanini umeingia kwenye siasa.
Mfano unaamka asubuhi unafungua mlango na kukuta watu zaidi ya hamsini wanakusubiri wakiomba uwasaidie baadae unalazimika kuuza vitu vya ndani ili uwasaidie.
Ukifika nyumbani kwangu sina lolote zaidi ya kukutana na harufu kali ya vitunguu, huwezi
kuamini kama ni nyumba ya mbunge wenu.
Wabunge kwa hali hiyo tunaadhirika, kama huna miradi ya kujiongezea kipato ndio umekwisha, alisema.
Alisema kutokana na ukata baadhi ya wabunge wamekuwa wakikacha kurejea kwenye majimbo
yao ya uchaguzi na badala yake wanaamua kukaa Dar es Salaam.
*Hajapokea lakini anazitamani
Mbunge huyo alisema kuwa yeye binafsi hajawahi kulipwa posho mpya ya vikao vya Bunge na
kuongeza kwamba ofisi ya Bunge imekuwa ikiwazungusha kuwalipa na kusababisha afulie ile mbaya.
Nadhani watu hawaelezi ukweli, malipo ya posho hizo mpya ni blaa blaa tu kwani mie binafsi sijawahi kulipwa hata siku moja isitoshe nimekuwa nikisoma kwenye magazeti na kusikia kwenye vyombo vingine vya habari.
Labda kama ofisi ya Bunge imebagua na kuwalipa wabunge wengine watueleze tujue, alisema.
Alidai kutokana na kutolipwa hiyo posho mpya wamepigiana simu na wabunge wengine na wamekubaliana kufanya mgomo wa kutoingia bungeni katika mkutano ujao wa Bunge hadi wafahamu hatima ya malipo yao.
Bila kuwataja kwa majina wapo baadhi ya wabunge kutokana na ukata wanashindwa
kulipia nyumba za kulala wageni, wanalazimika kulala kwenye magari yao huku suti zao zikiwa zimetundikwa kwenye kiti cha nyuma, amini usiamini wanalia kama watoto wadogo, alisema.
Akiunyambulisho mshahara wake alisema kama Mbunge analipwa Sh 70,000 za posho na
mshahara wake ni Sh 2,500,000 lakini baada ya makato anasalia na Sh 800,000 tu.
Makato hayo ni ya gari nililokopa na makato mengineyo hivyo nimefulia ile mbaya nikisafiri na gari langu kutoka Mpanda hadi Dodoma natumia Sh 700,000 kwa mafuta tu, alisema.
Madiwani wakaza uzi Hata hivyo madiwani hao bila kuuma uma maneno, walimtaka mbunge huyo akienda bungeni atoe shilingi kwenye mshahara wa waziri husika akishinikiza posho za madiwani ziboreshwe.
source : Habarileo.
my take SIJAMUELEWA MWANDISHI WA HABARI HII