Mbunge Blandes kalidanganya bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Blandes kalidanganya bunge

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Kamakabuzi, Nov 16, 2011.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nimeongea na watu wengi wa Karagwe kuhusu kauli aliyosema bungeni mbunge wa Karagwe Blandes kuwa wananchi wa Karagwe wamemtuma kuwa wanakubali muswada wa tume ya katiba uliopo bungeni upite kama ulivyo, nao wamesema hawajawahi kumtuma chochote juu ya suala zima la katiba mpya.
  Tangu mjadala wa mchakato wa katiba uanze wananchi wa Karagwe hawajawahi kuulizwa maoni yao na walikuwa wanamsuburi huyo mbunge awaeleze kama wao ni sehemu ya Tanzania au la kwa maana mwezi april muswada ulijadiliwa dsm, dodoma, na zanzibar kana kwamba tanzania nzima ni maeneo hayo matatu tu!
  Wakati wanasubiri aje kujibu hoja hizo alishindwa kufanya hivyo kwa kusingizia eti hatakuwa na muda kwa sababu ya kuwa kwenye kamati ya bunge juu ya sakata la Jairo. Hivyo hakuzungumza na wananchi hao juu ya katiba.
  Tangu hapo hajawahi kuja kuzumgumza na wananchi; wananchi wanasema hivyo kwa sababu pale alipokusudia kuja redio za wananchi (Radio Karagwe na Radio Fadeco) zilitumika kuwatangazia ujio wake na ratiba kamili, na tangia hapo hawajawahi tangaziwa kuwa mbunge atafanya ziara yoyote, hadi muswada ukapelekwa bungeni kusomwa kwa mara ya pili.
  Kwa hiyo wananchi wa Karagwe hawajawahi kujadili muswada huo na mbunge wao, na wala hawajawahi kumtuma akubali muswada wa sasa.
  Tunamtaka Blandes afute kauli yake haraka iwezekanavyo kwa amesema uongo bungeni na amewasingizia wanachi wa Karagwe mambo ambayo hawajafanya. Kama hataki kufuta kauli yake na kuwaomba msamaha wananchi hao, basi athibitishe ni kikao gani cha wananchi kilichokaa kuzungumzia katiba na kikaazimia kumtuma akubali muswada.
  Great thinkers, suala la katiba si sawa na suala na barabara au maji au umeme ambalo mbunge anaweza tu kusema wananchi wangu wanataka.......!
  Kwa kuwa najua Blandes hatafuta kauli yake kutokana na jeuri ya ccm, naomba mwongozo wa hatua za kisheria kumshtaki mbunge huyu, kumkataa ili uitishwe uchaguzi mwingine.
   
 2. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kauli za ushabiki zitamgarimu anamaanisha wananchi wake ndo hawapendi haki ya tume huru! utajuta wameshakushtukia na vipesa vya vitumbua ulivyoahidiwa kupitisha mswaada
   
 3. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hata Rage jana amelidanganya bunge. Eti wananchi walikuwa wanajadili kwenye redio.
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,004
  Likes Received: 3,189
  Trophy Points: 280
  Hata Kilango alisema alitumwa na wana same.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nimeongea na madiwani watatu ambao nimeweza kupata namba zao, wote wanasema hakuna walikokaa na kumtuma jambo hilo - kwanza haonekani hata kwenye vikao vya madiwani. Nafuta namba yake ya simu nimtwangie
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,770
  Trophy Points: 280
  Wabunge wengi wa CCM wanapochangia kuhusu jambo hili la mswada wanasitisha huduma ya kuwawakilisha wananchi waliowapa kura na kugeuka kuwa wawakilishi wa mafisadi kwa kulazimisha madaraka makubwa kwa rais ambayo ni dhahiri ndio yamepelekea taifa hili kuzama kiuchumi kwana madaraka haya makubwa ya rais yanayotetewa na wabunge hawa wa CCM yamemfanya raisi kushiriki ktk ufisadi na kuwalinda mafisadi tanzania.
  Tanesco arusha asanteni kwa kutukatia umeme.
   
 7. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Madiwani hao wamsubiri kwenye vikao vyao ili wambana na aseme waliomtuma.
   
 8. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama walinunua hizo kura unadhani watasemaje? Tutaona mwisho wake
   
 9. Akami

  Akami Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Blandes atuombe radhi,binafsi sikuwahi kusikia wala kuona akifanya mikutano na wananchi na kutueleza kuhusu katiba,aache kujipendekeza.Kama vipi tutakutana 2015 atakapokuja tena kutuomba kura!Atueleze ni lini na wapi tulimtuma,aache kutudhalirisha,Wanyambo ni watu makini sana hatuwezi kumtuma upuuzi kama huo
   
 10. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wengi ni waongo sana. Hata wale wa ZNZ eti nao wanasema wananchi wao wamewaambia wanapenda Muungano na wanaunga pumba wanazoendesha sasa mjengoni
   
 11. E

  Echikaka Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hawezi kurudi nyuma ila kwa nguvu ya umma(cdm)atajuta
   
Loading...