Mbunge aweka kando ubunge, afanya kazi ya kutoa `uchawi` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge aweka kando ubunge, afanya kazi ya kutoa `uchawi`

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAGEUZI KWELI, Mar 9, 2012.

 1. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,932
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  NA THOBIAS MWANAKATWE
  9th March 2012

  [​IMG]
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani


  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, juzi aliweka ubunge wake kando na kurejea kazi yake ya uganga kwa kutoa ‘wachawi' katika kijiji cha Kwemazandu.

  Mbunge huyo alifanya kazi hiyo baada ya kuhudhuria mkutano wa kijiji uliopitisha maamuzi ya kumtimua mmoja wa wanakijiji wao kwa tuhuma za kishirikina.

  Akizungumza na NIPASHE kwa simu kutoka Korogwe, alisema alilazimika kufanya kazi hiyo wakati wa mkutano wa halmashauri ya kijiji ambao pamoja na mambo mengine, ulijadili suala la kijiji hicho kukosa mvua kwa kipindi kirefu.

  Kufuatia kutonyesha kwa mvua hiyo, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakimtuhumu mkazi mwenzao, (jina limehifadhiwa) kwamba amekuwa akijigamba mitaani kuwa mvua kijijini hapo haitanyesha.

  Baada ya wajumbe wa kijiji kuchangia kuhusu suala hilo, ndipo mbunge alipoondoka huku akiongozana na wajumbe hao pamoja na wananchi waliofurika kumwangalia, wakielekea katika nyumba ya mtuhumiwa huyo kwenye kitongoji cha Kimunyu.

  "Jamani mnakumbuka kwenye kampeni nilivyosema, napenda niwakumbushe, nilisema kazi ya ubunge ni ya miaka mitano lakini kazi yangu ya uganga siwezi kuiacha nitaifanya hadi nitakapokufa," alisema Profesa Majimarefu.

  Mbunge huyo baada ya kueleza hivyo aliongozana na mwenyekiti wa kijiji hicho, mtendaji wa kijiji na mwenye nyumba hizo kuingia nao ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.

  Baada ya kuingia katika nyumba hiyo, Profesa Maji Marefu alitoka akiwa na tunguri mbalimbali zilizodaiwa kumilikiwa na mtuhumiwa huyo.
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,200
  Likes Received: 1,386
  Trophy Points: 280
  u ikawaje, mwisho wake ilikuwa nini?
   
 3. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 2,960
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hawa ndio watutunaowategemea watuwakilishe na kutunga sheria bado wanaamini mambo ya kichawi?
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 4,961
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Kudadeki malizia sasa ishiiiiii??!!!!...............baadae mvua ilinyesha au?
   
 5. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,543
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Dah.....................! Hivi mpaka lini watz tutaongozwa na hawa wachawi? Ni bora tupate kiongozi ambaye ni mchungaji, padri au shehk kuliko kuwachagua wachawi wakatuwakilishe bungeni, Alafu wa2 wa pwani mnachekesha sana kwa kuamini imani potofu zay hadi leo hamfanyi mabadiliko ya kisiasa uchumi na kijamii.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,384
  Likes Received: 1,362
  Trophy Points: 280
  Karne ya 21 tunafanya hivi!!! Hivi haya mambo kikatiba yameekaje?
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 8,526
  Likes Received: 1,694
  Trophy Points: 280
  Halafu huyo Mbunge ndiye mjumbe wa kamati ya Afya!!
   
 8. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Dr Ngonyani saidia Muhimbila watu wanakufa jamani
   
 9. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,355
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Duh, kumbe Profesa anatembea na 'mikoba' yake kila mahali!
   
 10. G

  Gaza Senior Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 101
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,513
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  duh! Ndo wabunge wetu hao! Akili zako changanya na zake!!!
   
 12. G

  Gaza Senior Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 101
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 20,627
  Likes Received: 3,131
  Trophy Points: 280
  Ha ha haa...kaka mkuu wa nchi mwenyewe yumo...
   
 14. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 9,871
  Likes Received: 2,078
  Trophy Points: 280
  Ni mjumbe wa kamati ya ufundi ya timu ya soka ya wabunge !!!
   
 15. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,687
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  hawa ndio wwatunga sheria wetu.
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,047
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  acha tu babangu.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 34,632
  Likes Received: 11,560
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio la huyo mbunge..tatizo ni wananchi wenyewe na eneo analotoka huyo mbunge.wlimu haijawasaidia ipasavyo.
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,047
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Fani haipotei.
   
 19. v

  valid statement JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,732
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pale jumba la magogoni akiingia hatakuta vitu kama hivi kweli pale?
  Sipaamini kabisa.
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,341
  Likes Received: 993
  Trophy Points: 280
  kazi tunayo mbona
   
Loading...