Mbunge ataka apangiwe vipindi afundishe sekondari

Mbunge ataka apangiwe vipindi afundishe sekondari

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
upload_2017-8-11_13-0-39.jpeg


MBUNGE wa Serengeti, Marwa Ryoba, ameutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari Serengeti kumpangia vipindi aweze kufundisha wanafunzi wa shule hiyo masomo ya sayansi anapokuwa mapumziko, anaripoti Malima Lubasha.

Ryoba alisema hayo wakati wa makabidhiano wa msaada wa madawati na magodoro yaliyotolewa na kampuni inayojishughulisha na utalii ya Grumeti Reserves Fund.

Alisema amechukua hatua hiyo baada ya kuridhishwa na matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka huu ambako wanafunzi wote 48 wamefaulu, daraja la kwanza wakiwa 12, daraja la pili 34 na la tatu wamefaulu watatu.

Chanzo: Mtanzania
 
Heko kwake, ila ingekuwa poa sana akaacha siasa kabisa akaanza kufundisha
 
Vyema sana.Angetafuta na kijana wa kumshikia vipindi wakati wa vikao vya bunge ili nguvu kazi ibaki sawa na alipo kuepo.

mafisadi hayana rangi
 
Ana taaluma ya ualimu na kama anao je katika hatua gani maana mashule yana ithibaki yake siyo kwa kuwa ni mbunge useme unaweza kufundisha na kama una vigezo vyote basi kuna taratibu za kuomba kazi siyo unajisemea tu,hizo ni kazi maalum na watu wamesomea
 
alikuwa na wazo zuri lakini sasa ambacho ameshangaza ni kutaka kufundisha katika shule ambayo tayari ina walimu na wanafanya vizuri. nlitegemea kama ana nia hiyo angeenda shule ambayo haina walimu wa sayansi ili sasa aisaidie ifanya vizur. but si kwa shule ambayo tayari ina mwelekeo mzuri au inafanya vizuri tayari.
 
Serengeti siku hizi ina kidato cha tano na sita?

Nakumbuka miaka ya mwanzoni ya 2000 shule ilikua na watoto wakorofi sana na wasio na akili kabisa.

Kuna shule nyingine inaitwa Kambarage nadhani, yenyewe ilikua na majambazi na wezi wa ng'ombe, hakuna aliekua anafaulu mitihani.

Aisee. Miaka mingi.
 
Alisema amechukua hatua hiyo baada ya kuridhishwa na matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka huu ambako wanafunzi wote 48 wamefaulu, daraja la kwanza wakiwa 12, daraja la pili 34 na la tatu wamefaulu watatu.

  • Anaomba kupangiwa vipindi na wanancnhi au na mpanga vipindi shuleni?
  • Anaomba kupangiwa vipindi baada ya kuona matokeo mazuri, kwanini hakuomba kupangiwa vipindi wakati matokeo yakiwa kinyume ili kuudhihirishia umma kuwa yeye ni mwana mabadiliko amefanikiwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi?
 
Back
Top Bottom