Mbunge anapofutwa uanachama je anavuliwa ubunge mara moja au mpaka akate rufaa akishindwa ndio anavuliwa ubunge?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Wanasheria wetu naomba Ufafanuzi katika hili Jambo.Binafsi pamoja na Elimu ndogo niliyonayo na uzoefu wa matukio yaliyowahi kutokea naamini Mbunge anapofukuzwa Uanachama anakuwa amepoteza Sifa ya kuwa Mbunge kwa Mujibu wa Katiba ya Nchi hivyo Spika anapopata Taarifa ya Maandishi kutoka Chama husika humvua Ubunge Mbunge huyo.

Yametokea kwa Wabunge wa CUF na Mama Sophia Simba Wa ccm wote hawa Walifukuzwa Uanachama na vyama vyao Spika akawavua Uanachama mara tu alipopata Taarifa ya Maandishi kutoka Vyama husika.
SUALA LA RUFAA Ya Kupinga Kufukuzwa Uanachama.

kwa Uzoefu wangu mdogo RUFAA ya Kupinga kufukuzwa Uanachama hukatwa wakati Tayari Umekwisha Vuliwa UBUNGE na sio vinginevyo kwani ili Uutetee Ubunge wako sharti uanze na Uanachama.

Swali la msingi
Je ni Wakati gani Mbunge anavuliwa Ubunge wake je ni baada ya kufukuzwa Uanachama au baada ya rufaa ya Kupinga kuvuliwa kusikilizwa na kushindwa?

Nawaomba Wanasheria wetu tupeni Elimu kwani kuna hili SAKATA la Halima na Wenzake 18 Mahakama imethibitisha kuwa Sio Wanachama lakini Wapo Bungeni wakati KATIBA ipo wazi kuwa Huwezi kuwa Mbunge bila Chama.

Suala la Rufaa yao kupinga Kufukuzwa UANACHAMA ilipaswa Waikate wakina wanevuliwa Ubunge Kama tulivyoshuhudia kwa Wabunge wa CUF na Ccm .

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Ngonjera inaebdelea mpaka bunge kitavunjwa na hao hao 19 watarudi katika bunge lijalo
 
Back
Top Bottom