Mbunge amtaka Rais Magufuli kumuiga Kenyatta na kuruhusu maandamano

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania kupitia CHADEMA, Godbless Lema amemtaka Rais John Pombe Magufuli kumuiga mwenzake wa Uhuru Kenyatta kupitia kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo, kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.

Akihutubia mkutano wa umma katika wadi ya Murieti, Lema alimsifu Rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda

Kulingana na gazeti hilo, Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinzani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.

Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.

''Demokrasi ni swala tata, mara nyengine linaweza kuathiri uchumi. Wawekezaji wengi huchunguza kiwango cha demokrasia katika taifa kabla ya kuwekeza. Iwapo tutaendelea na mkondo huu basi utatukwaza katika siku za usoni'', alisema.
Magufuli.jpg
 
inasikitisha sana ,maana kama ni kunyoosha nchi anaweza nyosha kwa misingi ya katiba na sheria za nchi .
 
Yaani huyu jamaa huwa anasema Katiba kwake si lolote wala chochote..........

Badala yake eti yeye priority no 1 kwake ni kuinyoosha nchi!

aibu sana kama anasema katiba si lolote , hajui kuwa ndo inampa kiburi akijua hawezi shitakiwa maana ana kinga ya kikatiba?
 
Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania kupitia CHADEMA, Godbless Lema amemtaka Rais John Pombe Magufuli kumuiga mwenzake wa Uhuru Kenyatta kupitia kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo, kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.

Akihutubia mkutano wa umma katika wadi ya Murieti, Lema alimsifu Rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda

Kulingana na gazeti hilo, Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinzani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.

Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.

''Demokrasi ni swala tata, mara nyengine linaweza kuathiri uchumi. Wawekezaji wengi huchunguza kiwango cha demokrasia katika taifa kabla ya kuwekeza. Iwapo tutaendelea na mkondo huu basi utatukwaza katika siku za usoni'', alisema.View attachment 569782

Hajitambui wala hana ufahamu. Nchi za dunia hii ni tofauti kiutamaduni, kimaendeleo, kisiasa nk. Hivyo mambo ya Kenya huwezi kutaka yawe sawa na Tanzania, au Marekani, au China, au Somalia, au Brazil au Urusi au Mexico etc.
Lema anatakiwa akafundishwe na aelewe hilo.
 
Back
Top Bottom